Hofu ya kunguni Ufaransa

Hofu ya kunguni Ufaransa

View attachment 2771374


Wananchi wa Ufaransa pamoja na watalii wanaoitembelea nchi hiyo wanaugulia maumivu baada ya kungátwa na kunguni ambao wamesambaa katika maeneo mengi hasa ya umma.

Kufuatia kuwepo kwa picha mbalimbali za video mitandaoni zikionesha kuwepo kwa wadudu hao hasa katika jiji la Paris kwenye treni za mwendokasi, hospitali, nyumba za sinema na uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Charles-de-Gaulle, Serikali ya Ufaransa imesema inaelekeza juhudi zake katika kupambana na kunguni hao.

"Jimbo linahitaji haraka kuweka mpango wa utekelezaji dhidi ya janga hili wakati Ufaransa inajiandaa kuwa mwenyeji wa michezo ya Olimpiki na Paralympic 2024," ameandika Naibu Meya wa Paris, Emmanuel Gregoire katika barua yake kwa Waziri Mkuu Elisabeth Borne.
Kunguni?

Au labd ni moja ya vivutio vya kitalii!
 
Kunguni hakai sehemu chafu tu
We humjui huyo mdudu akiingia ameingia.
Hata ikulu anaishi na anatamba vizuri
Hivi mkuu mazingira anayoishi kunguni na chawa ni tofauti?
 
Hivi mkuu mazingira anayoishi kunguni na chawa ni tofauti?
Chawa kichwani kunguni anajificha chini ya au kwenye mabanzi anataga humo kumbuka kunguni kutaga mayai haitaji kupandwa na dume kwa hio akipata sehemu yenye kitoweo Cha kutosha anataga mayai kwa wingi ukizima taa tu haoooo wanakuja ukipata usingizi tu haoooo wapo Shingoni wanakunyonya damu
 
Kunguni unaweza ukamtoa kwenye Gari la mbagara akiwa mmoja ukawa umemleta kwako akiwa mmoja tu akiingia uvunguni mwa Kochi anataga kunguni wengine 200 haitaji dume ili atage mayai
bora upambane na mbu unayemuona kuliko kupambana na kunguni aliyejificha mafichoni ukizima taa tu anakunyonya damu. Kunguni ni mdudu mshenzi sana, mbu akasome kwake
 
Walikufanyaje ,😆
Walinipa elimu ya kujua sumu ya yenye uwezo wa kumuua kunguni inapaswa kumuua na mtu pia.

Nilienda kwenye duka moja la dawa za mifugo nikaona dawa moja ambayo nilikuwa namuona dingi akinyunyuzia kuua sisimizi.

Nikamuambia muuzaji hii dawa naijua ina nguvu sana ebu nipatie itanifaa.

Hapo kunguni hata siwajui.

Muuzaji akaniambia "kama unataka kuitumia kwa ajili ya kupata usingizi usiku mmoja sawa"

Akanitisha ikabidi nimshangae kwanza nikafikiria kuwa katumia lugha ya biashara ili nimuungishe bidhaa yenye bei kubwa ili apate faida.

Nikasema nachukua zote. Akanipa zote na nikanunua na ile spray yake

Kweli nilipofika home nikajionea mwenyewe kuwa ile dawa haikuwa kitu kwa kunguni.

Kesho yake mi nikaondoka home, narudi baadaye natafuta spray siioni.

Kuuliza kumbe kuna jirani ameazima.

Nikawa najiuliza ameazima spray kwa ajili ya kazi gani ina maana naye ana kunguni?

Nilipoenda kuichukua nikakuta naye kuna mtu kamuazima, ikabidi anielekeze, huko ndio nikankuta jamaa amevua na shati katoa godoro nje anapulizia kunguni.

Jamaa alikuwa akimuona kunguni anampulizia dawa ya kutosha halafu anatulia kumsikilizia baada ya muda kujua amekufa, dawa imekolea .

Unakuta akiacha tu kupulizia baada ya muda kidogo yule kunguni anaanza kutembea tena jamaa ana sonya tu.
 
Back
Top Bottom