Dhana ya "modern city" Das'lam iondoeni, there's nothing like a modern city here. Sisi tujenge tu hicho kinachowezekana kujengwa maisha yaende.
Nikupe mfano, barabara ya Morogoro kuanzia city centre inahitaji usafiri wa aina zaidi ya tatu.
1. Roads for private and public cars. Hizo barabara zilizopo, njia mbili si sawa kabisa, zinaruhusu gari kuingia na kutoka lakini hazikidhi, walau njia tatu kwa sita, tatu kwenda tatu karudi. Hii inatakiwa toka city centre hadi Chalinze.
2. Mwendokasi.
Inatakiwa ianzie city centre hadi angalau Kibaha, sio pale Kimara, another mistake.
3. Trams.
Third transport choice uwe trams pembeni ya hizi njia tatu, hizi zitakuwa slow, kubeba watu wasioenda mbali, mfano mtu hapana kimara-msugule.
4. Trains.
Kutoka city centre hadi Chalinze, ipite pembeni ya barabara kuu.
Swala la uhaba wa usafiri tutazisikia kwa jirani.
Kuna issue nyingine, stand ya Ubungo inaenda Mbezi-Kimara, wasipoweka design nzuri pale Mbezi kutakuwa na foleni ya kufa mtu, yaani foleni lote la Ubungo mataa litahamia Mbezi.
Sasa, mfano niliotoa kwa barabara hiyo, unatakiwa kutekelezwa kwa barabara zote za jiji. There we can overcome the transport issue, pamoja na kujenga ring roads, street roads na penye umuhimu kujengwe flyovers, overpass roads na interchanges.