Wanajamvi mnisaidie hii,mala kadhaa hukuta mtu anakua na hofu,ni kama kitu ndani yake humsababishia kutokujiamini kwa mambo mengi na hata jambo dogo laweza kumyumbisha na kujikuta akiishi kwa hofu na uoga hata kama jambo ni la kawaida kabisa,swali langu ni je hofu husababishwa ea nini na nini dawa yake ya kuiondoa hofu na uoga?
Hofu hutokana na kukosekana kwa Upendo.
Wanajamvi mnisaidie hii,mala kadhaa hukuta mtu anakua na hofu,ni kama kitu ndani yake humsababishia kutokujiamini kwa mambo mengi na hata jambo dogo laweza kumyumbisha na kujikuta akiishi kwa hofu na uoga hata kama jambo ni la kawaida kabisa,swali langu ni je hofu husababishwa ea nini na nini dawa yake ya kuiondoa hofu na uoga?
kuna mtu alinieleza kwa upande wake anaweza akapigiwa simu na rafiki wake aidha wa kawaida au mpenzi wajumuike pamoja. roho ikikataa ule mualiko hali ya mwili inabadilika sana anakuwa dhaifu. vilevile anaweza akawa amepanga kazi za kufanya siku husika, bosi wake akatokea akampa kazi mpya, roho ikikataa mwili unabadilika anakuwa dhaifu, hiyo siku inawezekana asifanye kazi yeyote kabisa. changamoto kubwa hali ya roho kukubali au kukataa ni automatic, yaani hawezi kuizuia. kwa hakika inamuathiri kiuchumi na kijamii.naomba ufafanuzi wa hili au tiba yake.
Angalieni vyema swali langu la mwisho,nini dawa ya kuondoa hofu,kwa mfano,unaweza mkuta mtu hata sio masikini wa fedha wala elimu lakini ana mambo yanamyumbisha,akitokewa na jaribu fulani katika maisha yake mtu huyo huishia kuogopa na kua na hofu mpaka anatafuta washauli,mwingine waweza kuta hata mke wake au mume wake wa ndani au mpenzi wake anaweza akamyumbisha kwa kiasi kikubwa ilihali watu hawa hulala kitanda kimoja,Je ni uumbaji wa MUNGU juu ya mtu huyu?Je ni kukosa kujiamini?au ni sili ipi iko ndani ya watu hawa waoga na nini dawa ya kuwasaidia?
Naomba kwanza unieleze maana ya neno ''jaribu/majaribu''maana naona kama linatumika kuficha failure binafsi za kibinadamu, mfano mwanafunzi asiyezingatia masomo yake sawa sawa, huyo naye akifeli mitihani tuite ni jaribu/majaribu? Nani anayekuyumbisha? Na kwa nini akuyumbishe? Kwa nini uyumbe? Mambo mengine ni ya kiimani tu, na ni bora tuyaache au tuyatumie hukohuko kwenye imani tu!! Kama ni hofu juu ya kitu kisichokuwepo, au usichokijua (fear of unknown) hapo tunaweza kuulizana chanzo na sababu zake, ila kama ni hofu juu ya simba unayemwona dhahiri akikuvizia hapo hakuna cha ku discuss!! Tutakwambia tu kuwa hofu hiyo imesababishwa na madhara yanayoweza kusababishwa na simba ambayo wewe mwenyewe unayajua, otherwise hofu pia ina faida zake, tena nyiingi tu, ndiyo maana imechangia hadi wewe leo unaishi kwenye nyumba yenye kuta imara! Yenye fence na ulinzi imara, una bima ya afya na mali pia, una akaunti benki na makoti ya baridi japo ni msimu wa jua kali nk nk nk.Angalieni vyema swali langu la mwisho,nini dawa ya kuondoa hofu,kwa mfano,unaweza mkuta mtu hata sio masikini wa fedha wala elimu lakini ana mambo yanamyumbisha,akitokewa na jaribu fulani katika maisha yake mtu huyo huishia kuogopa na kua na hofu mpaka anatafuta washauli,mwingine waweza kuta hata mke wake au mume wake wa ndani au mpenzi wake anaweza akamyumbisha kwa kiasi kikubwa ilihali watu hawa hulala kitanda kimoja,Je ni uumbaji wa MUNGU juu ya mtu huyu?Je ni kukosa kujiamini?au ni sili ipi iko ndani ya watu hawa waoga na nini dawa ya kuwasaidia?
acha kukariri, kwani ukikutana na simba au mnyama yeyote mkali ukapatwa na hofu hapo utasemaje simba huyo hana upendo? Au ikipiga radi ukapatwa na hofu utasemaje mungu aliyeumba hiyo radi hana upendo?
Tusaidie ndugu,unamaanisha nin?
Nilimaanisha kuwa binadamu ana uwezo kabisa wa kuchukua usukani na kuwa na control ya akili yake. Kitu kikifanywa mara nyingi hujenga mazoea na mazoea ugeuka tabia. Una uwezo unaoitwa will power, ukiamua unaweza kuibadili hali yoyote.
Nilimaanisha kuwa binadamu ana uwezo kabisa wa kuchukua usukani na kuwa na control ya akili yake. Kitu kikifanywa mara nyingi hujenga mazoea na mazoea ugeuka tabia. Una uwezo unaoitwa will power, ukiamua unaweza kuibadili hali yoyote.