Hofu inayotawala Mataifa ya Ulaya Dhidi ya Waafrika na Bara lao

Hofu inayotawala Mataifa ya Ulaya Dhidi ya Waafrika na Bara lao

80% ya watu wote Duniani ni whites(wazungu+asians+Arabs) huku 20% pekee black.
Sasa hapo tutakuja lini kuwa overtake watu weusi Duniani.
 
Kwani mtu kukuletea uzazi wa mpango anakuwa hana nia njema na wewe? Sijajua we ni jinsia gani ila kama ushawahi kuona madhira yanayowakumba wazazi waliacha kutumia uzazi wa mpango basi utakubali kuwa kila kwenye ubaya kuna chembe chembe za wema.
Nimekuelewa alafu kama sijakuelewa! Kwamba kuna madhara mtu anapata akiacha kutumia uzazi wa mpango?
 
Zamani walichukuliwa utumwani kwa lazima siku hizi wanagombea wenyewe tena kwa njia za panya au halali viza ubalozini.
Leo biashara ya utumwa ikirudi afrika sidhani kama kuna kijana atakubali kubakia afrika.
Yote hii chanzo ni watawala wa kiafrica wameshindwa kuwakomboa waafrika.Ule msemo wa mwafrika hana uwezo wa kuongoza Jamii ikastawi unapata maksi.
Wakoloni walichukua raslimali kiduchu sana hata robo tu haifiki kulingana na raslimali tele zilizojaa na hazitumiki.
Wakoloni waliweza waletea waafrika maendeleo makubwa Sana ikiwemo kumaliza kabisa tatizo la ajira,masoko ya mazao yao nk.
Watawala wa kiafrica wameshindwa zitumia raslimali tele zilizojaa kuleta ustawi wa maendeleo wa kiafrica.
Matatizo ya mwafrika chanzo ni mwafrika mwenyewe chanzo cha vita congo ni ubinafsi wa mobutu.Congo itakuwa na amani siku kagame akifa, kagame na mseveni ndio wanufaika wakuu wa vurugu za Congo kwa kumiliki makundi ya waasi yanayoiba raslimali za Congo.
Hapa Mzungu anahusika vipi na ukosefu wa amani afrika, ubinafsi ndio chanzo cha vita na vurugu zote afrika.Ubinafsi ni tabia ya watawala wa kiafrica ni kama wapangaji yaani awatazami future ya afrika bali ustawi wa familia zao.
 
We unavyoona wana encourage population? Fanya tafiti wanawake wangapi wameathirika na vidhibiti mimba.
sijasema wana encourage, nimekuuliza kwa nini wasi encourage ? Wana discourage, bali wewe hujui kwa nini wanafanya hivyo. wazungu wana uwezo wa kuchukua chochote toka kwetu, directly or indirectly na huna uwezo wa kuwazuia. udhibiti wa nchi za dunia ya tatu ni kwa wananchi wao wasiweze kuwanyoshea kidole au kuandamana tu, nje ya hapo hakuna kitu. wanazuia tuzizaane kama panya kwa sababu uwezo wa uchumi wetu hata kulea mto mmoja ni shida. usishabikia wanasiasa, hospitali za Rufaa za mikoa zimegeuka vituo vya kutoa ushauri. hakuna hata paracetamol. vyuo vikuu watoto wa kike usiku wako kwenye mataa, wa kiume ni machinga, kupata hela ya kujikimu.
 
Ni dhana tulijengewa na Wazungu kuwa hatuwezi kitu. Ila amini hata hapa Tanzania kuna Familia zakawaida kabisa tu zinamiasha mazuri sana kupita hata familia za kizungu. Pia kuna waafrika wana akili kuliko unavyodhani. Malkia wa uingereza alifanyiwa operation na Kamuzu Banda mwafrika hapo jirani yetu. Ni ushamba sana na kujiaibisha kujiona we mwafrika ni takataka.

