Hizi picha za Singapore kabla ya kupata uhuru mwaka 1965 zinemenifikirisha sana

Tanzania mpaka tupate Magufuli mwingine. Viongozi wa bembeleza bembeleza bila kukaza sauti na kuchapa viboko hawawezi kutuendeleza. Waziri mkuu wa kwanza wa Singapore ( Lee Kuan Yew) na rais wa tatu wa South Korea (Park Chung Hee) walikuwa wakali sana kwenye kusimamia serikali zao. Walichapa watu viboko sana hadi raia wakanyooka. Hadi leo ukienda Singapore ukatupa uchafu barabarani unatandikwa viboko vya papo kwa papo.

Baada ya raia kunyooka na kuwa discpline, hakukuwa na wizi wa mali ya umma wala rushwa na jamii ikaanza kukua kimaendeleo hadi leo tunvyowaona.

Rushwa na kutegemea njia za mkato mkato ndiyo sumu ya maendeleo kwa Tanzania pamoja na kuwa na raslimali nyingi. Rwanda inayoongozwa na dikteta imeashakuwa mbele yetu.
 
Jamani

Nimekutana na picha hizi za nchi ya Singapore. Nimeshangaa sana

Hivi Afrika changamoto nini? Mbona hawa jamaa walikuwa sawa kabisa na Tanzania mwaka 1965

View attachment 3572003

View attachment 3572004

View attachment 3572005

View attachment 3572006

View attachment 3572007

Singapore kwa sasa

View attachment 3572036View attachment 3572035View attachment 3572034Maendeleo hayo na neema zote ni kutokana na u.aono mazuri chini ya ongozi bora wa Mzee Lee Kuan Yew​

Tanzania mpaka tupate Magufuli mwingine. Viongozi wa bembeleza bembeleza bila kukaza sauti na kuchapa viboko hawawezi kutuendeleza. Waziri mkuu wa kwanza wa Singapore ( Lee Kuan Yew) na rais wa tatu wa South Korea (Park Chung Hee) walikuwa wakali sana kwenye kusimamia serikali zao. Walichapa watu viboko sana hadi raia wakanyooka. Hadi leo ukienda Singapore ukatupa uchafu barabarani unatandikwa viboko vya papo kwa papo.

Baada ya raia kunyooka na kuwa discpline, hakukuwa na wizi wa mali ya umma wala rushwa na jamii ikaanza kukua kimaendeleo hadi leo tunvyowaona.

Rushwa na kutegemea njia za mkato mkato ndiyo sumu ya maendeleo kwa Tanzania pamoja na kuwa na raslimali nyingi. Rwanda inayoongozwa na dikteta imeashakuwa mbele yetu.
Maendeleo hayo na neema zote ni kutokana na u.aono mazuri chini ya ongozi bora wa Mzee Lee Kuan Yew
 
Maono bila usimamizi thabiti ni kama kutwanga maji ndani ya kinu. Rais Mkapa ma Kikwete walikuwa na maono mazuri lakini hawakuyasimamia; angalau Mkapa alijitahidi lakini Kiwete hakuwa na usimamizi wowote
 
Sera ya Ujamaa ya Nyerere ambayo ilitaifisha mali za watu halafu serikali ikashindwa kuziendeleza hizo mali! Kuanzishwa kwa vijiji vya ujamaa na kuwalazimisha watu kwenda kuishi mazingira wasiyo yapenda au kuwa famliar nayo!

Kuanzishwa kwa ccm na Katiba ya 1977, nk. Kukosekana kwa viongozi wazalendo, wanamapinduzi na wenye maono ya mbali!!

Haya yote hayajaicha nchi yetu salama.
 
Wapo waislamu nguli humu jf ..unajua kwa nini awajibugi hovyo hoja zangu ujificha..? Nilisha wahi kuelezea na evidence wakakimbia ...
Kuna wakati mtu anaona mada zako hazina busara, anakuacha uandike ujinga. Sio kwamba watu hawawezi kujibu, bali mtu aliyejawa na upumbavu kumjibu ni kupoteza rasilimali mda na nishati ya akili.

Hii nchi haijalishi ni mkristo aua muislamu, wote tumechangia pakubwa kuifanya masikini. Wakristo wangapi wapo kwenye nafasi kubwa ila ni wezi, majambazi, wala rushwa na wapiga madili?
 
Halafu Singapore haina natural resources yeyote ile,

Wamedili na issue za Shipping and investing in it's human capital,rather than relying on natural resources.
 
