Hofu imenitanda nahisi nina tezi dume

Hofu imenitanda nahisi nina tezi dume

Chitiva

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2020
Posts
951
Reaction score
1,171
Amani iwe kwenu . Niende moja kwa moja kwenye mada, kwa muda mrefu nilikuwa nahisi hali yangu ya mfumo wa mkojo haiko sawa. Lakini kubwa ni kushindwa kujiziwia nikibanwa na haja ndogo. Mara nyingi nilikuwa nikienda hospitali niliambiwa nina mkojo mchafu( u.t.i) napewa dawa natumia napata nafuu na ile hali inapungua kwa kiasi maisha yanaendelea.

Sasa tatizo limeanza kuwa kubwa kuanzia mwezi wa nane mwanzoni. Nikiwa na mkojo kiasi kidogo tu nahisi unabana Sana na Mara nyingi najikojolea. Nikaanza kupata maumivu makali Sana ya korodani moja ya upande wa kulia na mishipa inayoshikilia, msuli wa uume chini ya korodani unakaza na kujivutavuta, uume kukakamaa, nikikojoa nahisi Kama mkojo umebaki njiani, nikawa nakohoa Sana pia. Nilipoenda hospitali niliambiwa nina mkojo mchafu Kama kawaida nikapewa Cipro. Baada ya kumaliza hali ya kuto ku control mkojo ikawa inaendelea na dalili zingine nilizokuwa nazo pia.

Sasa tarehe 15 ya mwezi huu nikaona ngoja niende dispensari ambayo mmiliki wake ni daktari wa hospitali ya wilaya. Nilivyompa maelezo akaniandikia nika check damu na mkojo. Majibu nikaambiwa mfumo wangu wa mkojo kuanzia kwenye figo hadi kwenye kibovu umeshambuliwa vibaya na bakteria.

Na hali hii kwa namna moja huwa inasababisha tezi dume. Akaniandikia dawa ambazo nu felcine, tetracycline na secnidazole. Sasa hofu yangu ni kwamba hii hali niliivumilia kwa muda mrefu Sana, je nimesalimika kweli na tezi dume??

Mnanishauri nini wana jamiiforums.

Samahani kwa uandishi wahovyo
 
Mkuu wala usijitie hofu nenda katibiwe procedure zake siku moja tu ila usiache tatizo likawa kubwa kafanye linalotakiwa kufanywa muhimu pata Dr mzuri huu sio ugonjwa wako tu wanaume ndio tatizo kubwa ila wahi utapona tu usichelewe.
 
Shukrani
 
pole sana hilo tatizo kwa sasa linawasumbua wanaume wengi na kadiri unavyotumia madawa ndivyo unajiweka kwenye hatari ya kuzidi kuharibu mfumo wa mkojo na uzazi kwa ujumla
hali hii usipopata tiba stahiki itakupelekea kupata vijiwe katika FIGO ba nwishowe FIGO kufeli

kabla hatujaenda kwa UNDANI
ulifanya URINE CULTURE
Ulifanya UTRA SOUND kwenye mfumo wa mkojo
Ulifanya FULL BLOOD CHECK

hvyo vipimo vitatu ulifanya na majibu yalikuaje
 
pole sana hilo tatizo kwa sasa linawasumbua wanaume wengi na kadiri unavyotumia madawa ndivyo unajiweka kwenye hatari ya kuzidi kuharibu mfumo wa mkojo na uzazi kwa ujumla
hali hii usipopata tiba stahiki itakupelekea kupata vijiwe katika FIGO ba nwishowe FIGO kufeli
Hivi kuna uhusiano kati ya tezi dume na kidney stones...?
 
Hivi kuna uhusiano kati ya tezi dume na kidney stones...?
bila shaka ukiwa naTEZI dume ya muda mrefu hujaopata Tiba huwezekano wa kupata KIDNEY STONE huwa mkubwa kutokana na KIBOFU chako kinakuwa hakimalizi mkojo wote yaan inakuwa tabu sana

lkn alichokuwa anaumwa hapo jamaa kwa maelezo yake Sio TEZI DUME.

bali ni ATHARI zilizotokana na SHAMBULIO la BACTERIA katika mfumo wake wa mkojo na utumiaji mbaya wa dawa za ANTIBIOTIC
 
Amani iwe kwenu . Niende moja kwa moja kwenye mada, kwa muda mrefu nilikuwa nahisi hali yangu ya mfumo wa mkojo haiko sawa...
Pole sana
Binafsi naona unahitaji kwenda kwenye hospitali ya daraja la juu na ni umakini tu unahitajika. Mwone daktari na kwa maelezo uliyotoa, ni vyema kupata kipimo cha:

1: Mkojo (Urine routine), kama itaonekana kuna maambukizi ndo ufanye culture/uoteshe mkojo.

2: Ufanye KUB ultrasound. Itakayohusisha kuangalia mfumo mzima wa mkojo na tezi lenyewe. Uwepo wa vijiwe kwenye njia ya mkojo. Uwepo wa maumbile yasiyo ya kawaida.

Kuna mambo ambayo hayajatajwa wazi mfano: umri na eneo linalosumbua zaidi, ambayo itasaidia kufikiria tatizo halisi. Pia maambukizi yoyote yaliyowahi kutokea na ukawa unatoa majimaji au usaha?

Maambukizi huweza kuleta kuvimba kwa kiasi kidogo na kwa muda mfupi kwa tezi dume lakini siyo ugonjwa husika wa tezi dume (benign prostate hypertrophy/BPH).

Hivyo, tulia ufanye ufatiliaji kwa makini.
 
A
Pole sana
Binafsi naona unahitaji kwenda kwenye hospitali ya daraja la juu na ni umakini tu unahitajika. Mwone daktari na kwa maelezo uliyotoa, ni vyema kupata kipimo cha...
Asante Sana mkuu, nitafanyia kazi ushauri wako?
 
Amani iwe kwenu . Niende moja kwa moja kwenye mada, kwa muda mrefu nilikuwa nahisi hali yangu ya mfumo wa mkojo haiko sawa...
Mkuu usijali. Kapime haja ndogo tena Kisha leta majibu ikibidi pm mkuu nakuelekeza dawa ya hiyo shida Kuna jamaa alikuwa na tatizo Kama hilo kadumu nalo takribani miaka 7 lakini baada ya maelekezo yupo njema kabisaaaaaaaa.
 
Sasa mkuu we unataka uishi miaka mingapi? Wacha woga kunywa dawa utapona
 
Kwa namna alivyoelezea juu ya tatizo lake inabidi afanye kazi ya ziada na kama ulivyosema mtu anaweza kumaliza muda mrefu sana anahangaika na mateso hayo sababu ya kutopata tiba sahihi...
Kuna ukweli katika hayo mkuu
 
Tezi dume ukiliwahi wala sio shida unapona tu ila kwa dawa za kienyeji tena rahosi sana
 
Mkuu usijali. Kapime haja ndogo tena Kisha leta majibu ikibidi pm mkuu nakuelekeza dawa ya hiyo shida Kuna jamaa alikuwa na tatizo Kama hilo kadumu nalo takribani miaka 7 lakini baada ya maelekezo yupo njema kabisaaaaaaaa.
Shukrani mkuu
 
Back
Top Bottom