Lady Ra
JF-Expert Member
- Mar 23, 2014
- 879
- 991
Za Usiku wakuu,
Jana kulikua pale Mlimani City na utoaji wa Tuzo za Sinema Zetu International Film Festival, au SZIFF kwa kifupi. Tuzo hizi ziliandaliwa na kuratibiwa na kituo cha Television cha Azam TV ambacho kinamiliki pia channel ya Sinema Zetu.
Katika tuzo hizi, Msanii Salim Ahmed (Gabo Zigamba) aliibuka mshindi katika categories mbali mbali. Binafsi sina shaka kabisa kua Gabo ni Msanii Mzuri, ila ambacho sijakielewa ni Filamu iliyotumika kumpatia Gabo tuzo hizi.
Gabo alichukua Tuzo hizo kupitia Filamu yake ya SAFARI YA GWALU ambayo aliigiza kama Mwanafunzi mwenye Umri mkubwa. Nachofahamu filamu hii ndio pia iliyompatia Tuzo Gabo mwaka jana. Yaani mpaka tunaingia kwenye Mchakato Gabo ndio alikua "Bingwa Mtetezi" kupitia filamu hiyo hiyo, sasa iweje tena itumike na mwaka huu?
Kama Tuzo ni zinatolewa kila mwaka, inakuaje miaka miwili mfululizo Gabo anatumia filamu moja hiyo hiyo kujipatia ushindi? Hivi hata kwenye Mziki zikitolewa tuzo si zinakua za kipindi cha mwaka mmoja tu nyuma uliopita? Ina maana Gabo atatumia miaka mingapi kuingia na Filamu hiyo hiyo moja tu ilhali kila siku zinazalishwa filamu mpya nyingi tu za kutosha??
Naomba kueleweshwa tafadhali