Tanzania mpaka tupate Magufuli mwingine. Viongozi wa bembeleza bembeleza bila kukaza sauti na kuchapa viboko hawawezi kutuendeleza. Waziri mkuu wa kwanza wa Singapore ( Lee Kuan Yew) na rais wa tatu wa South Korea (Park Chung Hee) walikuwa wakali sana kwenye kusimamia serikali zao. Walichapa watu viboko sana hadi raia wakanyooka. Hadi leo ukienda Singapore ukatupa uchafu barabarani unatandikwa viboko vya papo kwa papo.

Baada ya raia kunyooka na kuwa discpline, hakukuwa na wizi wa mali ya umma wala rushwa na jamii ikaanza kukua kimaendeleo hadi leo tunvyowaona.

Rushwa na kutegemea njia za mkato mkato ndiyo sumu ya maendeleo kwa Tanzania pamoja na kuwa na raslimali nyingi. Rwanda inayoongozwa na dikteta imeashakuwa mbele yetu.
Naunga mkono hoja Mkuu,

Mabadiliko hayawezi kuja kimiujiza tu bila jamii husika kubadilika,
kiongozi anatakiwa aibadili jamii yake kifikra kwanza,mabadiliko huanza na mindset.
 
Sera ya Ujamaa ya Nyerere ambayo ilitaifisha mali za watu halafu serikali ikashindwa kuziendeleza hizo mali! Kuanzishwa kwa vijiji vya ujamaa na kuwalazimisha watu kwenda kuishi mazingira wasiyo yapenda au kuwa famliar nayo!

Kuanzishwa kwa ccm na Katiba ya 1977, nk. Kukosekana kwa viongozi wazalendo, wanamapinduzi na wenye maono ya mbali!!

Haya yote hayajaicha nchi yetu salama.
China imeendelea sana huku mashirika na makampuni yote makubwa yakiwa ni mali ya serikali. Hoja yako ni dhaifu sana. Tatizo kati ya Tanzania na China ilikuwa ni kwenye usimamizi; china mtu akihujumu mali ya umma anayongwa, Tanzania mhujumu alikuwa anahamishwa.
 
Hapo kwenye CCM na katiba yao ya 1977 hadi leo nakubaliana na wewe. CCM na genge lake wamekuwa oligarchs wa nchi hii, wameshikilia rasilimali zote za nchi, mifumo yote muhimu.
 
China imeendelea sana huku mashirika na makampuni yote makubwa yakiwa ni mali ya serikali. Hoja yako ni dhaifu sana. Tatizo kati ya Tanzania na China ilikuwa ni kwenye usimamizi; china mtu akihujumu mali ya umma anayongwa, Tanzania mhujumu alikuwa anahamishwa.
Hoja yangu haiwezi kuwa dhaifu. China ilifanya mabadiliko makubwa kwenye sera yao ya Ujamaa kwenye miaka ya 1970''s baada ya Mao Tse Dong na Waziri mkuu wake wote kufariki ndani ya muda mfupi.

Kutoka hapo serikali ya China ilitoka kwenye Ujamaa wa kihafidhina wa 1949 baada ya Mapinduzi yao ya Kijamaa, na ambao Wachina wengi walikuwa hawaupendi kama ilivyokuwa pia kwetu! Na wakaingia kwenye Ujamaa moderate wenye mchanganyiko na ubepari! Yaani viongozi walio iongoza China baada ya Mao Tse Dong miaka ya 1970's waliamua kuchukua yale mazuri ya Ujamaa na mazuri machache ya ubepari, ndiyo ikazaliwa hii China unayoina leo!

Kwa hiyo uache ubishi usio na sababu. Na wakati Wachina (role model wa Nyerere) wanafanya maboresho kwenye mfumo wao wa Ujamaa, Mzee wako Nyerere aliendelea na mfumo ule ule wa kizamani! Matokeo yake ndiyo haya sasa. Huo usimamizi ulikosekana kwa sababu ya ubinafsi na kushindwa kuweka mifumo mizuri ya kisheria kupitia Katiba, nk.
 
Tanzania nayo ilitoka kwenye ujamaa wa kihafidhina mwaka 1985; iko wapi leo? Nyerere aliondoka madarakani na ujamaa wake ukafa miaka 41 iliyopita na wewe eti bado unamlaumu leo ni Dali Ki ya ufinyu wa maono. Poland iliyokuwa ya kijamaa mpaka mwaka 1992, yaani miaka saba baada ya Tanzania kuacha ujamaa,na leo iko mbali unadhani ni kwa sababu gani kama siyo usimamizi.

