Hofu ya HIV inanitesa

Hofu ya HIV inanitesa

Mh? Kwanza sharti la kwanza ukienda kujifungua ni kupima ngoma ili wakushauri jinsi ya kumkinga mtoto dhidi ya maambukizi. Sasa unasema una watoto wanne hujawahi ulizwa au kusikia habari hiyo! Baasi kuna mawili! Wewe ni safi, au wewe ni carrier huwezi ambukiza! Kuambukiza ukimwi mpaka mchubuko! Labda manzi ana mdebwedo kiasi cha kutomchubua! Rudi hospitali ukapime labda Mungu yuko upande wako!
Carrier yeye virus havimsumbui lakini anaambukiza kama wengine.
 
Aende clinic kwani yeye mwanamke? Kama mke wake angekuwa kamwambukiza angeambiwa kabla ajajifungua na angemwambia mme wake mleta mada!
Yeah nimewaza kama hivyo pia,huyo mwanamke angekuwa muathirika angeambiwa amlete mzazi mwenzake kwa njia yoyote ile jamaa angesakwa mtaani.
Sasa sijajua huyu jamaa sijui alipima zahanati wapi akaambiwa positive isije ikawa kuna makosa fulani yalifanyika,lakini hakuna suluhisho la hili jambo zaidi ya kwenda kupima tena kuthibitisha kwa usalama wake pamoja na familia yake.
Uzembe wa kuogopa kwenda kupima ni hatari cha msingi ni kujitoa Muhanga tu siku moja na kwenda kupima hakuna namna.
 
Habari wakuu! Niende Moja Kwa moja katika story niliyopitia mwaka 2009 nilibatika kuanza kazi mkoa fulani Kwa kweli sikuwa mtu wa maneno mengi ni kazi tu Basi akatokea Binti mmoja. Tukapendana kijana nikajiweka. Bila tabu,nilikuwa muoga sana wa HIV Mimi na mwenzangu kabla ya kupelekeana moto afya ilizimgatiwa tulitafuta vipimo na kukagua afya na kujikuta safi kabisa.

Ndani ya mwaka na yule demu wivu ukawa mwingi nikaamua kubeba begi tukaachana bila nongwa baada ya miezi michache nikaamua kwenda kukagua afya kucheki Ngoma,nikaenda kama Leo wakatoa damu Kwa kipimo Cha rapid test kutokana na muda nikatoka na kurudi baadae kusomewa majibu nikaonekana HIV+ Kwa kweli niliona kama Dunia imenielemea na kutamani kufa nilipungua uzito Kwa stress hata nilipoambiwa nirudi sikurudi Kwa ajili ya vipimo vya mara ya pili,

2011 nikapata demu mwingine huku hofu ikitanda kuwa naua mtoto wa watu 2012 nikaona maisha yakaendelea 2015 akajaaliwa kupata mtoto na hata klinic sababu kibao sikupima mtoto wa nne sasa swali najiuliza je, uwezekano wa kuwa HIV+ upo ama la na watoto wapo salama elimu kwenye hili
Hukuambiwa positive ila uliambiwa urudie kipimo
Ki kawaida majibu ya positive huwa ni baada ya kipimo cha pili!
Kama ulipima kipimo kimoja hyo wanasema NON REACTIVE
 
Back
Top Bottom