Hizi simu nzuri sana kuliko hata Tecno, zinauzwa kwa bei nafuum

Hizi simu nzuri sana kuliko hata Tecno, zinauzwa kwa bei nafuum

JituMirabaMinne

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2020
Posts
3,381
Reaction score
9,744
Najua ndugu zangu wa tecno mtakuja hapa na povu kama lote. Ila acha niwaambie tu kwamba hienda hamkuwaza sawa walati mnanunua hivyo vifaa vyenu vya mawasiliano.

Anyway nimechagua kadhaa ambazo ni bei rahisi. Japo zingine zinaweza kuwa refurbished lakini zinaperform vizuri tu.

Watu wengi wanaotumia tecno husema eti ooooh nmelipa hela kidogo, nmepata simu ambayo ina specs kubwa. My friends acha tu niwaambie kwamba huwa mnapigwa. Yes huwa mnapigwa bei kwa kuuziwa simu ya kawaida tu kwa bei ya juu.

Sasa hebu tuone hizo simu.

1. Iphone 6s Plus
Tena variant ya 128GB jamaa wanazuza kwa $214 tu kwa pc moja.

Screenshot_20200529-173347.jpg


2. Huawei P30 lite
Variant ya 128GB unaipata kwa $197 tu.

Screenshot_20200529-173541.jpg


3. LG V35 thinq
Hiki chuma kina SD845 camera nzuri na unaweza ukaweka Gcam ukitaka. Inapatikana kwa less than $200.

Screenshot_20200529-174529.jpg


4. Realme Q
With only $175 unapata hiki chuma.

Screenshot_20200529-173801.jpg


5. LG V30
Hii Ina SD835 na unaweza kuipata kwa $135 tu tena kwa variant ya 128GB.

Screenshot_20200529-174457.jpg


6. Apple Iphone SE
Kwa mnaoijua hii simu ni level za Iphone 6s. Yaani hata mwenye iphone 6 hapo hatii mguu. Inapatikana kwa $128 tu tena kwa variant ya 64GB

Screenshot_20200529-173927.jpg


7. Apple Iphone 7
Variant ya 128GB unaipata kwa around $200.
Screenshot_20200529-173651.jpg


8. Lenovo K5 pro

Moja kati ya simu ambazo ziko well around basi ni hii lenovo. Around $100 unaweka kuipata kwa variant ya 4GB Ram 64GB of storage.



Screenshot_20200529-174035.jpg


9. LG G6

Hii ina SD821. Variant ya 32GB unaipata kwa around $80. Halafu hii hii simu ni IP68 yaani ni waterproof.

Screenshot_20200529-174134.jpg


Aiseee simu zipo nyingi sana kali kuliko hizo tecno zenu halafu kwa bei chee.

Mfano hizo LG zote tatu nilizopost hapo ni IP68 water and dust resistance. Sasa wanaotumia tecno atakuambia mimi simu ambayo haiingii maji ya nini. wakati akiidondosha simu yake kwenye maji bahati inazima mazima anaenda kununua mpya.

Most of hizo simu hapo zinaperform vizuri kwenye mtandao kuliko tecno zenu za Cat 4 kwenye 4G. Mfano hizo LG zinakimbiza sana mtandao. Mfano hiyo LG V35 thinq ni Cat 16 ambapo max download speed kwenye 4G ni 1024Mbps.

Aiseee nmechoka kuandika ngoja nisubiri mapovu yangu kutoka kwa watumiaji wa tecno.
 
Mkuu, nilipo anza kusoma hizo figure ulizo ziita pesa ndogo za $D's nikajikuta kwaharak nazibadili kichwani, nikaishia paragraph yakwanza na hata picha sikuangalia. Maana tayari akili yangu iliniambia kwamba huu uzi umenipita kimo.
 
Mkuu, nilipo anza kusoma hizo figure ulizo ziita pesa ndogo za $D's nikajikuta kwaharak nazibadili kichwani, nikaishia paragraph yakwanza na hata picha sikuangalia. Maana tayari akili yangu iliniambia kwamba huu uzi umenipita kimo.

$100 ni 230000 roughly. Kwa hiyo wala siyo figure za kutisha. Hakuna simu inavuka 450k hapo.
 
Zinauzwa bei poa kwakuwa nyingi ni 3G na 4G wakati wenzetu wako 5G

Jr[emoji769]

5G bado ina makandokando mengi ndo maana baadhi ya makampuni bado yapo kwenye 4G na mengi yaliyoingia 5G yameingia kwa kulazimishwa na watengeneza processor wao. Mfano qualcom.
 
Kuliko kutuma hela kwa mtu nisiyemjua bora niagize mzigo mimi mwenyewe AliExpress auu KIKUU maana wako makini na hawana utapeli wa aina yeyote.
 
Back
Top Bottom