Hizi ni Sifa za wadada wanaoishi peke yao; Je wewe unaijua ipi

Hizi ni Sifa za wadada wanaoishi peke yao; Je wewe unaijua ipi

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Hizi ndizo sifa za wadada wanaoishi peke yao, zikiangazia tabia na maisha yao ya kila siku kwa njia ya utani na ukweli wa mitaani.


Hawapendi Wageni: Akija mgeni ananuna na kufikiria ni saa ngapi ataondoka ili arudi kulala au kuangalia muvi.
  • Kupika Mpaka Njaa Ikaribie Kuwaua: Mara nyingi hawapiki; hula viporo au kusubiri mpaka mwili utetemeke kwa njaa ndipo wapike.

  • Kuamka ni Saa 7 Mchana: Kitu kinachowaamsha ni njaa kali au sauti ya mtu wa taka, na bado wanaweza kugoma kuamka.

  • Hawapatani na Mwanga: Hata ikiwa ni saa 8 mchana, ndani utadhani ni saa 3 usiku kwa sababu madirisha, milango na mapazia vyote vimefungwa.

  • Muda Wote Wamejifungia Ndani: Anaweza kujifungia ndani hadi majirani wakadhani hayupo na kuanza kumsema, kumbe yupo ndani anawasikia.

  • Kuosha Vyombo ni Mpaka Akose Cha Kupikia: Vyombo havioshwi kwa wakati labda akose kabisa chombo safi cha kutumia.

  • Wana Boda Boda Wao: Kazi kubwa ya bodaboda wao ni kuwaletea oda za chipsi au zawadi kutoka kwa wazazi/marafiki.

  • Ukibisha Hodi Hawafungui: Anajua sauti zote za wanaogonga; kama hataki kukufungulia, huwezi kuingia labda ubomoe mlango.

1789546208701.png
 
Nadhani tujifunze kutofuatilia maisha personal ya mtu as long as hayakuathiri wewe kwa vyovyote vile... Acha watu waishi wao wanaona vile inafaa... Umaskini, wivu, idleness ,na chuki ndio vinafanya tunafuatilia maisha ya wengine
 
Back
Top Bottom