Kwa kifupi, serikali kupitia mamlaka yake ya TRA kitengo cha kodi za magari used wanazingua. Inabidi watengeneze formula upya.
Kwasababu, moja: theoretically, gari la zamani linatakiwa liwe na kodi kubwa kuliko gari jipya. Ila angalia CX5 hizi tatu, moja ya 2024, then 2023 na 2022. Ya 2024 ina ushuru mkubwa zaidi ya mil 10 kutoka 2022.
View attachment 3015297View attachment 3015298View attachment 3015300
Na pili, wajue haya magari sasa sio anasa ni chombo cha usafiri, na kinatusaidia katika mishe mbalimbali. Haina haja gari unalipia vitu kibao kuanzia kodi, unakuja kulipia kwenye mafuta kodi, bima nao wanakodi yao serikali, etc. Wangepunguza gharama za kuagiza.
Tatu, kuna magari wangeyawekea exemption mfano yenye cc chini ya 1000 au ya umeme au gesi etc. Ata kama sio 100% free basi kodi iwe ndooogo sana.