Kama hujui, ujamaa wa Nyerere ndio uko China leo ila kuna fursa ya biashara binafsi huku zile kubwa zote zikiwa za serikali. Tv Hisense ni kamuni ya serikali, Kampuni ya ndege Comac ni ya serikali Makampuni 80% ya magari madogo na makubwa ni ya serikali, treni zote ni za serikali, mabenki makubwa yote ni ya serikali Makampuni ya meli yote ni ya serikali, migodi mikubwa yote ni ya serikali. Kuna tofauti gani na sera za Nyerere wakati huo na hizo za China leo
 
Tanzania mpaka tupate Magufuli mwingine. Viongozi wa bembeleza bembeleza bila kukaza sauti na kuchapa viboko hawawezi kutuendeleza. Waziri mkuu wa kwanza wa Singapore ( Lee Kuan Yew) na rais wa tatu wa South Korea (Park Chung Hee) walikuwa wakali sana kwenye kusimamia serikali zao. Walichapa watu viboko sana hadi raia wakanyooka. Hadi leo ukienda Singapore ukatupa uchafu barabarani unatandikwa viboko vya papo kwa papo.

Baada ya raia kunyooka na kuwa discpline, hakukuwa na wizi wa mali ya umma wala rushwa na jamii ikaanza kukua kimaendeleo hadi leo tunvyowaona.

Rushwa na kutegemea njia za mkato mkato ndiyo sumu ya maendeleo kwa Tanzania pamoja na kuwa na raslimali nyingi. Rwanda inayoongozwa na dikteta imeashakuwa mbele yetu.
Halafu huyu Magufuli unayemsifia angekuwa ni kiongozi makini, mzalendo na mwenye maono ya mbali! Asingewekeza kwenye kujijengea nguvu yake tu ya kiutawala, au ya kuogopwa! Kwa sababu nchi inaishi milele, ila wanadamu tunapita tu.

Alitakiwa aimarishe mifumo ya kiutawala, kisheria na kikatiba! Ili hata asipokuwepo, mifumo aliyoiacha iendelee kufanya kazi kwa manufaa ya nchi. Kwa mfano angefanikisha mchakato wa Katiba mpya ya wananchi, angezipa taasisi kama Takukuru na vyombo vingine vya dola uhuru na uwezo wa kupambana na rushwa, wezi, mafisadi, nk.
 
tofauti kuu na afrika ni moja 1 tu, singaporeans hawakuwaona wazungu maadui atleast siyo directly hivyo baada ya uhuru waliendelea kujifunza na kuendeleza yale ambayo wazungu waliyaanzisha vs afrika ilishikwa na communists akina nkrumah & co. ambao waliwaona Christians ni maadui wakaungana na muslims againsts Christianiaty na hivyo walianza ku-destroy the so called colonial legacy na kuleta uafrika ambao ni islam on steroids na msumari wa mwisho ulipigiliwa na Mugabe aliyebomoa zimbabwe iliyokuwa inafanya vizuri kiuchumi na ilikuwa ni upper middle income country iliyojitosheleza karibia kila kitu kuanzia food security mpaka energy Mugabe akaleta ukomunisti kwamba ndiyo afrika, hilo ndiyo kosa na tofauti kubwa ya kihistoria kati ya asia na afrika wote tulitawaliwa lkn waasia walikuwa clever zaidi na kuelewa.

chukulia kesi ya taiwani ambayo ilitawaliwa na japan baada ya ukoloni waasisi wao hawakuanza kubomoa misingi ya ukoloni iliyoachwa japan na wajapani walikuwa brutal kwa wataiwani lkn baada ya ukoloni taiwani wakaenda kujifunza japani siri ya mafanikio yao na ilikuwaje hadi wakaweza kuwatala, taiwani haikuanza kubomoa misingi ambayo japani iliiweka taiwani wakati wa ukoloni pia hawakuwa na muslisms hiyo nayo ni factor matokeo yake taiwani iljifunza na kufwata mfano wa "colonial master" japan leo hii taiwan iko juu.

hivyo waafrika baada ya uhuru waliungana na mulisms againsts Christiniaty na ndiyo maana afrika imerudi nyuma badala kwenda mbele, waafrika walipaswa kutambua ugomvi wa muslims na wazungu hautuhusu wanajuana wenyewe wametoka mbali na maugomvi yao na its not our problem. tusingechukuwa upande wa muslims against Christianity bali tungewaachia muslims wenyewe, najua its more complicated than that kwani communists ni wazuri sana kwenye propaganda lkn hiyo ndiyo sababu kwa nini afrika imerudia nyuma na south east asia imeenda mbele ingawaje wote tulitawaliwa ...
 