Ukiona mahali unapingwa sana au haukabaliki bila sababu jua kuna kitu unawazidi. Ni juhudi zako kujua wanateseka na nini juu yako.
usiangalie maisha ya watu wawili watatu kuwakilisha kundi la watu. mtanzania yupi wa kawaida umsemae, wakati kundi kubwa hawana uhakika na mlo wa leo? ambao ikitokea ajali ya gari ndio neema kwao kupata kwa kuiba? mwaka kesho subirikuna njaa, serikali tetemeko kagera ilikataa kutoa msaada kwa wahanga, kisingizio haikuleta tetemeko. masikini wa ulaya analipwa na kupewa pa kuishi, masikini wa kwako anachomwa moto akishikwa akiiba mkate.
 
Zamani walichukuliwa utumwani kwa lazima siku hizi wanagombea wenyewe tena kwa njia za panya au halali viza ubalozini.
Leo biashara ya utumwa ikirudi afrika sidhani kama kuna kijana atakubali kubakia afrika.
Yote hii chanzo ni watawala wa kiafrica wameshindwa kuwakomboa waafrika.

Kiongozi wa Africa naye anaamrishwa tu. Ukikataa ndo unawekewa vikwazo ni ngumu sana kwa wao kukataa. Mifano ipo hai tu kwa viongozi wa africa walioenda kinyume na matakwa yao. Anzia libya, Misri Iraq ingawa sio africa hata Zimbabwe walipata shida sana.
 
  • Thanks
Reactions: ba4
Uliyopost ni kweli kabisa Misss Chuga
Lakini pia njia nyingine wanazotumia ni chanjo.
Bill gate - jambazi kuu - aliwahi kusema kuwa "Tukifanya vema katika chanjo, tutaweza kupunguza population ....

Conclusion yako ni poa sana, kwamba:
//Na waasa sana Waafrika tujichunge sana maana Ongezeko letu sio pendezo kwa mataifa mengine. Chunga uhai wako tuwe wadadisi kwa vitu tunavyoletewa. Pia waafrika wenzangu tuwatunze watoto tunaowazaa kwa kuwalea vyema kwa kufanya kazi kuwalisha ili waweze kuwa imara wenye afya.//

Tatizo ni kuwa viongozi wengi wa Africa wako tayari kunyenyekea wazungu kwa sababu ya vijisenti, kiasi kwamba wako tayari kutoa sadaka waafrika wenzao. Mungu anawaona.
wazungu hawatii hela kwa viongozi wa Africa, wanajikaanga kwa mafuta yao wenyewe. viongozi wapora hela na kwenda kuficha huko kwa wazungu.
 
Zamani walichukuliwa utumwani kwa lazima siku hizi wanagombea wenyewe tena kwa njia za panya au halali viza ubalozini.
Leo biashara ya utumwa ikirudi afrika sidhani kama kuna kijana atakubali kubakia afrika.
Yote hii chanzo ni watawala wa kiafrica wameshindwa kuwakomboa waafrika.Ule msemo wa mwafrika hana uwezo wa kuongoza Jamii ikastawi unapata maksi.
Wakoloni walichukua raslimali kiduchu sana hata robo tu haifiki kulingana na raslimali tele zilizojaa na hazitumiki.
Wakoloni waliweza waletea waafrika maendeleo makubwa Sana ikiwemo kumaliza kabisa tatizo la ajira,masoko ya mazao yao nk.
Watawala wa kiafrica wameshindwa zitumia raslimali tele zilizojaa kuleta ustawi wa maendeleo wa kiafrica.
Matatizo ya mwafrika chanzo ni mwafrika mwenyewe chanzo cha vita congo ni ubinafsi wa mobutu.Congo itakuwa na amani siku kagame akifa, kagame na mseveni ndio wanufaika wakuu wa vurugu za Congo kwa kumiliki makundi ya waasi yanayoiba raslimali za Congo.
Hapa Mzungu anahusika vipi na ukosefu wa amani afrika, ubinafsi ndio chanzo cha vita na vurugu zote afrika.Ubinafsi ni tabia ya watawala wa kiafrica ni kama wapangaji yaani awatazami future ya afrika bali ustawi wa familia zao.
Great
 
Adui wa mwafrika ni mwafrika mwenyewe. Viongozi wetu hawako committed kuleta mabadiliko.
Tunapambana na adui mwingine wakati adui yetu tunaishi naye.
Waafrika ni rahisi kuamini hizi conspiracy theories .. hatujui kuchambua mbivu na mbichi hakika.
 
