Hofu ya maambukizi ya VVU inanimaliza kiafya, nilishiriki ngono na muathirika wa UKIMWI

Asee wewe ni muoga sana mkuu!
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Mkuu uzi wetu umekukosea nini...
Hahahaha watu wakiwaza naku soma comment za ukimwi humu gear inacharge kabisa...wanaanza kurequest nyuzi za minyegezo zifutwe mapema
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Wanaume tuna kazi sana.
Unasema siku ya kufa nyani miti huteleza.
Mkuu ondoa hofu,nakumbuka hiyo hali iliwahi kunikuta kipindi fulani hivi kuna binti nilimuonaga fb alikuwa anasoma chuo fulani hivi basi nikamfukuzia kwa muda mrefu akawa hasomeki sasa baadae alivyomaliza chuo akarudi dar ni baada ya miaka 3.
Nikajaribu kutupa ndoano mtoto akajaa nikaenda kumla kimasihara japo nilitumia kinga.
Ikapita kama miezi 3 hivi nikapata typhoid ikanisumbua sana na mimi sijawahi kuumwa typhoid serious kama kipindi kile maana nilimeza dawa nikahisi kama ndio inazidi.
Sasa wakati nimejilaza yule demu akanitext.
Demu:Mambo my
Mimi😛owa niambie
Demu:Ndio nini kuniambukiza ukimwi mwenzio?
Mimi:Nilinyong'onyea Pumzi ikapanda nikajikaza kisha nikamjibu,una uhakika ni mimi
Demu:Ndio ni wewe maana mimi nina miezi 6 sijakutana na mwanamme mwingine.
Mimi:Mapigo ya moyo yakaongezeka nikajikaza na kumjibu,lakini mbona tulitumia kinga?
Demu:Hapana nakumbuka uliivua
Mimi:Una uhakika uyasemayo
Demu:Lakini Mungu anakuona,umeamua kuniua mtoto wa watu,sawa bhana,wewe si umenikomoa.
Majadiliano yaliishia hivi basi nikaishiwa nguvu nikalala usiku mzima nikifikiria dah itakuwaje sasa.
Basi unaambiwa kuanzia ile wiki nikaanza kukonda na kukata tamaa nikasema ndio basi tena kumbe hii homa kali inayonisumbua ni kwa ajili ya HIV.
Hiyo hali ikanitesa kama mwezi mmoja hivi,sasa baadae nikasema potelea mbali ngoja nikapime nijiandae tu kuanza kutumia ARV.
Nikaenda Hospitali ya wilaya nikaingia nikajiandikisha mapokezi nikaenda kukaa foleni,lakini nilionekana mnyonge sana kuliko watu wote yaani sikuwa na amani kabisa.
Baadae ikafika zamu yangu nikakutana na madokta wawili vijana wadogo wa kike na mwingine wa kiume wenye miaka kati ya 27 hadi 30.
Wakanikaribisha vizuri kisha wakaanza kunihoji sababu ya mimi kuamua kwenda kupima,endapo nitakutwa muathirika nitachukua hatua gani na stori nyingi za hapa na pale.
Walikuwa very charming wakanifanya ile huzuni yangu ipotee nikaanza kutabasamu.
Baadae wakaniuliza uko tayari kwa kupima nikawajibu ndio,wakanitoboa na kuchukua sampo ya damu.
Nikangoja kama dakika 5 hivi majibu yakawa tayari kisha wakaniuliza,upo tayari kupokea majibu?mimi nikasema ndio.
Wakanijibu"Majibu yako yanaonesha uko Negative yaani hauna maambukizi ya ukimwi.
Unaonekana wewe ulikuwa mtu makini huwa unazingatia kutumia zana wakati wa tendo na pia huwa huchukui wanawake ukiwa umelewa kupitiliza yaani wakati wote huwa unachukua mwanamke wakati upo katika hali ya kujitambua hicho ndicho kilichokusaidia.
Aisee nilipata furaha ya ajabu,nikaingiza mkono mfukoni nikatoa noti ya elfu 10 nikawapa wale madokta nikawaambia mtakunywa soda asanteni na kwaherini.
So nilivyoona kisa chako hiki nikakumbuka hii stori yangu ni kama zinaendana.[emoji38]
 
siku hizi kuna arv nameza kidonge kimoja kwa mwaka, tatizo hamuongei na watu vizuri.
 
Duuh
 
Niliwahi kabla ya 72hrs kuisha, na kila week napima mpaka mda huu navoandika hapa sina maambukizi ila ninahofu sana, nasubiri nijitazamie miezi 4 to 5
Kupima kila wiki au kila siku ni sababu ya stress tu Ila inatosha ulivyopima kabla ya kuanza kingatiba, baada ya kumaliza dawa na miezi 3 baadae...ikiwa negative bas inabaki hivyo forever labda upate maambukizi mapya, muhimu ni kujiepusha na mazingira hatarishi kama ya ulevi ambapo unaweza kufanya maamzi bila kutumia utashi wako, kifupi ni kama unakua umejibaka mwenyewe maana kimsingi unakua umefanya tendo hilo bila nafsi yako kuridhia ndio maana ulevi ukiisha, nafsi inakusuta kuwa hujaitendea haki....ni sawa na kufanya maamzi ukiwa na hasira sana au furaha sana, utafanya maamzi yasiyo sahihi na kujutia baadae. Mungu atusaidie sana.
 
Niliwahi kabla ya 72hrs kuisha, na kila week napima mpaka mda huu navoandika hapa sina maambukizi ila ninahofu sana, nasubiri nijitazamie miezi 4 to 5
Relax hofu inaua haraka sana kuliko huo ugonjwa unaohofia
 
Mhhh! Naona Wazinzi wanatiana Moyo, huu Uzi sio wangu, ngoja nipite hivi.
 
Nina mademu wawili. Wote wana huo ukimwi wenu feki tena kwa kuwapima mwenyewe kwani walikuwa hawaamini kwamba naweza kuwa nao ili hali wao ni positive mm negative. Nakung'uta kavu na niko sawa kabisa
Jamani mutahadhari na wachawi kama hawa, wanawadanganya ili muweze kuingia kwenye mtego
 
Nina mademu wawili. Wote wana huo ukimwi wenu feki tena kwa kuwapima mwenyewe kwani walikuwa hawaamini kwamba naweza kuwa nao ili hali wao ni positive mm negative. Nakung'uta kavu na niko sawa kabisa
Usipotoshe mzee ila nakubaliana na wee nin jamaa angu nae kwa kujuwa kuwa bint amezaliwa nao huo ugonjwa lkn bint kanona kweli Ila jamaaa kwa kuona tunda zuri akaamuaa kumtafuna hvyo hvyo mpk Leo Hana huo ukimwi hiki Ni kisa Cha kweli kbsa
 
Usipotoshe mzee ila nakubaliana na wee nin jamaa angu nae kwa kujuwa kuwa bint amezaliwa nao huo ugonjwa lkn bint kanona kweli Ila jamaaa kwa kuona tunda zuri akaamuaa kumtafuna hvyo hvyo mpk Leo Hana huo ukimwi hiki Ni kisa Cha kweli kbsa
Mimi nimepotosha. ila kwa jamaa yako yeye ni kweli. Dunia haitaisha maajabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…