Hofu husababishwa na nini?

Hofu husababishwa na nini?

Binafsi natambua hivi;
Hofu ni hali impatayo mtu pale anapokosa ujasiri/ni matokeo ya kukosekana kwa ujasiri...kwa tukio hatarishi ambalo bado halijatokea, linalotokea au linatarajiwa kutokea.

Hivyo mtu anapokosa ujasiri iwe ni 'inner power' au 'physical ability' huingiwa na hofu na kuona kuwa atamezwa na hatari iliyopo mbele yake...

Unaweza kuikimbia hofu kwa kufanya au kufuata yafuatayo;
1. Kujiamini (kuwa na mtazamo chanya)...

2. Kujiandaa kimwili na kiroho...(kuwa na ujuzi wa mambo yanayokukabili na yatayokukabili)

3. Kuomba msaada toka katika NGUVU zilizokuzidi nguvu...

Wanajamvi mnisaidie hii,mala kadhaa hukuta mtu anakua na hofu,ni kama kitu ndani yake humsababishia kutokujiamini kwa mambo mengi na hata jambo dogo laweza kumyumbisha na kujikuta akiishi kwa hofu na uoga hata kama jambo ni la kawaida kabisa,swali langu ni je hofu husababishwa ea nini na nini dawa yake ya kuiondoa hofu na uoga?
 
Unaweza kuikimbia hofu kwa kuanza kujiamini (kuwa na mtazamo chanya)...

Anawezaje kushinda jambo hilo na kua hulu kifikla kisha kutatua tatizo?
 
Wanajamvi mnisaidie hii,mala kadhaa hukuta mtu anakua na hofu,ni kama kitu ndani yake humsababishia kutokujiamini kwa mambo mengi na hata jambo dogo laweza kumyumbisha na kujikuta akiishi kwa hofu na uoga hata kama jambo ni la kawaida kabisa,swali langu ni je hofu husababishwa ea nini na nini dawa yake ya kuiondoa hofu na uoga?

inasababishwa na life experience, kwako au kwa kuona kwa watu wengine.
 
Atiii???

Mbona umeni-quote tena miye miye Watu8?

Nimezinguka... Hahaaa
Kujibu swali lako kwanza yapasa kujua Binadamu ni kiumbe kilichoumbwa na kupewa uwezo mkubwa mno ambao ni free will. Yaani binadamu ana uwezo hata wa kumkana aliyemuumba na akatumia will yake kujidai anavyotaka humu Duniani.
Lakini mimi binafsi naamini katika Higher power na naona ukiamua ku align your will with the higher power unakuwa even more powerful.
Kwahiyo nikiangalia jibu lako la post #21 naona umeiweka vyema all the same.....lol
 
Hahah...pole sana kwa kuzinguka lol

Kwa kujibu hivi sasa nadhani nimekuelewa...

Nimezinguka... Hahaaa
Kujibu swali lako kwanza yapasa kujua Binadamu ni kiumbe kilichoumbwa na kupewa uwezo mkubwa mno ambao ni free will. Yaani binadamu ana uwezo hata wa kumkana aliyemuumba na akatumia will yake kujidai anavyotaka humu Duniani.
Lakini mimi binafsi naamini katika Higher power na naona ukiamua ku align your will with the higher power unakuwa even more powerful.
Kwahiyo nikiangalia jibu lako la post #21 naona umeiweka vyema all the same.....lol
 
Fear is not real. It is a product of thoughts you create by forecasting what will happen. Do not
misunderstand me. Danger is very
real. But fear is a choice.
 
Ni mawimbi ya fikra tu yanapojihami... Wakati mwingine ni defence mechanism ya ubongo.
^^
 
