The Sunk Cost Fallacy 2
JF-Expert Member
- Nov 8, 2022
- 9,436
- 10,944
Hello!
Hofu imewakumba Wazazi kufuatia kuripotiwa Kwa taarifa kwamba Watoto wamekuwa Wakifundishwa kulawitiana wakiwa Mashuleni.
Shule ndio zilikuwa kimbilio la Wazazi lakini nako sio salama tena, kama jamii tunaelekea wapi?
Yale maadili ya Watznzania Yako wapi? Kila siku tunaingia makanisani na misikitini lakini maovu ndio kwanza yanazidi.
Ikiwezekana serikali ipige marufuku matumizi ya smartphone kwa vijana chini ya miaka 18 na kuwe na Sheria Kali ikibidi kunyongwa Kwa watu watakaobainika kuharibu Watoto Wetu.
Source: Nipashe.
👇
=======
Watoto wafundishwa kulawitiana shuleni
Shule binafsi kuna uchafu mwingi. Baada ya mume wangu kupata uhamisho wa kituo cha kazi, nami nilikwenda masomoni, tukalazimika kuwahamishia kwenye shule ya bweni watoto wetu wawili, Selina (si jina lake halisi) anasimulia mkasa uliojaa ukakasi wa yanayojiri kwenye baadhi ya shule nchini."
Selina, mkazi wa Manispaa ya Moshi na mzazi wa watoto wawili, anaendeleza simulizi yake, akisema kuwa kutokana na uhamisho huo wa kikazi, yeye na mumewe waliwapeleka shule binafsi watoto wao wawili - wa kike (7) na wa kiume (9) na baada ya mwaka mmoja walibaini mabadiliko hasi ya kitabia, hasa kwa mtoto wao wa kiume waliyempeleka kwenye moja ya shule binafsi zilizoko Moshi Vijijini.
"Baada ya mwaka mmoja kupita, nilirejea na kuwachukua wanangu kurudi shule za kutwa. Siku moja wakati ninaendelea na majukumu yangu, nilimwona kupitia dirishani mwanangu wa kiume akimfundisha mtoto wa jirani namna ya kufanya vitendo vya ulawiti.
“Nilisononeka na kukaa na mwanangu, nikamdadidi kwa nia ya kutaka kujua wapi alikojifunza tabia hiyo.
“Mwanangu alinieleza kuwa vitendo hivyo walifundishwa na patron (msimamizi wa kiume wa wanafunzi shuleni) wa ile shule nilikompeleka kwa mwaka mmoja.
"Alinieleza kuwa walikuwa wanafundishwa vitendo hivyo nyakati za usiku na walipewa onyo wasitoe taarifa kwa wazazi wala walimu huku wakiahidiwa zawadi mbalimbali, zikiwamo kalamu na penseli pamoja na kupewa fursa ya kuzungumza na wazazi kwa simu wanapopata shida," anasimulia.
Mama huyo anasema mwanawe alimweleza kuwa msimamizi huyo wa wanafunzi huwapatia watoto mafuta maalum ya kufanyia vitendo hivyo, kukiwa na utetezi kwamba mafuta hayo yanawaepusha kupata michubuko.
"Mwanangu aliniambia kwamba wavulana wa darasa la sita na la saba ndiyo huja kuwafanyia vitendo hivyo wanafunzi wa madarasa ya chini.
"Patron huwaambiwa ikiwa watakubali, wataanza kupakwa mafuta ili wasiumie na wale wanaowafanyia hivyo, watawasaidia majukumu mbalimbali ikiwamo kufua, kufuta viatu kuchukuliwa chakula na kununuliwa vitu mbalimbali na wakikaidi, patron angewachukulia hatua za kinidhamu.
"Baada ya kupata taarifa hizi, imenilazimu kuchukua hatua ya kuwatafuta watu wa kiroho pamoja na kumpeleka mtoto hospitalini, sijathubutu kumweleza baba yake, ila kiukweli tunaomba vyombo vya usalama vya mkoa vichunguze kwa kina, haya matukio yapo na ni ya aibu!" Selina analalamika.
