Hofu ya HIV inanitesa

Hofu ya HIV inanitesa

Rapid test inapima uwepo wa virus kwenye sample, not necessarily HIV, ndio maana inahitajika confirmatory test , sasa wewe kuona tu ni postive ukakimbia
 
Mkuu wewe Ukimwi unao 💯 Ila watoto wanaweza wakawa nao au wasiwe nao. Fika kituo cha Afya mapema kwa ajili ya ushauri zaidi
 
Inawezekana unao na hujaambikiza au vipimo havikusoma sahihi ulivyopima. Case kama yako zipo unaweza kua na virus ila mwenzio asipate bila kutumia dawa wala kinga.

Cha msingi kapime uwe na uhakika. Uliwezaje kutofika clinic kwa watoto wote wanne?
 
2018 nilienda kupima pale Muhimbili clinic za wazazi pale. Yule nesi alituchukua damu, Lakini zili karatasi na vile Vi rapid test akakandamizia. Alafu kafungua feni mpaka mwisho aisee mikaratasi inapepea nikasema huyu dada huyu. Sasa karatasi zikichanganyika hapa za X zikaenda kwa Y si balaaa. Lakini bahati nzuri tuliopima tulikuwa couple (pair) zoote tulikuwa vizuri aisee. Nilisubiri yale matokeo kwa hofu kubwa sana.
 
Aende clinic kwani yeye mwanamke? Kama mke wake angekuwa kamwambukiza angeambiwa kabla ajajifungua na angemwambia mme wake mleta mada!
Nyie ndo mnaambukiza watu magonjwa kwa kujihesabia haki, aliyekwambia kwamba mkeo akipima hana maambukizi basi na wewe huna nani??
Wanapowaita wote kwa pamoja ili iwe rahisi kuwasaidia kumlinda mtoto km mmoja wenu kaathirika..!!
 
Ni mda wa kufunga zipu na kuibana kwa lufuli hadi hali ikae sawa🤣
Serious,. Vinginevyo ni kupukutika😂😃😃
Nakumbuka ile Novel ya " Passed like a Shadow" shwaaaa!
 
Habari wakuu! Niende Moja Kwa moja katika story niliyopitia mwaka 2009 nilibatika kuanza kazi mkoa fulani Kwa kweli sikuwa mtu wa maneno mengi ni kazi tu Basi akatokea Binti mmoja. Tukapendana kijana nikajiweka. Bila tabu,nilikuwa muoga sana wa HIV Mimi na mwenzangu kabla ya kupelekeana moto afya ilizimgatiwa tulitafuta vipimo na kukagua afya na kujikuta safi kabisa.

Ndani ya mwaka na yule demu wivu ukawa mwingi nikaamua kubeba begi tukaachana bila nongwa baada ya miezi michache nikaamua kwenda kukagua afya kucheki Ngoma,nikaenda kama Leo wakatoa damu Kwa kipimo Cha rapid test kutokana na muda nikatoka na kurudi baadae kusomewa majibu nikaonekana HIV+ Kwa kweli niliona kama Dunia imenielemea na kutamani kufa nilipungua uzito Kwa stress hata nilipoambiwa nirudi sikurudi Kwa ajili ya vipimo vya mara ya pili,

2011 nikapata demu mwingine huku hofu ikitanda kuwa naua mtoto wa watu 2012 nikaona maisha yakaendelea 2015 akajaaliwa kupata mtoto na hata klinic sababu kibao sikupima mtoto wa nne sasa swali najiuliza je, uwezekano wa kuwa HIV+ upo ama la na watoto wapo salama elimu kwenye hili

Nenda kituo cha afya kapime ili uwe na jibu moja tu, unayo au huna.

Kila la kheri.
 
Toa hofu kapime tena utupe mrejesho, wapo waliopima zaidi ya mara Moja nakupata majibu tofauti, "nothing kills as does fear". Be strong.
 
Mwili wa binadamu una siri nyingi mno ambazo hata sayansi pengine hauzijui. Amini katika nature.

We endelea na maisha, ukiumwa malaria katibu malaria, ukiumwa kifua katibu kifua. Piga msosi balance diet, Epuka Junk Food kama masoda soda, sijui energy drinks. Haya magonjwa imported yasikutusue akili sana,
 
Habari wakuu! Niende Moja Kwa moja katika story niliyopitia mwaka 2009 nilibatika kuanza kazi mkoa fulani Kwa kweli sikuwa mtu wa maneno mengi ni kazi tu Basi akatokea Binti mmoja. Tukapendana kijana nikajiweka. Bila tabu,nilikuwa muoga sana wa HIV Mimi na mwenzangu kabla ya kupelekeana moto afya ilizimgatiwa tulitafuta vipimo na kukagua afya na kujikuta safi kabisa.

Ndani ya mwaka na yule demu wivu ukawa mwingi nikaamua kubeba begi tukaachana bila nongwa baada ya miezi michache nikaamua kwenda kukagua afya kucheki Ngoma,nikaenda kama Leo wakatoa damu Kwa kipimo Cha rapid test kutokana na muda nikatoka na kurudi baadae kusomewa majibu nikaonekana HIV+ Kwa kweli niliona kama Dunia imenielemea na kutamani kufa nilipungua uzito Kwa stress hata nilipoambiwa nirudi sikurudi Kwa ajili ya vipimo vya mara ya pili,

2011 nikapata demu mwingine huku hofu ikitanda kuwa naua mtoto wa watu 2012 nikaona maisha yakaendelea 2015 akajaaliwa kupata mtoto na hata klinic sababu kibao sikupima mtoto wa nne sasa swali najiuliza je, uwezekano wa kuwa HIV+ upo ama la na watoto wapo salama elimu kwenye hili
pole sana. kwa lugha nyepesi, hapa mlikutana wote wawili mkifichana hali zenu, ila mwenzio anakinga watoto anaozaa. Mungu akusaidie upite vyema katika safari hio. Mkumbuke Mungu kwanza, and where you will spend your eternity, bila kuokoka ni motoni, hivyo andaa maisha yako ukiwa hai ili kule utakakoenda pawe pazuri milele. hii sio kwa waliougua ngoma tu, hata walio wazima kwani wanakufa ghafla kwa ajali au vifo vingine, andaeni maisha yenu ya milele, mtakuwa wapi> mpeni Yesu maisha, okoka ili maisha yako ya sasa na ya baadaye yawe mikononi mwa Yesu.
 
Ni 2009? Au na 2019, mbona ni miaka mingi sana.
ngoma huwa inaweza kukaa hata 10 years mwilini na upo fresh tu. ila ikija kufumuka ndio hivyo tena. hata hivyo nina ndugu yangu ana 30 years now tangu atambulike kama anayo.
 
Back
Top Bottom