Hizi tozo kubwa kwenye uingizaji magari zinalenga nini hasa?

Hizi tozo kubwa kwenye uingizaji magari zinalenga nini hasa?

Naomba nichangie kidogo hapo kwenye kodi na ushuru wa magari, zifuatazo ni kodi na ushuru na tozo mbalimbali zinazotozwa hapa nchini kwa upande wa TRA

1 kodi ya kuagiza gari (Impot Duty) hii inalipwa asilimia 25 ya thamani ya gari (CIF) na nchi zote za Africa mashariki zinatoza kodi hii kwa gari inayoingizwa nchini

2 Ushuru wa bidhaa kulingana na ukubwa wa engine (cc) Hapa viwango vinaanzia 0%, kwa gari ambayo ina CC 0-999cc hapa ushuru wake ni 0, ya thamani ya gari kuna kiwango cha asilimia 5% ya thamani ya gari jumlisha impot duty, kwa gari ambayo ina CC 1000-1999, hapa utalipa ushuru wa 5% na kuna 10% hapa unalipa kwa gari zote zenye CC kuanzia 2000cc

3 Ushuru wa bidhaa kulingana na umri wa gari, hapa viwango vinaanzia asilimia 0, 15 na 30%, gari yenye umri wa miaka 0-8 hapa utalipia 0% na gari ya umri kati ya 8-10 hapa utalipia 15% na gari ambayo ni zaidi ya miaka 10 hapa utalipia 30%

4 kuna Tozo ya kuendeleza reli (RDL) hapa unakatwa 1.5% ya Thamani ya gari (CIF)

5 kuna tozo ya kuchakata taarifa (CPF) hapa unalipia 0.6% ya thamani ya gari

06 kuna Kodi ya VAT, hapa ni asilimia 18% ya gharama ya gari kujumlisha kodi zote ambazo nimezielezea hapo juu

7 kuna tozo ya Whalfage kiswahili sikumbuki ni nn, hii ni asilimia 1.6% ya thamani ya gari japokua kwa budget ya juzi kodi hii itakua inakatwa na TPA wenyewe

Upande wa TPA kuna tozo zifuatazo

1 Kuna Handling Charges ambayo hii ni USD 7.5 ya ukubwa wa gari (CBM) au Ujazo wa gari (KG) itakayokubwa kuliko mwenzake ndio hutumika

2 kuna corridol levy ambayo ni usd 3.5 ya ukubwa au ujazo wa gari

3 Kuna VAT ambayo ni 18%

4 Charges za kutoa mzigo bandarini hapa unamlipa Clearing & Fowarding gharama hua zinategemeana na mzigo wa gari ila wengi ni kuanzia (USD 150) kwa gari moja

5 Kuna tozo ya TBS, Bima, Nk hizo ndio baadhi ya tozo na gharama za viwango nilivyoandika hapo vinaweza kua vimeongezeka au vimepungua lakini vingi vimeongezeka

Sasa kwann Tanzania kodi ya gari ipo juu kuliko baadhi ya nchi za Afrika mashariki, jibu ni kwamba, wenzetu mfano kenya wao wana sheria inayoleta ukomo wa gari kuingizwa nchini kwao na wanataka gari ambayo ina umri wa kati ya miaka 0-8 tu tokea itengenezwe na wanalipa kodi ya kuingiza mzigo na VAT tu, na kwetu TZ sisi hatuna zuio la umri wa gari ni unaingiza gari lolote tu la umri wowote

But nimejitahid sana kuelezea ila kama unahitaji elimu ya kujua gharama za kitu chochote unachoagiza nje hasa magari karibuni ofsini kwetu kwa ajili ya ushauri na kupata msaada wa kuagiziwa gari ulipendalo kwa gharama nafuu sana na zenye ubora

Kwa ushauri na isaidizi nipigie +255 (0) 719 263 074 huu ushauri kwetu ni buree kabisa, Tupo Bamaga mwenge jengo la Dora Tower gorofa ya pili mkabala na kebbys hotel Dar es salaam tanzania (Joex Motors)
 
Hiyo Payee ndio kichefuchefu yaani hii nchi ukija kutoboa labda uwe mwizi
Na waliotoboa wengi ni wezi wanaotengeza mazingira ya kuongeza mzigo kwa Watanzania ili waweze kuzichota na kuishi maisha ya anasa. Tanzania watumishi wa serikali ni matajiri kuliko watu wa private sector. Huwa nasikitika sana kusikia neno mtumishi wa UMMA sijui UMA. UMA upi unaouibia na kuuacha ukiishi umaskini wa kutupwa wewe ukiishi maisha ya anasa.
 
Inasikitisha sana mkuu
 
Hii hapo chini ni gari Mazda CX5 ya 2014 ambayo unamlipa mjapan milioni 14 unusu.

Kikokotoo cha kodi ya tra kwenye gari hilo ni milioni 10 unusu. Ukijumlisha unapata kama milioni 25 hivi. Hapo bado haujaweka gharama za bandarini.

HAPA UKIANGALIA NI KAMA SISI NA HAO WATENGENEZAJI NI KAMA TUNAGAWANA PASU KWA PASU.

Sasa unajiuliza kwanini kunawekwa tozo kubwa kama hizi kwa vitu ambavyo hata hatuvitengenezi sisi? lengo ni nini hasa?

