Amani iwe kwenu . Niende moja kwa moja kwenye mada, kwa muda mrefu nilikuwa nahisi hali yangu ya mfumo wa mkojo haiko sawa. Lakini kubwa ni kushindwa kujiziwia nikibanwa na haja ndogo. Mara nyingi nilikuwa nikienda hospitali niliambiwa nina mkojo mchafu( u.t.i) napewa dawa natumia napata nafuu na ile hali inapungua kwa kiasi maisha yanaendelea.
Sasa tatizo limeanza kuwa kubwa kuanzia mwezi wa nane mwanzoni. Nikiwa na mkojo kiasi kidogo tu nahisi unabana Sana na Mara nyingi najikojolea. Nikaanza kupata maumivu makali Sana ya korodani moja ya upande wa kulia na mishipa inayoshikilia, msuli wa uume chini ya korodani unakaza na kujivutavuta, uume kukakamaa, nikikojoa nahisi Kama mkojo umebaki njiani, nikawa nakohoa Sana pia. Nilipoenda hospitali niliambiwa nina mkojo mchafu Kama kawaida nikapewa Cipro. Baada ya kumaliza hali ya kuto ku control mkojo ikawa inaendelea na dalili zingine nilizokuwa nazo pia.
Sasa tarehe 15 ya mwezi huu nikaona ngoja niende dispensari ambayo mmiliki wake ni daktari wa hospitali ya wilaya. Nilivyompa maelezo akaniandikia nika check damu na mkojo. Majibu nikaambiwa mfumo wangu wa mkojo kuanzia kwenye figo hadi kwenye kibovu umeshambuliwa vibaya na bakteria.
Na hali hii kwa namna moja huwa inasababisha tezi dume. Akaniandikia dawa ambazo nu felcine, tetracycline na secnidazole. Sasa hofu yangu ni kwamba hii hali niliivumilia kwa muda mrefu Sana, je nimesalimika kweli na tezi dume??
Mnanishauri nini wana jamiiforums.
Samahani kwa uandishi wahovyo