Yah nadhani sisi wote ni wapenda mziki mzuri so tuenjoy mziki mzuri na sio kwa kukashifiana. Nyimbo za kifo zinaishi haswa zile zisizo mtaja mtu moja kwa moja. Mfano Kifo wa Rayvanny ni mzuri ila amemuimbia Magufuli moja kwa moja so ukipigwa kwenye msiba say wa Mengi haitapendeza kivile.
Nyimbo alizotaja mtoa mada nyingi waliimbiwa watu ila ni general sio specific ingawa kuna watu wanatajwa lakini kiaina sana sio moja kwa moja mfano wimbo wa kazi yake mola wa Madee aliimbiwa Abdul Bonge na ule wimbo wa Tutakukumbuka wa GK aliimbiwa jamaa wa Kwanza Unit ila walitajwa kidogo na maudhui ya nyimbo yalikuwa general.
Ushauri kwa wasanii wetu: Ukiimba nyimbo ya kifo jaribu kuifanya iwe general na sio specific kwa mtu fulani. Siku hizi wasanii wanaimba na technology inawabeba sana wanamuziki, watupe vitu bora vinavyoishi
Bonus truck
Sikilizeni wimbo wa Nas f/ Quan - Just a moment