Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Karb
NangurukuruSomanga
Ndugu zanguni wajuvi, wadadisi na wengineo,
Mie ndugu yenu Kiranga cha Ngeda wa viunga vya bandari iso salama, Kiranga wa upande wa Mbwamaji, Kiranga wa Mkuranga,kakae Muamini na mwana wa Fundi Shomvi na Sikudhani binti Muhamedi.
Mara nilivyotoka pande za Msanga Kisiju nikaambiwa ukishangaa maajabu ya Rufiji gari kupita juu ya mto hutafika Utete wala Mpwapwa, zaidi ya hapo maendeleo siku hizi yako huku bandari iso salama kwenye majumba yaliyopandiana, nikachungulia nikaona kweli mnafaudu, hata Mbagala na Charambe tu harufu wanaisikia, na mimi nikaona niombe kugonga hodi hodi mnikaribishe mlionitangulia.Nisambe nimenyimwa maji wakati kisima chatitiri.
Salamu sana kutoka Msanga Kisiju, Kilwa Pande, Kilwa Kivinje, Kilwa Kisiwani, Songo Songo, Somanga, Muhoro mpaka pande za Sala Sala na Mkuranga.Ningewatumia pepeta na mabumunda ya motomoto lakini nimeambiwa humu naweza kutuma picha tu, na mie kamera sina, labda siku nyingine wakija wapima viwanja na midarubini yao ile nitawaomba wanipige picha niiweke muone ninavyofukuzana na ngedere na kima. Sasa niage nikimbilie kuangalia hesabu za minazi maana wakwezi na komba hawakawii kumuadhiri mwenzenu huku. Baada ya hapo mkiniona kimya mjue safari ya Mafia imewadia.
Natanguliza ungo wa shukurani
Kwa leo ni hayo tu,
Wasalaam,
Kiranga cha Ngeda Sangala Kandumbwa
Ha haaaa.Ndugu zanguni wajuvi, wadadisi na wengineo,

Sasa mzaramo gani wee huna dini?
Na leo tarehe 30 July acha tuufukue tena KirangaHuu utambulisho kila mwaka unafukuliwa
Kuna jamaa nikiwaambia kiswahili ni kigumu kuliko KIINGEREZA wakawa wanabisha waje hapa wanitafasirie kiranga kasema Nini 😅Ndugu zanguni wajuvi, wadadisi na wengineo,
Mie ndugu yenu Kiranga cha Ngeda wa viunga vya bandari iso salama, Kiranga wa upande wa Mbwamaji, Kiranga wa Mkuranga,kakae Muamini na mwana wa Fundi Shomvi na Sikudhani binti Muhamedi.
Mara nilivyotoka pande za Msanga Kisiju nikaambiwa ukishangaa maajabu ya Rufiji gari kupita juu ya mto hutafika Utete wala Mpwapwa, zaidi ya hapo maendeleo siku hizi yako huku bandari iso salama kwenye majumba yaliyopandiana, nikachungulia nikaona kweli mnafaudu, hata Mbagala na Charambe tu harufu wanaisikia, na mimi nikaona niombe kugonga hodi hodi mnikaribishe mlionitangulia.Nisambe nimenyimwa maji wakati kisima chatitiri.
Salamu sana kutoka Msanga Kisiju, Kilwa Pande, Kilwa Kivinje, Kilwa Kisiwani, Songo Songo, Somanga, Muhoro mpaka pande za Sala Sala na Mkuranga.Ningewatumia pepeta na mabumunda ya motomoto lakini nimeambiwa humu naweza kutuma picha tu, na mie kamera sina, labda siku nyingine wakija wapima viwanja na midarubini yao ile nitawaomba wanipige picha niiweke muone ninavyofukuzana na ngedere na kima. Sasa niage nikimbilie kuangalia hesabu za minazi maana wakwezi na komba hawakawii kumuadhiri mwenzenu huku. Baada ya hapo mkiniona kimya mjue safari ya Mafia imewadia.
Natanguliza ungo wa shukurani
Kwa leo ni hayo tu,
Wasalaam,
Kiranga cha Ngeda Sangala Kandumbwa
Nisambe nimenyimwa maji wakati kisima chatitiri😀Kuna jamaa nikiwaambia kiswahili ni kigumu kuliko KIINGEREZA wakawa wanabisha waje hapa wanitafasirie kiranga kasema Nini 😅
Vumbi aiseee 😅Nisambe nimenyimwa maji wakati kisima chatitiri😀
Kiswahili ni kigumu sana,na kina lack literatureVumbi aiseee 😅
Kumbe kiranga anakijua Sana kiswahili Cha ndani ndani..Kiswahili ni kigumu sana,na kina lack literature
Timu ya mjini huyo! Ni mjuvi wa mambo mengi mnooKumbe kiranga anakijua Sana kiswahili Cha ndani ndani..
Japo anaishi UNITED STATES OF AMERICA