Naomba kwanza unieleze maana ya neno ''jaribu/majaribu''maana naona kama linatumika kuficha failure binafsi za kibinadamu, mfano mwanafunzi asiyezingatia masomo yake sawa sawa, huyo naye akifeli mitihani tuite ni jaribu/majaribu? Nani anayekuyumbisha? Na kwa nini akuyumbishe? Kwa nini uyumbe? Mambo mengine ni ya kiimani tu, na ni bora tuyaache au tuyatumie hukohuko kwenye imani tu!! Kama ni hofu juu ya kitu kisichokuwepo, au usichokijua (fear of unknown) hapo tunaweza kuulizana chanzo na sababu zake, ila kama ni hofu juu ya simba unayemwona dhahiri akikuvizia hapo hakuna cha ku discuss!! Tutakwambia tu kuwa hofu hiyo imesababishwa na madhara yanayoweza kusababishwa na simba ambayo wewe mwenyewe unayajua, otherwise hofu pia ina faida zake, tena nyiingi tu, ndiyo maana imechangia hadi wewe leo unaishi kwenye nyumba yenye kuta imara! Yenye fence na ulinzi imara, una bima ya afya na mali pia, una akaunti benki na makoti ya baridi japo ni msimu wa jua kali nk nk nk.

nimecheka sana!well said ndugu
 
Wasiwasi hausaidii. Imeandikwa katika Zaburi 37:8 "Ukomeshe hasira, uashe ghadhabu, usikasirike, mwisho wake ni kutenda mabaya."

Hakuna haja ya kuwa na hofu.. Mungu yuko nasi. Imeandikwa katika Mathayo 6:31-33 "Msisumbukie, basi mkisema, tuleni nini? au tunyweni nini, au tuvae nini? kwa maana hayo yote mataifa huyatafuta kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. Basi utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake na hayo yote mtazidishiwa."

Hatuwezi kuondoa hofu katika maisha yetu hadi tuwe na jambo jingine jema na maombi. Imeandikwa Wafilipi 4:6- 7 " Msisumbukie kwa neno lo lote, bali katika kila neno kwa kusali na kuomba pamoja na kushukuru haja zenu na zijulikane na Mungu na amani ya Mungu ipitayo akili zote itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu."

Kuwa na hofu ni kupoteza muda. Imeandikwa katika Luka 12:25-26 "Na yupi kwenu ambaye ajisumbua ambaye aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja basi ikiwa hamwezi hata neno lililo dogo kwa nini kujisumbua na hayo mengine?."

Mpe Mungu hofu zako. Imeandikwa katika 1Petro 5:7 "huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote kwa maana yeye hujishuguliza sana kwa mambo yenu."

Mkuu mbona mstari uliou-quote hauzungumzii Hofu bali hasira..., au nimeshindwa kuelewa!
 
Binafsi natambua hivi;
Hofu ni hali impatayo mtu pale anapokosa ujasiri/ni matokeo ya kukosekana kwa ujasiri...kwa tukio hatarishi ambalo bado halijatokea, linalotokea au linatarajiwa kutokea.
Hivyo mtu anapokosa ujasiri iwe ni 'inner power' au 'physical ability' huingiwa na hofu na kuona kuwa atamezwa na hatari iliyopo mbele yake...
Unaweza kuikimbia hofu kwa kufanya au kufuata yafuatayo;
1. Kujiamini (kuwa na mtazamo chanya)...

2. Kujiandaa kimwili na kiroho...(kuwa na ujuzi wa mambo yanayokukabili na yatayokukabili)

3. Kuomba msaada toka katika NGUVU zilizokuzidi nguvu...

Sawa kabisa mpwa Watu8. . . . Kuchagiza kidogo tu ni kuwa namba moja msingi wake uko kwenye namba mbili "Kujiandaa" hapa ndipo haswa kwenye ushindi dhidi ya hofu. . .Kujiandaa kifikra, kiuchumi, kisaikolojia, na yote yahusianayo na jambo ambalo unaenda kulikabili na ili kuishinda hofu na kuishi kwa kujiamini ni bora kila mtu ajiweke katika hali ya tahadhari kwa mambo kama ugonjwa, vifo, hali ngumu za kimaisha kama uchumi, ujuzi wa kazi unayoifanya na mambo kama hayo ujitengenezee "comfort zone" ambayo lolote likitokea basi una operate humo kwenye zone yako.. . . . . . .Jiandae kana kwamba uko peke yako ili ikitokea hali itayosababisha ukose msaada basi ndani ya zone yako uweze kukabili changamoto hata pasipo msaada!!! Ingawa pia unatakiwa uwe na social capital sambamba na comfort zone yako binafsi. . .. .

Mwisho ni kumuomba sana Mungu akuepushe na yale yasiyo na heri kwako, akutie nguvu juu ya changamoto za kilimwengu na kiimani. . . .
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom