Hizi shule za English Medium zimetugeuza Wazazi kuwa Walimu?

Hizi shule za English Medium zimetugeuza Wazazi kuwa Walimu?

Nani Kakudanganya kayumba hawawezi kufikiri?
English medium ni kiingereza tu anaongeza sio maarifa, Kama mwanao ni kiazi English medium haiwezi kumfanya genius, Na Kama ni genius Hata akisoma kayumba atatamba tu.

Hebu tafakari, kuna mtoto A anasoma primary na secondary Kwa gharama ya mil 20+,na kuna mtoto B anasona kayumba primary, Kata secondary halafu wanakutana chuo kikuu wote wanagraduate degree ile ile.

Wakishagraduate wote wanakuwa jobless, yule aliyesoma akiwa anaenda Kwa school bus anajikalia zake Nyumbani Mara Kwa uncle, hawezi kujiongeza kwasababu amezoea kulishwa kila kitu, aliyesoma kayumba anajiongeza kwasababu ni mpambanaji tangu mwanzo.

Huo ndio uhalisia uliopo mtaani, sasa Nani mwenye akili hapo?
Na Kwa Mzazi mwenye akili kuliko kupeleka mwanao akajifunze kiingereza,kuchora na kuimba Kwa mamilioni huko English medium ni bora Kama unaona ana uwezo mzr ukampekeka kayumba ukamfungulia fixed account, hiyo pesa ya ada ukawa unamuwekea Kwa uaminifu, akifika chuo atakuwa Na mtaji mkubwa sana wa kujiajiri.
Secondary ndio ataenda kayumba nzuri ila primary big no

Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
 
Mimi nilimupa majibu ya urongo na akapewa pato! Nikagundua I am just wasting my money here, waweza jaribu pia
ooh I once saw amepatishwa while the answers zilikua wrong nikashangaa Sana aisee. Umakini ni sifuri kabisa yaani.
 
Watoto kila siku wanarudi na homework mpya mzazi uwasaidie. Ukimuuliza anakuambia mwalimu hajamuelekeza akaelewa.

Sasa nalipia ada zaidi ya milioni ili watoto wapewe homework niwe mwalimu wao?
Kwa nini hawawafundishi wanafunzi wakaelewa ndipo wawape hizo home work wakazifanye!?

Wazazi wengine hatuna hulka ya kufundisha na wengine ndio tuliishia la sababa.

Tunatafuta hela na kulipa ada ili walimu wawafundishe sio watuletee homework kuja kutupima ujinga wetu..!! Walimu fanyeni kazi yenu ya kufundisha msihamishe goli.

Mbona kwenye ada hatupunguziwi kwamba tumeshiriki kufundisha watoto hivyo tulipwe stahiki zetu!
Pole sana aisee, mimi binafsi simfanyii mtoto home work, swali likimshinda cha kwanza namuuliza mmefundishwa? akinijibu wamefundishwa tutaanza kudiscuss pamoja na kurefer kwenye kitabu, akijibu hawajafundishwa namwambia fanya unayoyaweza, akimaliza yanabaki ambayo yamemshinda, nayapiga picha namtumia mwalimu, chini naandika haya maswali yamemshinda mtoto tunaomba majibu.....ooh ayaache tu kesho akija tutayafanya, basi tunafunika daftari tunaendelea na mambo mengine. Lakin namwambia mtoto kesho ukichapwa sababu hujamaliza homework uje uniambie. Kuna mwalimu alishawahi kumchapa mtoto kisa hajamaliza maswali ya home work wakati hajayafundisha, kesi ilifika hadi board ya shule

Home work zenyewe watoto wanapewa nyingi, unakuta mtoto ana home work za masomo matatu au manne, karudi nyumbani saa kumi na mbili hana muda wa kupumzika anakaa mezani hadi saa nne usiku anafanya home work tu bado maswali mengine aliyopewa hajafundishwa. Mzazi nae karudi kachoka na stress za siku nzima ufike tena uanze kufanya home. Kazi ya mzazi ni kuhakikisha mtoto anafanya home work na kukagua kazi zake za shule lakini sio kuwa mwalimu. Walimu mbadilike!
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Aisee elimu ya tz ni upumbavu mtupu,

Sasa hapo hiyo homework atakuwa kafanya mwanafunzi au mzazi?

Lengo la homework ni kumpima mwanafunzi kama kaelewa alichofundishwa au la!
Yani unampa kazi akafanyie nyumbani kulingana na kile alichofundishwa!

Sasa mzazi ukimfanyia akaenda kupata vema atajiona na akili lakini kiuhalisia anakuwa hajaelewa chochote.

Hizi shule kumbe bora mtoto umpeleke kayumba tu.
Niliwahi kumpigia mwalimu mkuu msaidizi nikamwambia mnachokifanya si sahihi, akasema watarekebisha na nikamwambia mtoto hayo yaache. Yaani mahesabu nikiangalia naona picha tu namuuliza anasema kuanzia hapa hatujafundishwa. Mantiki yake sitokuja kuielewa haswa kwa familia mbazo wazazi si wasomi sana.
 
Watoto kila siku wanarudi na homework mpya mzazi uwasaidie. Ukimuuliza anakuambia mwalimu hajamuelekeza akaelewa.

Sasa nalipia ada zaidi ya milioni ili watoto wapewe homework niwe mwalimu wao?
Kwa nini hawawafundishi wanafunzi wakaelewa ndipo wawape hizo home work wakazifanye!?

Wazazi wengine hatuna hulka ya kufundisha na wengine ndio tuliishia la sababa.

Tunatafuta hela na kulipa ada ili walimu wawafundishe sio watuletee homework kuja kutupima ujinga wetu..!! Walimu fanyeni kazi yenu ya kufundisha msihamishe goli.

Mbona kwenye ada hatupunguziwi kwamba tumeshiriki kufundisha watoto hivyo tulipwe stahiki zetu!
Hahahahha
 
Dogo aliwahi kuja na hii, "Parents use mobile phones, ___________, ___________ and ________.

😂😂😂😂😂!

Utopolo mtupu.

Swali ambiguous lisilokuwa na mbele wala nyuma!
Wa kwangu alikuja na swali "Sungura alimwambia nini fisi?" Hakuna hadithi hapo yaani ni swali from nowhere. Nikamuuliza hamjafundishwa? Hapana. Nikamwambia hata mimi sijui, akaanza kulia. Kumwokoa nikajifanya nimekumbuka. "Alimwambia wewe fisi unapenda mifupa". Baada ya wiki moja nikamuuliza kama aliwekewa 'pata' akasema bado ticha hajasahihisha. Sikuuliza tena.
 
Hizi shule wanachukua walimu wabovu tena form four ya kufeli na yote hii ni ubahili anaona kuliko amlipe mwalimu wa digrii sh laki 8 anachukua wa form 4 ya kufeli anamlipa laki 2 na nusu kwa mwezi.

Ni ujinga mtupu
Na bado hawawalipi kwa wakati, kila siku walimu wanaondoka wanatafuta wengine. Mtoto wangu naambiwa mwezi wa sita hawafungi (form two) wazazi tutoe laki 3 za chakula na gharama zingine wakati wa likizo. Tena wanakupigia simu wanakwambia tunazihitaji haraka tukanunue chakula kwani ni bei rahisi sasa, sijatoa na bado natafakari sana
 
Wa kwangu alikuja na swali "Sungura alimwambia nini fisi?" Hakuna hadithi hapo yaani ni swali from nowhere. Nikamuuliza hamjafundishwa? Hapana. Nikamwambia hata mimi sijui, akaanza kulia. Kumwokoa nikajifanya nimekumbuka. "Alimwambia wewe fisi unapenda mifupa". Baada ya wiki moja nikamuuliza kama aliwekewa 'pata' akasema bado ticha hajasahihisha. Sikuuliza tena.
Hilo jibu lilikujia tu [emoji1787]
 
"Competency based" ndo kifaa cha dudu gani hilo? How do one, become competent to something that he/she is not aware of? We need to pick up these bits of fancy!
hiyo competency based inafanya kazi kuanzia vyuo vya kati kwenda juu. Huku chini mwalimu ndiye mwenye wajibu mkubwa wa kuhakikisha mwanafunzi ameelewa.Kwa hiyo siyo sahihi. Mimi kwa sasa mtoto akiwa likizo hagusi madaftari apumzike aangalie katuni, akirudi shule ataendelea na masomo
 
Masomo kama SOCIAL STUDIES ni magumu kweli kweli. Mtoto darasa la tano anapewa swali la homework utadhani ni A level- "Explain in details the benefits and challenges of Regional integration by siting examples in economic, social and other aspects "!! [emoji86][emoji86][emoji86]

Mimi mzazi, I am like...seriously? [emoji56].

