Hizi shule za English Medium zimetugeuza Wazazi kuwa Walimu?

Wasipo wapa homework, mnazidai kwa nguvu, eti walimu hawafundishi! Kwa hiyo huku uswazi homework ndiyo swali ya mtaani. Wewe, nanirhiu, leo umepewa homework?
 
Aisee hii ni shida mwanangu maswali ya darasa la pili uafikir form3 du watamuua mwanangu, kweli mtoto wa std 2 una muuliza swali la mention four symptoms of tuberculosis kweli, mpaka nikampigia rafiki yanyu doctor mana mimi nilikua najua 2 tu. Sasa sijui nasoma mimi au mwanangu
 
afu ukute ulkua unamwambiaga wewe ndiyo ulkuwa kichwa darasani kwenu 😂 😂
 
Niliwahi kumfanyia dogo homework akaenda akakosa yote
Hebu kila mtu afanye kazi yake wasee mi na stress zangu za pesa na kujipiga na nyundo kwenye vidole badala mwalimu ufanye kaz yako unaniongezea mzigo na mm tena?
 
1. Permanent farming
2. Shifting farming

Kama nimekosea wadau watanisahihisha maana mimi mwenyewe elimu yangu ni ya form 4 ya kufeli tena QT
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hii mishule imefikia hatua watoto wanamwambia mama wewe hujui kila ukitupa majibu tunakosa, wanamwambia mama yao si umesoma hadi form 4 wewe sasa tatizo nini, mi nipo ndani nawasikiliza nacheka tuu[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 

nilitaka kwenda kinyume na mleta mada ila kwa comment yako hii, Nimehairisha mkuu 😂😂😂
 
Mkuu hii ID yako naionaga kule kwenye group letu la forex au siyo hii?
 
Yaani inaumiza Sana.
Lengo lao ni kuwaonesha watoto wetu kuwa sisi hatujui!?
Maana akikosa mmekosa wewe na mwanao.!!
Huu ni unyonyaji.
Yaani unalipia ada kubwa aafu uje kuanza kumfundisha mwanao kupanga sentence??
Kwa nini anaenda shule Kama ni hivyo.
Na Mimi nitapata wapi muda wa kuwaza kutafuta pesa ili nilipe hiyo ada!?
 
Ni hulka ya wanafunzi kusema hakuelewa au Mwalimu hakuelezea vizuri.

Wajibu wako kama mzazi sio kushiriki kumfundisha mtoto bali ni kuhakikisha mtoto anafanya kazi zake. Ugonjwa wa kutofanya kazi ni mkubwa.
 
comment-allez vous monsieur ?
Quell niveau de la langue française êtes vous ?
Moi, je ne parle pas bien,mais je comprends tous,quand qualqun parle.
Alors,comment vous allez?
 
Punguza jazba huwo ni wajibu wako
Wajibu wangu sio kumfundisha vitu ambavyo walimu wake hawajamfundisha.
Wanatakiwa kumfundisha ndipo wampe home work kumpima kama kaelewa.
Sio wampe kazi aje kutafuta majibu ili kesho ndio walimu wamuelekeze.
Sisi tulioishia la 7b tutawaelekeza Nini Hawa watoto.
Mimi naangalia madaftari Kama anafanya kazi na kuandika.
Kama Ana makosa zaidi maana yake haelewi.
Unakagua daftari la mtoto sehemu anayofundishwa ni ndogo kuliko homework unazofanya naye wewe.
Sasa walimu kazi yao Nini!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…