Hodi hodi kutoka kwa Kiranga

Hodi hodi kutoka kwa Kiranga

[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] sijawahi kusoma thread ya mgeni anayeomba kukaribishwa nikacheka hivi.
Kiranga ni nomaaa

Ni Nifah mtaalamu wa ufupisho au nimtegemee mwingine..
 
Duh hehehehehehee Kiranga umetisha, ndio kwanza naiona thread yako ya "utambulisho" umetisha...Big up kamanda😀😀
 
Ndugu zanguni wajuvi, wadadisi na wengineo,

Mie ndugu yenu Kiranga cha Ngeda wa viunga vya bandari iso salama, Kiranga wa upande wa Mbwamaji, Kiranga wa Mkuranga,kakae Muamini na mwana wa Fundi Shomvi na Sikudhani binti Muhamedi.

Mara nilivyotoka pande za Msanga Kisiju nikaambiwa ukishangaa maajabu ya Rufiji gari kupita juu ya mto hutafika Utete wala Mpwapwa, zaidi ya hapo maendeleo siku hizi yako huku bandari iso salama kwenye majumba yaliyopandiana, nikachungulia nikaona kweli mnafaudu, hata Mbagala na Charambe tu harufu wanaisikia, na mimi nikaona niombe kugonga hodi hodi mnikaribishe mlionitangulia.Nisambe nimenyimwa maji wakati kisima chatitiri.

Salamu sana kutoka Msanga Kisiju, Kilwa Pande, Kilwa Kivinje, Kilwa Kisiwani, Songo Songo, Somanga, Muhoro mpaka pande za Sala Sala na Mkuranga.Ningewatumia pepeta na mabumunda ya motomoto lakini nimeambiwa humu naweza kutuma picha tu, na mie kamera sina, labda siku nyingine wakija wapima viwanja na midarubini yao ile nitawaomba wanipige picha niiweke muone ninavyofukuzana na ngedere na kima. Sasa niage nikimbilie kuangalia hesabu za minazi maana wakwezi na komba hawakawii kumuadhiri mwenzenu huku. Baada ya hapo mkiniona kimya mjue safari ya Mafia imewadia.

Natanguliza ungo wa shukurani

Kwa leo ni hayo tu,

Wasalaam,

Kiranga cha Ngeda Sangala Kandumbwa
Karibu mzaramu halisi bila chenga, kwa maneno hayo hata usingejitambulisha tungejua tu ni mzaramu kwakwel, karibu sana jamvini ndugu yake mbwiga mbwiguke
 
Al-Watan una mbwembwe...

Huu uzi haunichoshi kuusoma kila mara Mungu akubariki saana hata kama unamkataa
 
Naona Mmefukua Makaburi Yakitambo Sana Kpindi Hicho Jf Siijui
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Dah!!..haya bana, ila nimekumbuka mijadala ya enzi hizo, seemz kama most/ all the best intellectuals wameiacha JF au wamebadili majina kuendana na utoto wa sasa!
Kabisaa Mkuu Nakumbuka Humu Akiandika Kitu Ulikuwa Unakosolewa Then Unafundishwa Uandishi Wa Mada Ila Kwasasa Jf Hovyo Sana
 
Duh! hivi kumbe Chikira Mtabari ndio Nahuja!!...Hii nimeijua leo kwenye hili kaburi ulilofukua!.. NAHUJA an old time mate! [emoji23]
Dah!!..haya bana, ila nimekumbuka mijadala ya enzi hizo, seemz kama most/ all the best intellectuals wameiacha JF au wamebadili majina kuendana na utoto wa sasa!
Teh Teh Teh Huyo Ni Shemeji Yako Dear NAHUJA Hebu Kuja Hapa Mara Moja Lazizi Wangu
Wala sikubadili jina kuendana na utoto. Nimeamua tu. Hata hilo la Chikira nalo nilikuwa nimebadilisha. Ingekuwa ninataka utoto ningefungua ID mpya lakini kama unaona vizuri bado inaonesha nimejiunga 2011. Nitake radhi kuniambia nataka utoto wa JF
 
Back
Top Bottom