MAJIRANI WA SHULE
Edwad Shirima, mkazi wa Mji wa Moshi, ana angalizo lake kimaadili, akidai vitendo hivyo vinachochewa na baadhi ya wamiliki wa shule hupokea fedha kutoka kwa watu wanaofadhili vitendo vya ushoga ili kuwa sehemu ya mkakati huo.
"Kuna shule moja inasemekana walimu wachache wanapewa taarifa juu ya miradi hiyo na kunakuwa na nembo zao, ila watekelezaji ni Patron.
"Kwa kweli kwa sasa hali ni mbaya, wazazi tuache kujikita katika kutafuta fedha, watoto wanaangamia," Shirima anatahadharisha.
Nehemia Munis, mfanyabiashara wa vitafunwa maeneo ya Stendi ya Moshi Mjini na mkazi wa Pasua, Manispaa ya Moshi, anasema mbali na ukatili unaofanywa na watoto kwa watoto chini ya viongozi wa shule, pia wapo vijana waendesha bajaj na pikipiki, maarufu bodaboda, ambao wamekuwa sehemu ya watu wanaowalawiti watoto wakati wanapowapeleka shuleni au kuwachukua kutoka shuleni kuwarudisha nyumbani.
“Mwaka jana watoto sita wa shule zilizopo katikati ya mji Muungano na Mawenzi walilawitiwa na dereva bajaj wakati wa kuchukuliwa shuleni.
"Tukiwa kijiweni siku moja, kuna mtoto akawa anatoka wadudu sehemu za siri na amekaa kwa masikitiko, tukamwita na kumhoji, akatueleza namna yeye na wenzake watano wanavyofanyiwa vitendo hivyo nyakati za kurejea nyumbani na dereva bajaj.
"Yaani huyo aliyepewa dhamana ya kuwaleta shuleni watoto, anawafanyia unyama. Tukachukua jukumu la kumpeleka shuleni na kuanika kilichokuwa kinaendelea," Munis anasema.
Elisante Mfuru, mkazi wa Sango wilayani Moshi, anashauri kila mwanajamii hana budi kufuatilia malezi ya watoto ili kuliepusha taifa kuwa na kizazi kilichopotoka kimaadili.
"Wapo watu watadai wazazi walaumiwe, ila mimi ninasema kila mmoja anapaswa kujitafakari kwa kuwa kuporomoko kwa maadili na utandandawazi kumechangia jamii kufika hapa tulipofika leo, jamii mzima tumejisahau," alisema.
WAZEE WA MILA
Elisaria Nkya (79), mkazi Narumu mkoani hapa, anawasilisha uzoefu wake kwamba zamani matukio hayo ilikuwa nadra kutokea, akinyoshea kidole wazazi kupeleka shule za bweni watoto wenye umri mdogo.
"Mtoto wa miaka miwili amepelekwa shule ya bweni ili mama asichoke, mila na desturi hazifuatwi tena, vijana wa miaka kuanzia 1990 na kuendelea hawajitambui, hawafuati maadili ya Mungu wala ya kimila. Ni kizazi kisichokuwa na maadili," anaonya.
Ni hoja inayoungwa mkono na Sebastian Kimaro (81), mkazi wa Rombo Mkuu, anayetaja kuporomoka kwa maadili, utandawazi na uvivu kwa vijana kutaka fedha za haraka kuwa chanzo cha tatizo.
"Zamani ukibainika umefanya tukio la namna hiyo (kulawiti), mwanamume unaitwa na wazee wakubwa wa ukoo, unashikishwa mbuzi kama ishara ya kuwapa na ikiwa umefanya hivyo unapaswa kufa mara tu mbuzi yule anapochinjwa.
"Hivyo, watu waliogopa kutenda, si kwa watoto tu, bali hata kwa wake zao japo wachache walikuwapo wenye tabia za kijinga kama hizi," anasema Zakaria Shirima (78), mkazi wa Kibosho Umbwe.
HATUA SERIKALINI
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Wily Machumu anakiri wamepata taarifa za matukio ya ukatili wa aina hiyo dhidi ya watoto kwenye baadhi ya shule binafsi na tayari wameanza uchunguzi wa kina ili kubaini ukweli wa jambo hilo kuchukua hatua stahiki za kisheria.
