Hizi pangua pangua za Rais Samia kwa wateule wake kila uchao zote zina maslahi kwa taifa au kuna flip-flops?

Uliisha ambiwa pangua pangua ni mbwembwe za madaraka, au hukuelewa?
 
Naamini hao mawaziri wanakuwa na JD zao pamoja na KPI's zao, bosi wako anawapa target na kuwapima Kila baada ya muda tuseme kila robo mwaka wakishindwa kuperform bosi anazohatua zakuchukua pia.

Inapaswa kuwe na team ya vetting na team ya kumuinterview kila mtu anayeteuliwa kuwa Waziri, Rais mwenyewe anapaswa kuwa kwenye team ya interview au iwe kama Kenya hao mawaziri wanafanyainterview na team then wanakwenda bungeni interview inaendeshwa live wote tunaona.
 
Muhimu kuwe na confirmation hearing. Hapo wabunge/ kamati maalum wanapitia CV za waliopendekezwa( vetting)wanauliza maswali kwanini wanafikiri watazimudu hizo nafasi, kuangalia maadili, uadilifu wao na utendaji wao kote walipopitia hadi hapo walipo, elimu zao na kuuliza maswali popote kwenye utata na kuwapa nafasi ya kujitetea. either wanakubaliwa au wanakataliwa kutokana na hii serious vetting.

Hali ilivyo sasa ni kutoheshimu Watanzania, Wizara husika, wateuliwa wote na majukumu yao, kazi zao, utu wao na ni dharau kwa Taifa kwa ujumla hasa ukizingatia huwa hatoi sababu yoyote ya maamuzi yake.

Ina reflect vibaya sana kwenye mamlaka ya uteuzi kwamba they have no ideas what they are doing, hawana vigezo, systematic approach, due dilligence, serious vetting. Seriousness on the part of mteuzi na hayuko serious kwenye majukumu yake muhimu kama teuzi sahihi.
 
Rais alifanya makosa mapema kabisa baada ya kukabidhiwa madaraka akaanza kupambana na teuzi za Magufuli akawarudisha wahuni waliokataliwa na Magufuli ili aonekane yeye ni mwema sana kwao na kuwaondoa wachapa kazi walioteuliwa na Magufuli. Leo tunaona anaanza kuwarudisha wale aliowatumbua na badala yake anawaondoa wahuni japo bado kuna wahuni wawili (Mwigulu na Bashe), akiwaondoa hao kidooogo tutaanza kuwaelewa, hao bado kawakumbatia.
 
Sisemi mengi, ila itoshe tu kusema kwamba Hayati JPM alikuwa bonge la Rais.
Itatuchukua miaka mingi sana kama nchi kuja kumpata mwingine kama yeye.
 
 
Naunga mkono hoja, hili pia niliwahi kuliuzia humu Could there be a problem with our vetting systems? These hirings and firings hazitaonekana kama signs za incompetence on part of appointing authority?
P
 
Tija itatoka wapi wakati yeye anaamini kuwa wateule wake ni kama suti, kwamba anaweza kuwabadili apendavyo kutegemea na shughuli.
Miaka mitatu madarakani bado hajajua anataka nini.
 
P pangua pangua ni kwa maslahi ya taifa,hizo ndio hutoa nafasi kwa watu mbalimbali ikiwa ni pamoja naP.
 
Mkuu Rua, ruaharuaha , naunga mkono hoja, jambo kama hili niliwahi kuuliza Could there be a problem with our vetting systems? These hirings and firings hazitaonekana kama signs za incompetence on part of appointing authority?
P
 
Rais Samia endelee kutengeneze a Professional Cabinet, Wizara Professional kama sheria ziongozwe na Mwanasheria nguli, Wizara ya Afya iongozwe na Daktari bingwa, Wizara ya Fedha iongozwe na mchumi, Wizara ya Biashara iongozwe na mfanyabiashara etc.
Hili ndiyo la muhimu
 
naunga mkono hoja
P
 
Naunga mkono hoja。
niliuliza humu Could there be a problem with our vetting systems? These hirings and firings hazitaonekana kama signs za incompetence on part of appointing authority?
kisha nikauliza Hizi pangua pangua za Rais Samia kwa wateule wake kila uchao zote zina maslahi kwa taifa au kuna flip-flops ?.
kisha nikashauri Should We Demand More Right to Information Kwenye Teuzi za Key Posts? Ziwe Endorsed na Bunge With Security of Tenure? Mawaziri Wasiwe Wabunge?
P
 
Wanaoteuliwa wamepwaya hivyo Rais inabidi ateuteu ili muda uende maana watu ni walewale. Hii inaonyesha hitaji la haraka la KATIBA MPYA ili kuwepo na utaratibu mpana wa namna ya kupata Viongozi wa kuteuliwa na wa kuchaguliwa.
 
Kwa sasa sifa kuu ya uteuzi na hata ajira Serikalini ni UCHAWA. Hakuna cha vetting process wala sifa ya Elimu. Ndiyo maana utendaji ni hafifu katika maeneo mengi Serikalini.
 
HBD Rais Samia!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…