Hofu ya HIV inanitesa

Hofu ya HIV inanitesa

relis

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2015
Posts
3,336
Reaction score
5,217
Habari wakuu! Niende Moja Kwa moja katika story niliyopitia mwaka 2009 nilibatika kuanza kazi mkoa fulani Kwa kweli sikuwa mtu wa maneno mengi ni kazi tu Basi akatokea Binti mmoja. Tukapendana kijana nikajiweka. Bila tabu,nilikuwa muoga sana wa HIV Mimi na mwenzangu kabla ya kupelekeana moto afya ilizimgatiwa tulitafuta vipimo na kukagua afya na kujikuta safi kabisa.

Ndani ya mwaka na yule demu wivu ukawa mwingi nikaamua kubeba begi tukaachana bila nongwa baada ya miezi michache nikaamua kwenda kukagua afya kucheki Ngoma,nikaenda kama Leo wakatoa damu Kwa kipimo Cha rapid test kutokana na muda nikatoka na kurudi baadae kusomewa majibu nikaonekana HIV+ Kwa kweli niliona kama Dunia imenielemea na kutamani kufa nilipungua uzito Kwa stress hata nilipoambiwa nirudi sikurudi Kwa ajili ya vipimo vya mara ya pili,

2011 nikapata demu mwingine huku hofu ikitanda kuwa naua mtoto wa watu 2012 nikaona maisha yakaendelea 2015 akajaaliwa kupata mtoto na hata klinic sababu kibao sikupima mtoto wa nne sasa swali najiuliza je, uwezekano wa kuwa HIV+ upo ama la na watoto wapo salama elimu kwenye hili
 
Kama ulipima ukaambiwa ni positive hakuna namna utakuja kupima uambiwe negative.

Toka uambiwe positive Nina uhakika Kuna ushauri ulipewa ila ukaupuuza .

Umezingua sana kwenda kutembea na mtoto wa watu Ili Hali una maambukizi, Kwa ujinga wako Kuna uwezekano hata hao watoto wanne ukawa umewaambukiza maradhi .

Jitambue sikiliza ushauri wa wataalam wa afya na uchukue hatua mapema.
 
Mh? Kwanza sharti la kwanza ukienda kujifungua ni kupima ngoma ili wakushauri jinsi ya kumkinga mtoto dhidi ya maambukizi. Sasa unasema una watoto wanne hujawahi ulizwa au kusikia habari hiyo! Baasi kuna mawili! Wewe ni safi, au wewe ni carrier huwezi ambukiza! Kuambukiza ukimwi mpaka mchubuko! Labda manzi ana mdebwedo kiasi cha kutomchubua! Rudi hospitali ukapime labda Mungu yuko upande wako!
 
Amekuambia hajawahi kwenda clinic Kwa watoto wote wanne
 
Kapime teena bwana, kuna ndugu yangu ane alipimwa na hiyo Rapid test akakutwa nao. Alinipigia simu analia km mtoto. Nikamwambia usianze dozi mpaka nije likizo tufanye vipimo upya. Maana nae yule tapeli tapeli mpaka wake za watu. Nilipofika tukaenda hosp wakampima hana tena walitumia hiyo rapid test. Wakachukua Gold test sijui wataalam watajua hana pia. Yaani alipagawa dogo alivua shati, akawa anajipepea.
Nikamwambia bahati yako ungekunywa hizo mbaazi mpk mwisho wa maisha yako.
 
Mh? Kwanza sharti la kwanza ukienda kujifungua ni kupima ngoma ili wakushauri jinsi ya kumkinga mtoto dhidi ya maambukizi. Sasa unasema una watoto wanne hujawahi ulizwa au kusikia habari hiyo! Baasi kuna mawili! Wewe ni safi, au wewe ni carrier huwezi ambukiza! Kuambukiza ukimwi mpaka mchubuko! Labda manzi ana mdebwedo kiasi cha kutomchubua! Rudi hospitali ukapime labda Mungu yuko upande wako!
Au jamaa anakula kiboss,kamoja dk 2 afu mpaka baada ya siku 2
 
2009 hadi leo mwili ungeshaanza kujibu mapigo. Yani 16yrs uishi nao bila kupata dalili zozote, mmh!
 
Unajua kuwa unaweza kushtakiwa na kufungwa kwa kitendo cha kuingia kwenye mahusiano ukijua kuwa una uwezekano wa kuwa HIV+ na kutomwambia mwenzi wako?

Kwanini uishi kwa bahati nasibu? Nenda kapime tena upate uhakika.
 
Habari wakuu! Niende Moja Kwa moja katika story ya kweli niliyopitia mwaka 2009 nilibatika kuanza kazi mkoa fulani Kwa kweli sikuwa mtu wa maneno mengi ni kazi tu Basi akatokea Binti mmoja. Tukapendana kijana nikajiweka. Bila tabu,nilikuwa muoga sana wa HIV Mimi na mwenzangu kabla ya kupelekeana moto afya ilizimgatiwa tulitafuta vipimo na kukagua afya na kujikuta safi kabisa.

Ndani ya mwaka na yule demu wivu ukawa mwingi nikaamua kubeba begi tukaachana bila nongwa baada ya miezi michache nikaamua kwenda kukagua afya kucheki Ngoma,nikaenda kama Leo wakatoa damu Kwa kipimo Cha rapid test kutokana na muda nikatoka na kurudi baadae kusomewa majibu nikaonekana HIV+ Kwa kweli niliona kama Dunia imenielemea na kutamani kufa nilipungua uzito Kwa stress hata nilipoambiwa nirudi sikurudi Kwa ajili ya vipimo vya mara ya pili,

2011 nikapata demu mwingine huku hofu ikitanda kuwa naua mtoto wa watu 2012 nikaona maisha yakaendelea 2015 akajaaliwa kupata mtoto na hata klinic sababu kibao sikupima mtoto wa nne sasa swali najiuliza je, uwezekano wa kuwa HIV+ upo ama la na watoto wapo salama elimu kwenye hili
Mkuu andika vizur ueleweke watoto wa 4 na hujawai kwenda hospital?? Mke naye hana dalili za kuwa HIV+ Ila wewe ni Hiv+ mmmh!!!
 
Back
Top Bottom