Hizi tozo kubwa kwenye uingizaji magari zinalenga nini hasa?

Hizi tozo kubwa kwenye uingizaji magari zinalenga nini hasa?

Braza Kede

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2012
Posts
3,840
Reaction score
6,844
Hii hapo chini ni gari Mazda CX5 ya 2014 ambayo unamlipa mjapan milioni 14 unusu.

Kikokotoo cha kodi ya tra kwenye gari hilo ni milioni 10 unusu. Ukijumlisha unapata kama milioni 25 hivi. Hapo bado haujaweka gharama za bandarini.

HAPA UKIANGALIA NI KAMA SISI NA HAO WATENGENEZAJI NI KAMA TUNAGAWANA PASU KWA PASU.

Sasa unajiuliza kwanini kunawekwa tozo kubwa kama hizi kwa vitu ambavyo hata hatuvitengenezi sisi? lengo ni nini hasa?

Huku sio kujikolonisha wenyewe kweli? kulikuwa na sababu au ulazima gani kuwa na tozo kubwa ivi wakati hatutengenezi hizo gari hapa? au tunataka kufidia nini kwa tozo kubwa namna hii? maswali ni mengi wakuu.View attachment 3013556
Screenshot_20240610-100350_Chrome.jpg
 
Wala hamna mwenye roho mbaya na nyinyi. Tatizo ni nchi kuwa na vyanzo vichache vya mapato. Wangekuwa wabunifu na kukawa na vyanzo vingi magari yasingekuwa kimbilio lao. Walipa kodi Tz ni wachache sana ndio maana wanashikilia vitu vile vile miaka nenda rudi wanaongeza kodi tu.
 
Kwa wenzetu kumiliki gari ni kitu cha lazima Kama ilivyo simu ya mkononi..... serikali zetu za Africa kumiliki gari ni anasa
Sema Tanzania tu mkuu Zambia au Malawi kodi ya gari ni ndogo sana nililipia gari ya mteja Zambia kodi sawa na Tsh 6m gari ya 2018 GD 6 hilux double cabin wakati hiyo gari Tanzania kodi yake itaenda zaidi ya 30m...
Fortuner ya 2018 hapa kodi ni Tsh 33m..bei ya kununulia gari ingine..
 
Kama Bajaji ya matairi matatu inafika kwa Tsh 10m jua hakuna Nchi hapo na pia wanashusha thamani ya fedha kirahisi mno fedha haina nguvu ya kununua kitu cha maana.. tunabaki kuuziana magari mabovu na machakavu kwa hela nyingi muda si mrefu tunaanzisha nyuzi hii gari mbovu mara sumbufu kumbe kodi ndio chanzo kikuu cha kukimbilia vitu vibovu vibovu ili kupunguza maumivu kumbe wapi...
 
Back
Top Bottom