Hodi Mwanza

Hodi Mwanza

Kwa mara ya kwanza Mwenye enzi Mungu akipenda nitawasili Mwanza siku ya kesho.

Gari wakati wa kwenda nitapanda basi la lampuni ya Kisbo halafu nitarudi na basi la kampuni ya happy nation.

Kwa nini kisbo? Kwa sababu sitapenda nilale njiani.

Wale wa ooh kapande mwewe (ndege) hapa sio mahali penu.... wengine passport tulishazichafua sana huko duniani so ndege sio issue sana! me kwa sasa ni basi mwanzo mwisho.

Ushauri mlionishauri kipindi kile kwenye uzi wangu wa wapi nikapumzike nimeuzingatia sana.

Baada ya mapumziko nitarudi na dagaa na samaki so msisite kunipatia oda zenu (Si mnajua tena yatima hadeki)

Haya mniombee safari njema.


Wewe unatoka mkoa upi kuja mwanza au unatoka mbeya, maana kama ni Dar to Mwanza hakuna gari inalala njiani kutokea Dar kuja mwanza labda viberenge(🤣)
 
Nipo stend hapa mbezi... hadi saa 11.59 sioni dalili ya gari kuondoka. Kisbo ya kahama naona ishaamsha.
Ngoja nivumilie labda nyama ziko chini
 
Ungepanda allys angalau zipo vzuri na zinawahi izo kisbo ni gari mbovu sana na ata ufanani nazo
Jaman si kuna uzi huku wanadai kisbo ndo zinafika haraka?? Eti japo bodi mbaya ila mashine nzuri??
Basi usijali nikirudi ally's itahusika. Ila hata hapa inaenda mwendo matata. Tunakaribia moro
 
Back
Top Bottom