Huku sio kujikolonisha wenyewe kweli? kulikuwa na sababu au ulazima gani kuwa na tozo kubwa ivi wakati hatutengenezi hizo gari hapa? au tunataka kufidia nini kwa tozo kubwa namna hii? maswali ni mengi wakuu.View attachment 3013556View attachment 3013557
Sababu
1. Kuongeza mapato ya serikali
2. Kupunguza msongamano wa magari
3. Kupunguza uchafuzi wa hewa kwa sababu magari mengi yametumika miaka hadi 20
4. Kuchochea utengenezaji wa magari hapa hapa nchni
5. Kupunguza matumizi ya mafuta
6. Kulinda viwanda vya ndani (local manufacturer eg Nyumbu)
 
Duh Aiseee! Isingekuwa kodi kila mtu angeweza kumiliki gari. Maana hivyo CX5 kwa mkononi ingekuwa milion 5 tu.
Duh mbona serikali inavuna mahali haijalima wala kupanda mbegu?!
Kodi kubwa sana, na marais wanaangalia tu, kodi za vinywaji tu zinapunguzwa ila ushuru wa magari kimyaaaaaaaaaaa,
 
Apa ni sawa na unalinunua gari mara mbili, unalinunua china, ukija tanzania unalinunua gari lako ulotoka nalo chiba
 
Bi Tozo Binti Chura anakaba kila Angle na hapa ipo Mama Kimzimkazi Mitano tena.
 
Hii hapo chini ni gari Mazda CX5 ya 2014 ambayo unamlipa mjapan milioni 14 unusu.

Kikokotoo cha kodi ya tra kwenye gari hilo ni milioni 10 unusu. Ukijumlisha unapata kama milioni 25 hivi. Hapo bado haujaweka gharama za bandarini.

HAPA UKIANGALIA NI KAMA SISI NA HAO WATENGENEZAJI NI KAMA TUNAGAWANA PASU KWA PASU.

Sasa unajiuliza kwanini kunawekwa tozo kubwa kama hizi kwa vitu ambavyo hata hatuvitengenezi sisi? lengo ni nini hasa?

Huku sio kujikolonisha wenyewe kweli? kulikuwa na sababu au ulazima gani kuwa na tozo kubwa ivi wakati hatutengenezi hizo gari hapa? au tunataka kufidia nini kwa tozo kubwa namna hii? maswali ni mengi wakuu.View attachment 3013556View attachment 3013557
Sheria za nchi juu ya ushuru hutofautiana kadiri ya mahitaji ya nchi, nafuu kwa watumiaji wa magari na mengineyo.

Tanzania tumepata unafuu kwamba unapoinguza gari kodi ya usajiri (registration) unalilipia mara moja ni kwa maisha yote ya gari ndio maana ushuru wa magari upo juu zaidi.

Nchi ambazo ushuru wa ku8nguza magari upo chini kila mwaka huwa wanafanya registration renewal kila mwaka, kwa maana kwamba kila mwaka pesa zinakutoka
 
Hakuna lolote Ni roho mbaya na ukosefu WA maarifa WA Namna ya kupata Kodi Magu alijaribu kubadili Ile Kodi akaweka kwenye mafuta nadhani alikusanya Hela nyingi zaidi
 
Kwa kifupi, serikali kupitia mamlaka yake ya TRA kitengo cha kodi za magari used wanazingua. Inabidi watengeneze formula upya.

Kwasababu, moja: theoretically, gari la zamani linatakiwa liwe na kodi kubwa kuliko gari jipya. Ila angalia CX5 hizi tatu, moja ya 2024, then 2023 na 2022. Ya 2024 ina ushuru mkubwa zaidi ya mil 10 kutoka 2022.

View attachment 3015297View attachment 3015298View attachment 3015300

Na pili, wajue haya magari sasa sio anasa ni chombo cha usafiri, na kinatusaidia katika mishe mbalimbali. Haina haja gari unalipia vitu kibao kuanzia kodi, unakuja kulipia kwenye mafuta kodi, bima nao wanakodi yao serikali, etc. Wangepunguza gharama za kuagiza.

Tatu, kuna magari wangeyawekea exemption mfano yenye cc chini ya 1000 au ya umeme au gesi etc. Ata kama sio 100% free basi kodi iwe ndooogo sana.
Bongo hatuna watu wanaofikiria vzr
 
Angalia hili jedwali la Kodi ya mafuta hapa ndipo utajua jinsi gani serikali yetu sio wabunifu wa kukusanya kodiView attachment 3015415
Mkuu Wewe elewa tu hatuna watu wabunifu na viongozi wetu Ni bola liende nenda kwenye misitu uombe kibali cha kukata mazao ya misitu yani Ni vituko,Kuna Sheria za hovyo zilitungwa miaka iyo lkn mpaka.sasa bado zipo tu Nchi hii kuishi yataka moyo
 
Kama Bajaji ya matairi matatu inafika kwa Tsh 10m jua hakuna Nchi hapo na pia wanashusha thamani ya fedha kirahisi mno fedha haina nguvu ya kununua kitu cha maana.. tunabaki kuuziana magari mabovu na machakavu kwa hela nyingi muda si mrefu tunaanzisha nyuzi hii gari mbovu mara sumbufu kumbe kodi ndio chanzo kikuu cha kukimbilia vitu vibovu vibovu ili kupunguza maumivu kumbe wapi...
Tena bajaji na bodaboda ndo zipigwe kodi mara tatu kabisa. Zinaharibu mji wa Dar kweli. Sasa hiv city Centre haitamaniki na bodaboda na mabajaji
 
Back
Top Bottom