TAJIRI MKUU WA MATAJIRI
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 11,999
- 24,328
Mvulana Aliyependa Kusoma
Kutokea umri mdogo, Jeff Bezos alikuwa na kiu kisichoisha cha kujisomea. Mama yake Jackie alimkuta Jeff mara nyingi akiwa chumbani, akiwa amezungukwa na milima ya vitabu, akiwa amepotelea kwenye dunia za mbali zilizoko vitabuni. Alimtia moyo kwa kupenda kujisomea, kwa kumpeleka mara kwa mara kwenye maktaba.
Vitabu ndivyo vilivyokuwa malango ya Jeff kupata maarifa na mawazo. Alisoma fasihi andishi zenye maudhui ya tungo za kisayansi kama vile " The Lord of Rings" cha J.R.R Tolkien, kilichoamsha shauku yake ya tekinolojia na maisha yajayo. Wasifu wa viongozi mashuhuri kama vile Thomas Edison zilimuonesha nguvu ya ugunduzi na uvumilivu.
Vitabu Vilivyomuunda Bilionea wa baadae
Jeff alivyokuwa anakua, vitabu viliendelea kushawishi sana namna yake ya kufikiri. Baada ya kuhitimu Chuo Kikuu cha Princeton, alipata kazi inayolipa vizuri kwenye masoko ya fedha na mitaji maarufu kama "Wall Street". Lakini hakuweza kunyamazisha matamanio yake ya kuwa mjasiriamali. Akishangazwa na uwezo wa tasnia mpya ya intaneti, alifanya maamuzi ya kijasiri mwaka 1994 ya kuacha kazi na kuanzisha duka la vitabu la mtandaoni Amazoni.
Kwanini vitabu? Jeff aliona fursa kubwa iliyokuwa wazi kwenye kuweza kuwasilisha vitabu vingi kirahisi kwa kila mtu aliyekuwa ameunganishwa kwenye mtandao wa intaneti. Zaidi ya hapo vitabu vilimaanisha kuwapa watu fursa ya kujipatia maarifa - na alitaka kusambaza maarifa kwa mapana yote duniani.(Sasa hivi Mwafrika au mtu yeyote popote ulimwenguni mwenye intaneti anaweza kusoma vitabu vyote bora kupitia ndoto hii)
Kushirikisha wengine mapenzi ya vitabu
Kadiri Amazoni ilivyokua kutokea kwenye biashara ndogo iliyoanzia kwenye gereji iliyokuwapo nyumbani kwa Jeff hadi kufikia kuwa kampuni kubwa ulimwenguni, jambo moja lilibakia kuwa na Jeff: Shauku yake ya vitabu. Aliwashirikisha wafanyakazi wake mapenzi yake ya kusoma vitabu, hata aliweza kuandaa orodha yake pendwa ya vitabu ambayo ilikuja kuwa maarufu kama "Orodha ya Jeff ya kujisomea" kwenye kampuni.
Vitabu kama vile kitabu kizuri cha biashara cha "Iliyojengwa Kudumu" ("Built to last") cha Jim Collins na kitabu cha hadithi kinachoangazia hulka "Mabaki ya Siku"("The Remains of the Day") cha Kazuo Ishigiro vilikuwa lazima kusomwa na mameneja na viongozi wa Amazon. Kwa kusoma vitabu vingi kwa mapana, Jeff aliamini kuwa timu yake ya uongozi itaunda mtaxamo mpana wa ulimwengu.
Leo hii, Jeff Bezos ni mmoja wa watu matajiri zaidi duniani. Lakini bado hajapoteza shauku yake ya kusoma vitabu aliyokuwa nayo tokea utotoni. Kirahisi na kiuhalisia kabisa, vitabu vilimtengeneza Jeff Bezos - na Jeff Bezos akasaidia kuwezesha vitabu kupaatikana kirahisi zaidi kuliko ilivyowahi kutokea awali.
Asante kwa kusoma 🙏🙏🙏