kindikwili
JF-Expert Member
- Oct 5, 2016
- 1,862
- 2,876
Habari iwe nanyi wakuu!
Kwanza niseme wazi kuwa hakuna jambo kubwa katika maisha kama kujitambua, kutambua utu na thamani yako. Mtu anayejitambua na kutambua utu wake hata akiwa na njaa kiasi gani hawezi kula chakula kilichopakwa mate na mtu aliyeshiba. Kama atafanikiwa kukishika atakirusha chini mbele yako kwani ataona umemdharau. Kweli njaa haina bouncer ila mwenye utu hawezi kula chakula cha nguruwe
Katika hama hama hii ya kutoka upinzani kwenda ccm kuna nadharia nyingi sana. Baadhi ya nadharia hizo ni kama ifuatayo
1. Kuna mgogoro ndani ya upinzani hasa chadema- Ukiwasikia wana nadharia hii kwa haraka haraka bila ya kufikiri vyema unaweza kuamini kwamba hama hama hii ni kwasababu ndani ya chadema kuna mgogoro.
Lakini ukifiri kwa kina unaweza kujiuliza ni mgogoro upi haswa uko CHADEMA kwa mfano, huo mgogoro umewaathiri vipi na kwa kiwango gani wanaohama? Je kwani huko wanakohamia hakuna mgogoro wowote?
Je kwani tangu upinzani uanze hakujawahi kuwa na migogoro mikubwa ndani ya upinzani? kama imewahi kuwepo kwanini watu hawakuhama vyama? Inawezekana CHADEMA kuna mgogoro ila hiyo siyo sababu haswa ya hama hama hii.
2. Utendaji uliotukuka wa serikali ya awamu ya tano- Wanaohama wana nadharia yao kwamba wanahama kwasababu wamemuelewa sana mheshimiwa Rais na serikali yake.
Kwamba anafanya yale ambayo wao kama wapinzani walikuwa wanayapigania siku zote hivyo wanaona hamna haja tena ya kuwa mpinzani bora waungane naye kwa kuunga juhudi. Huu mtazamo unashabikiwa na baadhi ya watu hasa wanaopokea wageni lakini nadhari hii inamapungufu mengi. Inaonesha kwamba wahamaji hawajui hata maana ya vyama vya upinzani na kazi zake pamoja na dhamiri ya chama cha upinzani.
Dhamira kuu ya chama cha upinzani ni kushika dola (kushinda uchaguzi na kuunda serikali), sasa itakuwa ni uwendawazimu mtu mwenye ndoto za kuunda serikali kusifu yanayofanywa na chama tawala. Yaani upinzani uanze kusema chama tawala wanafanya vizuri sana katika kila jambo na wanastahili kuungwa mkono.
Hata kama wanafanya vizuri watatafuta ubaya kwenye huo uzuri ili kushawishi wananchi. Kwahiyo mpinzani mwenye dhamira ya kweli hawezi kuhamia chama tawala hata kama wangefanya mazuri yote kwa muda mfupi na kwa namna nzuri kiasi gani.
3.Wananunuliwa na kushawishiwa kwa ahadi mbali mbali - Hii nadharia inazungumzwa sana na wale wanaoachwa, lakini kujua kama hii nadharia ina ukweli ama la tuangalie chimbuko la hama hama hii.
Chimbuko la hama hama hii ni jimbo la Arumeru Mashariki ambapo madiwani wa wali wa chadema walihamia CCM na siku chache baada ya hapo aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo alikuja na video clips zikimuonesha aliyekuwa mkuu wa wilaya hiyo akiwashawishi madiwani hao kuhamia CCM tena kwa ahadi ya kupewa udiwani uchaguzi ukirudiwa (washinde wasishinde).