Sijui elimu siku hizi ipoje?
Hata mtoto wa form four Kama hayupo vizuri,hawezi jibu hili swali
 
Ukitaka mkeo akuelewe lazima umpeleke mtoto English medium Tena yenye jina Kali Kama
DECEIVINGSHITBASE ENGLISH MEDIUM LEARNING INSTITUTION.
Siku ukitaka mlale mzungu wa nne mrudishe Shule ya Msingi Mwongozo inayomilikiwa na TAMISEMI
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Wa kwangu alikuja na swali "Sungura alimwambia nini fisi?" Hakuna hadithi hapo yaani ni swali from nowhere. Nikamuuliza hamjafundishwa? Hapana. Nikamwambia hata mimi sijui, akaanza kulia. Kumwokoa nikajifanya nimekumbuka. "Alimwambia wewe fisi unapenda mifupa". Baada ya wiki moja nikamuuliza kama aliwekewa 'pata' akasema bado ticha hajasahihisha. Sikuuliza tena.

Hizi shule ni vituko sana. Uzi huu ulikiwa wa maana sana kwao.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Baada ya kusoma huu uzi nimejikuta nikicheka sana siku ya,comment za wazazi/walezi........[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]......unaweza tengeneza vi-clip kabisa kama vya CHARLIE CHAPLIN leo mtajua hamjui.

Mwl. Wa Nidhamu,
P.o.Box *@&#/!£,
Jamii forum.
 
Kwa kweli ni kero na udharirishaji kwa sisi wazazi tusiosoma yani mwanangu daily homework ngumu lugha ndio sielewi basi inabidi nimsukume kwa jirani akamsaidie uko, Sasa sijui jirani ananifikiriaje[emoji1]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Bhasi tu hawezi kukwambia siri anayo yeye na mke wake.
 
Acha kabisa mkuu, binafsi pia inaniboa mnoo. Hapa dogo kaniletea maswali,nmejibu lakini kuna maswali mawili nmechemka.wajuzi wanisaidie please.

1.Farming involving permanent settlement is called...........
2.Farming with no permanent settlement is called.............

Nmemuambia akalale,namtafutia majibu atajaza alfajiri..nmejaribu ku Google lakini wapi
U P D A T E S.
Mwanangu karudi na kilio leo kuwa nmemkosesha,nmejisikia mnyonge sana.
Nawaomba walimu wa English medium mfanye kazi zenu,na pia wazazi tufanye part yetu.

IMG_20210511_181229_8.jpg
 
Katika experience ya jf hakuna uzi umenichekesha kama huu!! Nadhan because it's involve my career, I have 3 years experience in this industry lkn sijawah kukutana na malalamiko ya wazaz khs homework, basically huwa nahakikisha maswali yanatoka within their reach,,, Nita akikisha maswali yote yamefanywa though I don't mind kama amekosa maana hata wrong answer pia ni jibu kikubwa tu mtoto asumbue akili yake kutafuta solution ya jambo at the end of the day itamsaidia Mwanafunz mwenyew,,, kikubwa tu zisiwe too much to extent it become hectic,,, ila ukitaka kujua wazaz wako serious na elimu hebu usitoe homework hamna rangi utaacha kuona kumbe in other side wazaz wako bored namna hii!!!!
 
Mimi napenda sana kufanya nae homework , k vant yangu pembeni uku nampiga pindi.
Mimi ni mtumiaji sio mfanyabiashara so jioni nakua home
 
U P D A T E S.
Mwanangu karudi na kilio leo kuwa nmemkosesha,nmejisikia mnyonge sana.
Nawaomba walimu wa English medium mfanye kazi zenu,na pia wazazi tufanye part yetu.

View attachment 1781100
I'm sure majibu Yapo kwenye notes zake, kama hamna basi yatakuwepo kwenye kitabu, simple technique mnunulie vitabu vyake binafsi kikubwa wasaliana na mwalim umuulize kitabu gani anatumia kuwafundishia,,, then mzoeshe mwanao kusoma vitabu wanavyotumia shule baada ya hapo I'm sure kuletewa maswali ya homework it's going to be hostory for you
 
Back
Top Bottom