Hofu Yatanda Kwa sisi Washabiki wa timu ya Wananchi

Rajab_Omar

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2016
Posts
16,482
Reaction score
27,182
Naanza na Salamu ya Daima Mbele Nyuma Mwiko.

Mimi nikiwa Mwanachama na Mfuasi wa Timu ya Wananchi Kindakindaki kwakweli Mpira walioucheza Simba SC Jana dhidi ya Biashra United umetushituwa sana sisi Maelfu ya Wanachama wa Young Africans Sports Club na kuzua taharuki itakuwaje siku tutakayokutana nao!

Simba wameonesha uwezo wa hali ya Juu sana kwa kucheza mpira safi na wenye akili nyingi huku tukishuhudia vipaji vikubwa kwa ngazi ya Africa kama Konde Boy, Bwalya na Chama.

Nisiwe mnafiki Chama mmoja tu ni zaidi ya Kikosi chetu kizima cha Yanga. Kwasasa ninamlaumu Senzo tu aliyetudanganya kuwa Chama anakuja kwenye Timu yetu ya Wananchi.

In fact sisi Yanga kuna umuhimu wa kubadilika katika uendeshaji wa Timu ili tuendane na Kasi ya Simba ambaye niwazi kuwa na mwaka huu anakuwa Bingwa tena.
 
Vijora FC[emoji1550][emoji1550][emoji1550][emoji1550][emoji1550]
 
Katika historia ya soka ya nchi hii Simba ndio timu iliyofungwa maranyingi zaidi na Yanga kuliko timu yoyote. Kwaiyo mbumbumbu fc hajawai kuwa tishio kwa yanga.
Vijora fc
 
Hivi huko Simba mmesomea wapi propaganda? Wakati wa Sadam Hussein kilikuwa na mtu mmoja anaitwa nadhani Al Sahef..jina Kama Hilo ingawa sijapatia Sana...Ujerumani ya Hitler kulikuwa na propagandist anayeitwa Goebbels.

Simba wana propagandist wengi wakiongozwa na anayejiita msemaji wa klabu hiyo...yaani mikia wameleta Aina mpya ya uendeshaji wa soka...kutumia propaganda, kujaza viongozi TFF na kamati zote...kuhonga marefarii...yaani soka inaendeshwa kwa mipasho.

kwenye kupanga ratiba mikia nako wako...kwenye kupanga waamuzi mikia wamejaa...kwenye kamati zote mikia wamejaa...yaani maamuzi yanayotolewa ni ya kushangaza...msemaji wa mikia ameachwa atambe anavyotaka ...kudhalilisha timu na klabu nyingine...dah...Lakini mwisho wake ni mbaya that is for sure...this empire in soccer will crumble...kwa Sasa mikia wanatamba lakini hii siyo ya kudumu...Kuna Kila dalili kwamba empire itabomoka..na kwa hakika italeta mtikisiko wa kutisha..nimeandika...
 
Yanga si wamesema bado wanajenga muunganiko wa timu,wakikutana na Simba watafungwa nyingi labda mpaka msimu ujao timu ikiwa sawa ndo angalau wanaweza kuonyesha upinzani kwa Simba.
 
Katika historia ya soka ya nchi hii Simba ndio timu iliyofungwa maranyingi zaidi na Yanga kuliko timu yoyote. Kwaiyo mbumbumbu fc hajawai kuwa tishio kwa yanga.
Mavi ya kale hayanuki
 
Nadhani hata yale magoli manne ya jana yalifungwa na Wallace Karia,Wambura na Clifford Ndimbo.
 
Katika historia ya soka ya nchi hii Simba ndio timu iliyofungwa maranyingi zaidi na Yanga kuliko timu yoyote. Kwaiyo mbumbumbu fc hajawai kuwa tishio kwa yanga.
Kwa hiyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…