Hizi ni sababu za kwanini Askofu Gwajima anatakiwa kukamatwa na kufunguliwa mashitaka ya uchochezi

Hizi ni sababu za kwanini Askofu Gwajima anatakiwa kukamatwa na kufunguliwa mashitaka ya uchochezi

Ndugu zangu Watanzania,

Kwa namna askofu Gwajima alivyotoa ,kueneza na kusambaza Maneno ,kauli na matamshi yake kutoka kwenye kinywa chake. Ni ngumu sana kuachwa hivi hivi bila au pasipo kufunguliwa Mashitaka ya Uchochezi . Kwa sababu ametoa maneno na matamshi yenye kuleta uchonganishi na yenye kuchochea wananchi kuichukia serikali yao.

Ametoa maneno na kauli zenye kujenga chuki vifuani pa wananchi na hata kuweza kusababisha vurugu na machafuko , kutokana na kauli na meneno yake yenye kuonyesha na kuleta Taswira au picha ya kuhusisha matukio ya utekeji na kikundi ambacho kwa mdomo wake alisema kuwa kina ngtuvu na kupewa nguvu kutoka juu ambako hata wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wanaogopa kukigusa.

Lakini askofu Gwajima Ameleta maneno ya uchonganishi Mkubwa sana kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama na Mamlaka ya uteuzi. Jambo ambalo linaweza kuleta chuki na vinyongo kwa askari na wanajeshi wetu kutokana na maneno ya uzushi ,uongo na uchonganishi yaliyotolewa na askofu Gwajima. Kwa maslahi yake binafsi .

Hivyo anapaswa kukamatwa haraka ,kuhojiwa , kufikishwa mahakamani na kufunguliwa Mashitaka ya Uchochezi ili aweze kujibu. Hapaswi kufumbiwa macho aendelee kuligawa Taifa,kuleta uchonganishi, uchochezi,kujenga chuki na kusambaza uongo hapa Nchini.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Sasa umejuaje amechonganisha kabla hayajahojiwa? What if akihojiwa na inaonekana alichokuwa anasema ni sahihi?

Tusiwe mashabiki tu bila kufikiri kwa kina, tusiwe tukawa ndio watengeneza chuki katika jamii
 
Back
Top Bottom