Kweli uchaguzi uliporudiwa walishinda. Hakuna mbunge wala diwani aliyehamia CCM ambaye hakurudi kwenye nafasi yake, walikaribishwa na kupewa nafasi ya kugombea bila kufuata utaratibu wa chama na kushinda tena. Kuna wakati moja kiongozi fulani alisema CCM ilikubaliana nao kwanza kabla ya kuhamia. Hii nadharia ndiyo ambayo kwa mtazamo wangu unashika nafasi ya kwanza kwa wakati ule na nafasi ya pili kwasasa.
4. Dhamira ya kufuta upinzani tanzania kabla ya uchaguzi wa 2020- Hii nadharia pia inasemwa na wanaohamwa tena wanamnukuu kiongozi fulani wa ccm kwamba aliapa kufutilia mbali upinzani na kwamba mbinu hizi ni mkakati wa kutekeleza dhamira yake hiyo. Wanadai kutimiza lengo hilo ccm inatumia ushawshi, rushwa ya fedha na vyeo kudhoofisha upinzani na kuijengea upinzani taswira mbaya mbele ya wapiga kura. Hii nadharia pia ina mashiko na haiwezi kubezwa
5. Hofu ya kurudi kwenye nafasi baada ya uchaguzi ujao- Hii nadharia kwa upande wangu ndiyo inayoshika nafasi ya kwanza ya kwanini hama hama imezidi na itazidi sana. Watu wameanza kupata hofu kwa kauli na matendo ya watawala kumbuka usemi maarufu wa (nikuteue nikupe gari halafu unamtangaza mpinzani).
Kauli na matendo yanayoambatana nayo umefanya wapinzani waliojenga upinzani wao kwenye mchanga wa madaraka watikiswe haswa, kupatwa na uoga wa kupoteza nafasi zao na kufikiri kwamba walau kwa kuhamia CCM wanaweza kuambulia walau nafasi hizo au nafasi za kuteuliwa. Hii hofu imerahisisha kazi ya wanaoshawishi wapinzani kuhamia CCM na kama kweli wanalipwa basi hata thamani yao imeshuka sana kwani tayari washakufa kwa hofu.
Kadri hofu ya kupoteza nafasi unavyozidi kuelekea uchaguzi mkuu bado tutashuhudia wapinzani maslahi wengi sana wakihamia CCM maana huko kama watapitishwa na chama uwezekano wa kutangazwa washindi ni asilimia kubwa washinde wasishinde. Lakini hata wakishindwa kuna ukuu wa wilaya, ukurugenzi wa halmashauri, ukatibu tawala na vyeo vya uteuzi kibao.
6. Kuchelewa kwa fursa ndani ya upinzani- Hii nadharia inatetewa na wanaohama kwamba ndani ya upinzani fursa za kupata maisha ni chache na hazina maslahi. Ili upate fursa ni lazima upate ubunge, ambao nao hata kutangazwa ni shida. Lakini ndani ya CCM fursa zipo tela mfano ukuu wa wilaya , ukuu wa mkoa, ukurugenzi nk. Julius mtatiro na Dk Mashinji waliliweka vizuri sana wakati wakiomba kuhamia CCM.
Wanajiuliza kama Moses Machali, Kafulila, Prof Mkumbo, Anna Mghwira , Katambi etc wameula huko CCM bila jasho baada ya kusota upinzani kwanini wao waendelee kuhangaika huko upinzani?
Mwisho niseme tu kuwa lengo letu ni kujenga nchi yenye ustaarabu, unaoheshimu haki za kila raia na wenye mafanikio kiuchumi na kijamii. Siasa siyo vita , vyama vitapita ila nchi itabaki mpaka kurudi kwa Yesu (kwa wanaoamini). Tuunge mkono serikali pale inapofanya mazuri si lazima kwa kuhama chama na tukosoe pale inapobidi .
ILA KWA WAHAMAJI MNAJITIA MHUHURI AMBAO HAUTAFUTIKA KIRAHISI KWENYE PAJI LA NYUSO ZENU.
Karibuni kwa mjadala bila matusi lakini
Kindikwili-Masasi