Licking Wounds
JF-Expert Member
- Nov 28, 2014
- 3,979
- 5,146
Niliyakumbuka haya maneno matamu ya kiswahili ya mtaalam Kiranga nikaona bora niutafute😀Uzi wa zamani kinoma 😄
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Niliyakumbuka haya maneno matamu ya kiswahili ya mtaalam Kiranga nikaona bora niutafute😀Uzi wa zamani kinoma 😄
Possible...its almost 15 years nowHuenda baadhi ya watu walio comment kule mwanzo mwanzo hatunao tena 😐
15 yearsNiliyakumbuka haya maneno matamu ya kiswahili ya mtaalam Kiranga nikaona bora niutafute😀
Parefu sana,miaka ya binti kuolewa kabisa kwenye makabila flani hapa bongo15 years
Uzi una umri mkubwa umebakisha miaka mitatu kufikia umri wa utu uzima..Uzi wa zamani kinoma 😄
Kiranga uko wapi.....Shukurani nyingi kwa kuukumbuka uzi.
Yumkini tumesafiri pamoja kwa miaka yote hii.
Natumai tutaweza kusafiri pamoja zaidi.
Kiranga ChaNgeda Sakala Kandumbwa.
Pamoja sana ndugu Kiranga wa upande wa Mbwamaji, Kiranga wa Mkuranga,kakae Muamini na mwana wa Fundi Shomvi na Sikudhani binti Muhamedi 😀✊Shukurani nyingi kwa kuukumbuka uzi.
Yumkini tumesafiri pamoja kwa miaka yote hii.
Natumai tutaweza kusafiri pamoja zaidi.
Kiranga ChaNgeda Sakala Kandumbwa.
Salama kabisa.....Nimerudi viungani kwangu bibie, vipi huko salama?
Mmoja wa watu makini sana ndani ya JFNdugu zanguni wajuvi, wadadisi na wengineo,
Mie ndugu yenu Kiranga cha Ngeda wa viunga vya bandari iso salama, Kiranga wa upande wa Mbwamaji, Kiranga wa Mkuranga,kakae Muamini na mwana wa Fundi Shomvi na Sikudhani binti Muhamedi.
Mara nilivyotoka pande za Msanga Kisiju nikaambiwa ukishangaa maajabu ya Rufiji gari kupita juu ya mto hutafika Utete wala Mpwapwa, zaidi ya hapo maendeleo siku hizi yako huku bandari iso salama kwenye majumba yaliyopandiana, nikachungulia nikaona kweli mnafaudu, hata Mbagala na Charambe tu harufu wanaisikia, na mimi nikaona niombe kugonga hodi hodi mnikaribishe mlionitangulia.Nisambe nimenyimwa maji wakati kisima chatitiri.
Salamu sana kutoka Msanga Kisiju, Kilwa Pande, Kilwa Kivinje, Kilwa Kisiwani, Songo Songo, Somanga, Muhoro mpaka pande za Sala Sala na Mkuranga.Ningewatumia pepeta na mabumunda ya motomoto lakini nimeambiwa humu naweza kutuma picha tu, na mie kamera sina, labda siku nyingine wakija wapima viwanja na midarubini yao ile nitawaomba wanipige picha niiweke muone ninavyofukuzana na ngedere na kima. Sasa niage nikimbilie kuangalia hesabu za minazi maana wakwezi na komba hawakawii kumuadhiri mwenzenu huku. Baada ya hapo mkiniona kimya mjue safari ya Mafia imewadia.
Natanguliza ungo wa shukurani
Kwa leo ni hayo tu,
Wasalaam,
Kiranga cha Ngeda Sangala Kandumbwa
Unataka kumchapa kizinga cha utosi asubuhi yote hii?Kiranga uko wapi.....
Tulia mdudu.....Unataka kumchapa kizinga cha utosi asubuhi yote hii?
😀😀mdudu wa R anataka kukuharibia hisabatiTulia mdudu.....
Kitambo sana.Ndugu zanguni wajuvi, wadadisi na wengineo,