Hofu imetanda, Marekani imedeploy ndege wanajeshi Miami Beach

Usikute hajui kuwa Russia na US ni ajirani
 
nimesoma mahali wanasema Russia ana nyambizi pacific na zingine antlatic, that means yuko pande zote za US.........

majenerali wa US wanasema ndani ya miaka 2-5 ijayo Russia atakua na uwezo wa kudeploy nyambizi zaidi ya 5 kila upande (i.e pacific & antlatic) na hii wanasema itasumbua sana kiulinzi
 

Wenzetu wanaishi, kila siku mbongo zao zinawaza new high advance technology, sisi tumebaki majungu
 
Ndege zinazunguka kwa hofu😂😂.
Ni vile tu Russia hawajieni, ilitakiwa iwe inawalipieni japo bundle? Maana hata Warusi wenyewe hauwezi kuwakuta wakitoa michango kama hii
 
Hizo ndege hazina uhusiano wowote na unachojaribu kukihisisha nacho.
Alichofanya US ni kuisogeza hapo Guantanamo bay USS Helena ambayo ni ni nuclear powered fast attack submarine. Ipo hapo Guantanamo, just 900+ Km from Havana na ni straight line.
Hili swala la Russia kupeleka hizo nyambizi zake naona mmelikomalia sana kwa kuwa ni mara yenu ya kwanza kulisikia.
Kajifunzeni kuhusu ‘The flotilla’ , makubaliano ya kirafiki ya Majeshi ya Majini ya nchi mbili ambapo kila baada ya muda fulani hutembeleana na kufanya mazoezi ya pamoja. Hii siyo mara ya kwanza, imeshakuwa hivyo mara kadhaa huko nyuma.
 
Kwa wale waliokua wanaiona Urusi kama Haina akili utu na ustaarabu kuizuia NATO isiisogelee karibu Sasa nadhani watakua wamepata majibu sahihi kabisa kua NATO kuja karibu na Urusi ni hatari na shari.
Sasa hebu fikiria Urusi Haina ugomvi na USA je ni Nini kikepelekea USA kupeleka silaha karibu na Cuba mara baada TU ya Urusi kupeleka melivita nchini Cuba kwa ajili ya kufanya mazoezi?
Je mbona USA hufanya mazoezi na nchi nyingine sehemu nyingine hapa duniani lakini hatujaona Urusi akipelela majeshi namna hiyo?
Kwa Hali hiyo ndio wale waliokua wanailaumu Urusi kwa kuizuia Ukraine isijiunge na NATO Kwa sababu Ukraine kua mwanachama wa NATO kunapelekea USA kuikaribia Urusi kama vile Urusi ilivyoikaribia USA kupitia kwa Cuba.
Kama USA anaona si sahihi kwa Cuba kama taifa huru kukaribisha marafiki zake ambao ni maadui wa USA basi vivyo hivyo kwa Urusi ndivyo anavyoona sio sahihi kwa Ukraine kuwakaribisha maadui zake NATO
Kwa hofu aliyoipata USA basi Urusi anayo haki ya kuipiga Ukraine.
Wenye akili watakua wamenielewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…