Sasa mbona bado wanawapa Visa kama hiyo ndo sababu?
Labda kama wanatuogopa kwasababu tunawapelekea mzigo badala ya ahueni.

Sheria inawalizimu kutoa visa kutotoa visa kunaambatana na sheria maalumu kwa nchi zilizo kubaliana Mahusiano
 
Sheria inawalizimu kutoa visa kutotoa visa kunaambatana na sheria maalumu kwa nchi zilizo kubaliana Mahusiano
Wakitaka hawakosi sababu ya kutowapa waafrika Visa. Kama Marekani anaweza kiuka makubaliano aliyoingia na washirika wake kama nchi za NATO ije kuwa sisi waafriak.
 
Tunataka kiongozi ambaye kiuhalisia anaishi maisha yanayoendana na hali ya wananchi.
Ebu fikiri, Angela Markel na kuwa kiongozi la taifa kubwa la Germany ambalo linatupatia mpaka misaada, lakini anaishi kwa mshahara wake na kukatwa kodi.

Huo huo mshahara ndiyo analipia makazi, chakula na kila kitu kama raia mwingine.

Sasa njoo nchi zetu hizi za Afrika, mtu akiwa kiongozi anakula mshahara mkubwa na marupurupu kibao na bado anapewa nyumba sijui gari yani ni kama mshahara wake hauna matumizi.

Ili viongozi wajue magumu mwananchi wa kawaida anayopitia ni lazima waishi kawaida bila hivyo tutaendelea kusikia kauli za tumeongeza 1000 tu, yani unashindwa changia serikali 1000 tu.

Hatujawa na kiongozi ambaye kiuhalisia anataka leta mabadiliko zaidi ya siasa tu.
Na ndio maana wanatuongezea tozo ili kukidhi mahitaji yao
 
Ata tuwe wengi kama siafu kama hatuna uwezo wakumiliki teknolojia sisi ni bure kama bure zingine.Matatizo ya afrika chanzo ni mwafrika mwenyewe.Hizo porojo zote ulizoandika hapo bado inaonyesha sisi wenyewe ndio tatizo kwasababu tungekua tunajitambua kamwe tusingekubali kutumiwa kijinga namna hiyo.Siku zote kitu duni ndicho kinachoteseka.Wingi wa waafrika dunia bado hautaweza kuleta jambo lolote kwa wazungu kwasababu mwisho wa siku bado mzungu atatutumia sisi kama nguvu kazi kwasababu yeye atakua anamiliki teknolojia uku sisi tukiwa wengi kwa idadi tusio na uhakika wa maisha bora wala afya ya uhakika.Tutakua tishio siku tutakayoanza kutumia vichwa vyetu vizuri kwenye mambo makubwa nasio kwasababu ya matumizi ya misuli au viungo vya uzazi.
 
Soma vizuri. Alafu inaonekana una uelewa mdogo kubali tu. Mnavyokuwa wengi ndo watu wa kila aina wanatokea wenye vipawa mbali mbali angalia India na China walianza na phonex baiskeli sasa hivi mnapanda Yutong. Me nimeandika waafrica wengi wanaenda ulaya kutafuta maisha na kuendeleza race yao ulaya na mataifa mengine.
 
Wakitaka hawakosi sababu ya kutowapa waafrika Visa. Kama Marekani anaweza kiuka makubaliano aliyoingia na washirika wake kama nchi za NATO ije kuwa sisi waafriak.

Kama waamerika wakizua visa kwa nchi za Afrika nazo hazitotoa visa za waamerika kuingia Afrika na elewe wao wamewekaza sana ktk nchi za Afrika
 
Back
Top Bottom