Hizi shule za English Medium zimetugeuza Wazazi kuwa Walimu?

Hizi shule za English Medium zimetugeuza Wazazi kuwa Walimu?

Mi mwanangu ananiambia bonju mmmh nasema ndo nini hiyo?? Mother you do know bonju???
Kwishney[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Kwa mimi kifaransa tu ndo kinaniabisha ila mengine kama kawaida tu
 
Mi nimempiga mkwara akija na homework zake aje na text book ya Hilo somo coz majibu lazima yawemo umo. Maana anakawaida ya kuacha vitabu shule. Sitakangi ujinga.
Mimi nilimupa majibu ya urongo na akapewa pato! Nikagundua I am just wasting my money here, waweza jaribu pia
 
Mimi nishakataaga hizo mambo namwangalia mama yao anavopambana .
 
Kuna mtu juzi alituchekesha, alisema yeye hajasoma lazima aoe graduate aje amsaidie kufanya homework za watoto😂😂
 
Aisee hii ni shida mwanangu maswali ya darasa la pili uafikir form3 du watamuua mwanangu, kweli mtoto wa std 2 una muuliza swali la mention four symptoms of tuberculosis kweli, mpaka nikampigia rafiki yanyu doctor mana mimi nilikua najua 2 tu. Sasa sijui nasoma mimi au mwanangu
Wote. Si unaona na ww umepata kamwanga kidogo kuhusu tuberculosis [emoji848]
 
Hahahhaha mimi pia yani nasoma haswa nipo grade 1 na 3 A hatari. Ila pia jifunze kumtengeneza ajue kua anatakiwa asome mwenyewe. Mimj nampa page tatu asome kisha namuuliza maswal kdg inaanza kunipunguzia kazi
Asante sana, japo kijana wangu wa 5 huwa anamsaidia lkn huwa napenda zaidi niwepo...hilo wazo la kumpa page kadhaa asome kisha kumuuliza maswali ntalifanyia kazi...!
 
Kwa kweli ni kero na udharirishaji kwa sisi wazazi tusiosoma yani mwanangu daily homework ngumu lugha ndio sielewi basi inabidi nimsukume kwa jirani akamsaidie uko, Sasa sijui jirani ananifikiriaje[emoji1]
[emoji38] umenichekesha mkuu, wanajua pengine uko na kazi nyingi
 
Watoto kila siku wanarudi na homework mpya mzazi uwasaidie. Ukimuuliza anakuambia mwalimu hajamuelekeza akaelewa.

Sasa nalipia ada zaidi ya milioni ili watoto wapewe homework niwe mwalimu wao?
Kwa nini hawawafundishi wanafunzi wakaelewa ndipo wawape hizo home work wakazifanye!?

Wazazi wengine hatuna hulka ya kufundisha na wengine ndio tuliishia la sababa.

Tunatafuta hela na kulipa ada ili walimu wawafundishe sio watuletee homework kuja kutupima ujinga wetu..!! Walimu fanyeni kazi yenu ya kufundisha msihamishe goli.

Mbona kwenye ada hatupunguziwi kwamba tumeshiriki kufundisha watoto hivyo tulipwe stahiki zetu!
Kuna mambo madogogo yakukumbushia sio mbaya, ile usiende zaidi kumfanyia kufurahisha kadamnasi ni bora umwache akosee ili mwalimu mjue udhaifu wake na amfunde vizuri.
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Mtoto wangu Homework ya Kiswahili alikosa methali na nahau, mtoto akaulizwa nani kakusaidia akajibu baba... Mwalimu akamwambia babaako na wewe wote akili hamna....

Taarifa ikanifikia, nikaona isiwe tabu, kwakuwa ni class VII nimemhamisha mkoa yupo boarding na homework hainihusu tena.
😂😂😂😂😂
 
Hayo ya kuwategemea 100% ndio yaliyotufikisha hapa hivi sasa, hata mwanao akikuuliza kitu unashindwa kujibu kwa kuwa hukufunzwa kujishughulisha!
Japo mimi sina taaluma ya kufundisha lakini kwa sasa bila shaka mfumo wa utoaji elimu umebadilika!

Umetoka kwenye content based hivi sasa ni competence based, ambapo mwanafunzi ndiye anayepaswa kuwajibika zaidi! Mwalimu kazi yake ni kumwelekeza mtoto cha kufanya, hivyo kumtengenezea namna ya kufikiri na kutafiti zaidi!

Binafsi mwanangu anapofika nyumbani na homework ninavyoona anavyopambana kutafuta maelezo, nafurahia sana! Japo mara chache nipatapo nafasi namsaidia kidogo ila ameshazoea, na mara nyingi inabidi kitu kiwe kigumu sana ndio aulize!

Na hiyo ni baada ya kukosa majibu aliyoyaelewa maana hapendi kabisa kuandika kitu ambacho hakielewi!

Hivyo tusiwalaumu waalimu wa watoto wetu hivi sasa kwamba wanawabebesha mizigo, badala yake tuulaumu mfumo tuliopitia sisi ambao zaidi ulitufanya tuwe tegemezi pasipo kupata ujuzi wa kutosha!
Nakubaliana na wewe 100%.Dogo yupo std 5 nilimuuliza swali la histry f6 kama mzaha tu nione atajibu vipi.

Nilikua suprised aliweza kujibu kwa 90% alafu akamalizia kwa kusema bro mi siwezi sana histry.
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Mtoto wangu Homework ya Kiswahili alikosa methali na nahau, mtoto akaulizwa nani kakusaidia akajibu baba... Mwalimu akamwambia babaako na wewe wote akili hamna....

Taarifa ikanifikia, nikaona isiwe tabu, kwakuwa ni class VII nimemhamisha mkoa yupo boarding na homework hainihusu tena.
Kwa hiyo sasa hivi h/w yake anapeleka bwenini.[emoji1787][emoji1787]
 
Acha kabisa mkuu, binafsi pia inaniboa mnoo. Hapa dogo kaniletea maswali,nmejibu lakini kuna maswali mawili nmechemka.wajuzi wanisaidie please.

1.Farming involving permanent settlement is called...........
2.Farming with no permanent settlement is called.............

Nmemuambia akalale,namtafutia majibu atajaza alfajiri..nmejaribu ku Google lakini wapi
Dah mzee baba hukusoma geography
 
Naunga mkono hoja. Mzazi hutakiwi kumpa au kufanya wewe hiyo home work.Mtafutie nyenzo.Mfano, uwe na vitabu husika vya darasa analosoma mwanao waandishi tofauti.Mfano: Tie, Longhorn,adamson , na kama unajiweza uwe na kompyuta na umfundishe namna ya kuitumia n.k hivyo akikosa jibu anaweza kutafuta mwenyewe kwenye hivyo vitabu.EMitaala ya sasa ni "competency based"
"Competency based" ndo kifaa cha dudu gani hilo? How do one, become competent to something that he/she is not aware of? We need to pick up these bits of fancy!
 
Back
Top Bottom