Halafu huyu Magufuli unayemsifia angekuwa ni kiongozi makini, mzalendo na mwenye maono ya mbali! Asingewekeza kwenye kujijengea nguvu yake tu ya kiutawala, au ya kuogopwa! Kwa sababu nchi inaishi milele, ila wanadamu tunapita tu.

Alitakiwa aimarishe mifumo ya kiutawala, kisheria na kikatiba! Ili hata asipokuwepo, mifumo aliyoiacha iendelee kufanya kazi kwa manufaa ya nchi. Kwa mfano angefanikisha mchakato wa Katiba mpya ya wananchi, angezipa taasisi kama Takukuru na vyombo vingine vya dola uhuru na uwezo wa kupambana na rushwa, wezi, mafisadi, nk.
kwa vile hujui jinsi Lee Kuan Yew na Park Chung Hee walivyokuwa wanaogopwa. Mfano mzuri ni Kagame hapo pembeni anvyoogopwa na unaona nchi yake inayooka baada kuchinjana mwaka 1994. Scapegoats na responsibility avoidance ni jadi yetu. Bembeleza bembelza haileti nidhamu. Jeshini ambako kuna nidhamu sana ni kwa vile makamanda wanaogopwa.
 
Tanzania nayo ilitoka kwenye ujamaa wa kihafidhina mwaka 1985; iko wapi leo?
Hapa umechanganya. Miaka hiyo unayoitaja Tanzania ilishinikizwa na IMF na World Bank kukubali masharti yao ili serikali ipate mikopo na misaada ya kifedha kwa lengo la kunusuru uchumi wake ambao ulikuwa kwenye hali tete kwa kipindi hicho, kutokana na sababu mbalimbali za kiuchumi zilizojitokeza miaka ya 1970's na hiyo 1980's!

Hayo masharti waliyopewa kupitia Structual Adjustment programmes (SAP's) ndiyo yaliyo sababisha Mwalimu ang'atuke madarakani, na kumuachia Mwinyi ambaye aliyakubali na kuyapokea kama yalivyo. Kwa hiyo hapa utaona serikali ilishinikizwa. Haikuyakubali hayo masharti kwa kupenda. Ila kwa upande wa China, wao waliamua wenyewe. Hawakushinikizwa kuchanganya mazuri ya ujamaa na yale mazuri ya ubepari ili kuupata huu muunganiko walio nao kwa sasa.
 
Jamani

Nimekutana na picha hizi za nchi ya Singapore. Nimeshangaa sana

Hivi Afrika changamoto nini? Mbona hawa jamaa walikuwa sawa kabisa na Tanzania mwaka 1965

MAendeleo kwa nchi hii yapo, tena makubwa. Angalia dsm ya mwaka 1965 linganisha na dsm ya leo.
Angalia barabara za hii nchi 1965 linganisha na barabara za kuu za leo.

Angalia huduma za kijamii miaka ya 1965 linganisha na leo. Kifupi tu maendeleo yapo ila tulipaswa kuwa mbele zaidi.
Kuna maeneo yananishangaza mpaka sasa. Huduma za maji. Hili serekali imeshindwa kwa kiwango kikubwa.

Afya. Majengo ndio mengi ila huduma kwa maana ya matibabu ni 0.

Elimu. Inachezewa. Kila waziri anakuja na sera zake za elimu. Na kwa elimu hii tunayowapa watoto wetu haiwasaidii kujiajiri au kupata ajira.
Ccm japo ni janga la taifa ila maendeleo ni makubwa kwa maana ya miundo mbinu.
 
kwa vile hujui jinsi Lee Kuan Yew na Park Chung Hee walivyokuwa wanaogopwa. Mfano mzuri ni Kagame hapo pembeni anvyoogopwa na unaona nchi yake inayooka baada kuchinjana mwaka 1994. Scapegoats na responsibility avoidance ni jadi yetu. Bembeleza bembelza haileti nidhamu. Jeshini ambako kuna nidhamu sana ni kwa vile makamanda wanaogopwa.
Mimi sina tatizo na Magufuli. Ni kweli alikuwa ni mkali. Ila ukali wa kiongozi ni vizuri ukaendana na ujenzi wa mifumo imara ndani ya nchi. Hata huu mfano wa Kagame ulio utoa, ni kwamba amejenga mfumo wa uwajibikaji, nidhamu, uzalendo nk.

Na yeye mwenyewe anahakikisha anakuwa ni mfano wa kuigwa wa huo mfumo alio uanzisha. Hata kesho asipokuwepo, ninaamini mrithi wake ataendelea pale alipoishia mtangulizi wake.

Hiki kitu kwa bahati mbaya kwenye nchi yetu hatuna. Kila kiongozi akiingia madrakani anakuja na falsafa yake.
 
Back
Top Bottom