Hhahaha ama kweli wewe Mzaramo halisi...bila shaka hata Cholesamvula, Mzenga na Mafizi unaweza ukawa na ndugu na jamaa pia.Hahaha,
Minaki pale pua na mdomo na kwetu. Unapokutana na watu, tisa kati ya kumi hawakupi picha halisi.
Mlifika Mwanarumango?
Kote huko.Hhahaha ama kweli wewe Mzaramo halisi...bila shaka hata Cholesamvula, Mzenga na Mafizi unaweza ukawa na ndugu na jamaa pia.
heshima yako mkuu Kiranga unajua kucheza na lugha,tena zote.Kiswahili pamoja na ile iliyokuja na meli. KudosNdugu zanguni wajuvi, wadadisi na wengineo,
Mie ndugu yenu Kiranga cha Ngeda wa viunga vya bandari iso salama, Kiranga wa upande wa Mbwamaji, Kiranga wa Mkuranga,kakae Muamini na mwana wa Fundi Shomvi na Sikudhani binti Muhamedi.
Mara nilivyotoka pande za Msanga Kisiju nikaambiwa ukishangaa maajabu ya Rufiji gari kupita juu ya mto hutafika Utete wala Mpwapwa, zaidi ya hapo maendeleo siku hizi yako huku bandari iso salama kwenye majumba yaliyopandiana, nikachungulia nikaona kweli mnafaudu, hata Mbagala na Charambe tu harufu wanaisikia, na mimi nikaona niombe kugonga hodi hodi mnikaribishe mlionitangulia.Nisambe nimenyimwa maji wakati kisima chatitiri.
Salamu sana kutoka Msanga Kisiju, Kilwa Pande, Kilwa Kivinje, Kilwa Kisiwani, Songo Songo, Somanga, Muhoro mpaka pande za Sala Sala na Mkuranga.Ningewatumia pepeta na mabumunda ya motomoto lakini nimeambiwa humu naweza kutuma picha tu, na mie kamera sina, labda siku nyingine wakija wapima viwanja na midarubini yao ile nitawaomba wanipige picha niiweke muone ninavyofukuzana na ngedere na kima. Sasa niage nikimbilie kuangalia hesabu za minazi maana wakwezi na komba hawakawii kumuadhiri mwenzenu huku. Baada ya hapo mkiniona kimya mjue safari ya Mafia imewadia.
Natanguliza ungo wa shukurani
Kwa leo ni hayo tu,
Wasalaam,
Kiranga cha Ngeda Sangala Kandumbwa
Huyu mkuu ( Sura-ya-Kwanza ) yu wapi siku hizi? Alikuwa na vionjo fulani vya kipekee sana, sivioni tena baada ya ukimwa wake!Kiranga wa ngeda!, Oyee!!
Vigelegele!
Karibu!
Hapa ni JF...na kwanguwoteπ ni JF Ville!
Kula Breki!!!
ππππ
Sina breki za mbavu!
mie mwenyewe nimecheka maana nimeiangalia kumbe niya mwaka 2009 hahahahathread za zamani mnazifufua
kipindi hicho haujiu JFmie mwenyewe nimecheka maana nimeiangalia kumbe niya mwaka 2009 hahahaha
"kakae na Muamini na mwana wa Fundi Shomvi na Sikudhani binti Muhamedi"π ππKumbe Kiranga uliingia kwa mbwembwe namna hiyo
Wana Fasihi hayo wanayaita MAJIGAMBO. Kuna makabila wakati wa harusi bwana harusi inabidi ayatoe hayo. Hongera.Ndugu zanguni wajuvi, wadadisi na wengineo,
Mie ndugu yenu Kiranga cha Ngeda wa viunga vya bandari iso salama, Kiranga wa upande wa Mbwamaji, Kiranga wa Mkuranga,kakae Muamini na mwana wa Fundi Shomvi na Sikudhani binti Muhamedi.
Mara nilivyotoka pande za Msanga Kisiju nikaambiwa ukishangaa maajabu ya Rufiji gari kupita juu ya mto hutafika Utete wala Mpwapwa, zaidi ya hapo maendeleo siku hizi yako huku bandari iso salama kwenye majumba yaliyopandiana, nikachungulia nikaona kweli mnafaudu, hata Mbagala na Charambe tu harufu wanaisikia, na mimi nikaona niombe kugonga hodi hodi mnikaribishe mlionitangulia.Nisambe nimenyimwa maji wakati kisima chatitiri.
Salamu sana kutoka Msanga Kisiju, Kilwa Pande, Kilwa Kivinje, Kilwa Kisiwani, Songo Songo, Somanga, Muhoro mpaka pande za Sala Sala na Mkuranga.Ningewatumia pepeta na mabumunda ya motomoto lakini nimeambiwa humu naweza kutuma picha tu, na mie kamera sina, labda siku nyingine wakija wapima viwanja na midarubini yao ile nitawaomba wanipige picha niiweke muone ninavyofukuzana na ngedere na kima. Sasa niage nikimbilie kuangalia hesabu za minazi maana wakwezi na komba hawakawii kumuadhiri mwenzenu huku. Baada ya hapo mkiniona kimya mjue safari ya Mafia imewadia.
Natanguliza ungo wa shukurani
Kwa leo ni hayo tu,
Wasalaam,
Kiranga cha Ngeda Sangala Kandumbwa
We si ulisema msukuma huyu, msukuma wa kisarawe sijui [emoji134] [emoji134] [emoji134]Kumbe alikua mtata toka zamani ee
Ha ha haa mwanamke hupitwi weweWe si ulisema msukuma huyu, msukuma wa kisarawe sijui [emoji134] [emoji134] [emoji134]
ahahaaaπKumbe Kiranga uliingia kwa mbwembwe namna hiyo
Naanzaje kupitwa na utambulisho matata kama huu!!!Ha ha haa mwanamke hupitwi wewe
Ndugu zanguni wajuvi, wadadisi na wengineo,