Hizi ni siasa za kilaghai zisizo na tija kwa taifa letu. Kugawa mitundi ya gesi badala ya kukomaa JNHP ikamilike ni ni kutaka kutafuta kiki zisizofaa

WaTanzania mpunguze kulalamika, dunia nzima inaongelea nishati mbadala pia Ilani ya CCM na mpango wa taifa wa maendeleo wa miaka 5 (Ambayo ndio inamuongoza Rais na Mawaziri) inaongelea energy mix sio tu kwenye vyanzo vya umeme ila hata kwenye matumizi ya nishati majumbani.

Hivyo uwepo wa Hydro Power unatakiwa uende sambamba na nishati zingine kama Joto-Ardhi, Umeme wa upepo, Gesi n.k

So kama hamtaki gesi itumike waambieni wabunge wapinge utekelezaji wa mpango wa taifa otherwise mnaongea mambo msiyokua na uelewa nayo.
 
Sikutarajia hoja nyeupe kama hii kutoka kwako mkuu.
 
Kuwahamamsiha watu watumie nishati mbadala siyo kwa maigizo hayo!

Punguza gharama za gesi na umeme uone kama kuna mtu atahangaika na kuni!

Hivi mbibi kama huyo hata nyumba yake yu unavyoiona anaweza kutoa 25 elfu kila mwezi ili akanunue gesi ya kupikia?

Ni uzwazwa,! Watu kibao wamepeleka maombi ya kuunganishiwa umeme wana miaka hata 2 hawapati huduma, gesi bei inapanda kila kukicha, sasa mwananchi gani wa kijijini ana uwezo wa kununua gesi kila mwezi?
 
Tujadili hoja, kosa la January ni lipi hapo? kusimamia Ilani ya CCM ambayo JPM aliinadi ama?? Ilani Iliongelea hayo ya gesi kutumika majumbani sasa mnapinga nini hapo?
Ndiyo maana nikaanza kwa kusema sikutegemea hoja nyeupe namna hii kutoka kwa mtu wa aina yako. Unadhani hoja ni Januari kusimamia ilani?

Hiyo unayoita ilani ni wapi inasema utakelezaji wake ni 'kugawia' wananchi mitungi?
 
Mbona hayo TPDC walishaongea kwamba wanampango wa kusambaza gesi majumbani kwa subsidized price!!

Maboresho lazima yatakuja lakini kuanza kupinga mtu kuhamasisha matumizi ya gesi ni ajabu sana.

Hata umeme enzi hizo unaletwa mara ya kwanza ulikua na gharama, in fact tulianza na majenereta huko bush linawashwa saa 12 hadi saa 4 usiku!! Lakini taratibu mambo yamebadilika na bei sio Ile ya miaka ya 90?

So kuliko kupinga kabisa mshauri njia nzuri zaidi ndio mjadala unakua na tija. Nakumbuka siku JPM anawasha umeme kwenye nyumba ya tembe mlimshangilia sana kwamba kavunja rekodi ila sikusikia mkiongelea gharama za Luku za kila mwezi kwa wananchi maskini!!! So tuache unafiki na tutoe support Ile Ile kwa huyu
 
Ndiyo maana nikaanza kwa kusema sikutegemea hoja nyeupe namna hii kutoka kwa mtu wa aina yako. Unadhani hoja ni Januari kusimamia ilani?

Hiyo unayoita ilani ni wapi inasema utakelezaji wake ni 'kugawia' wananchi mitungi?
Unapotaka kufanya promotion ya kitu lazima kuwepo na pre requisite kama market testing, feasibility studies n.k sasa kugawa mitungi Ili kuona response ya Wananchi ni kosa Gani?

Hata mwendokasi watu walipanda bure siku za kwanza sasa mbona hamkuita ni maigizo??

Hii ni promotion tu ila bigger picture ni Ilani na mpango wa taifa unaotaka waTanzania kutumia energy mix Ili kukidhi mahitaji ya nishati kwa ajili ya uzalishaji na majumbani.

Tuwe optimistic na tushauri maboresho sio kukosoa idea nzuri hivi
 
Kweli wasomi wetu ni tatizo. Huyu makamba ndio msomi wetu huyu kwa mambo hayo?. Kwa mbinu hizo ndio anataka na urais?
 
Pesa za serikali zinatumiwa na CCM kuwagawia wanaccm wa Umoja wa Wanawake! Chama kimoja kimeshika hatamu, nchi hii inawenyewe na wenyewe ni CCM.
 
Ulaya Kwa zaidi ya miaka 30 kuitegemea Urusi kama chanzo Cha Energy .

Leo Vikwazo walivyowawekea Warusi, vinaiathiri Ulaya zaidi kuliko Urusi.

JPM aliona mbali, aliona Umuhim wakujitegemea kisawasawa kwenye NISHATI.


ila kwakua sahizi tunaongozwa na Rais wa aina ileeee, anayeweza Vijana wake wa aina ileeee , Usisashangae sahizi hata huko NSSF Wamejazana wale Vijana wa Mjomba, Shangazi.....


Unategemea nn?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…