Hizi online companies za kukopesha pesa!

Hizi online companies za kukopesha pesa!

mimiamadiwenani

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
5,718
Reaction score
7,784
Habari!
Hapa tunazungumzia PesaX, FiniLoan na kadhalika. Hizi ni online platforms ambazo zinajinadi kuwa zinakopesha pesa.

Vigezo vyake huwa ni namba au kitambulisho cha NIDA, leseni ya udereva, kitambulisho cha mpiga kura, au cha utaifa.

Nina maswali mengi sana. Hizi platforms zinapata faida?
Ni biashara nzuri?
Changamoto zake ni zipi?

Kwa sasa zimekuwa trending mno. Ukiingia facebook basi 56% ya ads ni za mikopo. Naombeni ufafanuzi zaidi. Huenda nikawa interested kuanzisha biashara hii mbeleni.

Ahsanteni sana!
 
Unakopeshwa 50elfu,unatumiwa 37elfu,unaambiwa ulipe 63elfu ndani ya siku 8.

Maana yake ni kwamba,watu 2 wakilipa madeni yao ya elfu 63 wameishalipa hasara ya mtu mmoja na nusu.
Watu 3 wakilipa wameshafidia hasara ya watu 2 ikiwa hawatalipa.ndio maana watu hawalipii na bado matangazo ya mikopo hayakomi.
 
Halafu zote zinafanana ...

Utafikiri za mtu mmoja ...

Ukikataliwa sehemu moja basi umekataliwa kwenye Apps zote..
 
Back
Top Bottom