"Tumepata taarifa za kuwapo matukio ya kikatili hasa katika baadhi ya shule binafsi zilizopo mkoani hapa, tunafanya uchunguzi wa kina ili kubaini shule hizo na kuzichukulia hatua za kisheria.
"Pia tunaendelea kutoa elimu ya kina juu ya kutambua wajibu wao na kuwa walinzi wa watoto chini ya Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009. Serikali mkoani hapa hatutavumilia kuona mtu anafanya ukatili, viongozi wa dini watusaidie, jamii tubadilike," anahimiza Katibu Tawala.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu analaani ukatili huo dhidi ya watoto na kuwaomba wabunge wa mkoa huo kwenda bungeni kuwasilisha hoja ya kubadilisha sheria ya adhabu dhidi ya wanaofanya vitendo hivyo.
Anasema kuna tatizo la mmomonyoko mkubwa wa maadili, akifafanua kuwa watu wamegeuka kuwa wanyama, wakitenda mambo kama hawana akili.
"Tuna kesi kadhaa katika mkoa wetu, jitu zima lina akili, linakwenda kumchukua mtoto wa miaka 10, anakusaidia nini? Wanawake wapo wengi na wengine hawajaolewa, kwanini usiende kuoa na kukaa na mke wako?" Babu anahoji.
Anaongeza: "Mkoa wa Kilimanjaro umekithiri vitendo vya ukatili wa kijinsia, hali ni mbaya kwa sasa. Na zipo pia shule ambazo hutumia alama maalum za ushoga, nimeshawaita wamiliki wa shule hizo kujieleza."
Waziri wa Elimu, Sayansi na Tenolojia, Prof. Adolf Mkenda anasema wizara yake kwa kushirikiana na viongozi wa dini na wazazi, ina jukumu kubwa la kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto vinavyoendelea kwa kasi nchini.
"Tumekuwa tukisikia visa vingi vya unyanyasaji wa kijinsia, sijui ni kwa sababu sasa ni rahisi sana kupata taarifa au dunia imeharibika zaidi.
"Vyovyote vile, tuna jukumu la kuhakikisha tunazuia vitendo hivi. Tunajua watoto wamekuwa wakitumia muda mrefu shuleni na (shule) nyingine ni za kulala, hivyo bado wizara inaendelea kutafakari," anasema Prof. Mkenda na kusisitiza kuwa kila mmoja ana jukumu la kuhakikisha anakuza maadili ya watoto.
Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime katika mazungumzo na Nipashe kuhusu suala hilo, anasema wamejipanga kuwapa mafunzo askari na wakaguzi wao ili kuendana na wakati, akisisitiza utendaji wa uhalifu umebadilika kutokana na kukua kwa sayansi na teknolojia.
Anabainisha kuwa Desemba 31 mwaka jana, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini alitoa nafasi kwa askari na wakaguzi 29 kwenda India kwa ajili ya mafunzo ya unyanyasaji wa watoto katika mitandao na kushughulika na makosa ya kimtandao.
"Tutaendelea zaidi kuhakikisha askari na maofisa wetu wanapata elimu na weledi zaidi wa kuzuia uhalifu na kupeleleza kesi pale zinapotokea," Misime anasema.
VIONGOZI WA DINI
Katibu Mkuu wa Baraza la Waisilamu, Nuhu Mruma anasema wanaendelea kupingana na ukatili dhidi ya watoto na wanawake, wakitoa elimu kuhusu kufuatilia na kutoa taarifa za matukio yote ya ukatili.
Askofu wa Jimbo Katoliki la Moshi, Ludovick Minde anautaja utandawazi watu kukosa maadili na wazazi kujikita katika shughuli za kimaendeleo zaidi kuliko malezi ya familia, kuwa ni miongoni mwa vichochea vya matukio ya ukatili.
“Familia hazina muda wa kusali kwa pamoja. Sisi kama kanisa na Jimbo Katoliki Moshi tutaendelea kupinga ukatili wowote ule utakaofanywa na mtu yeyote yule," anasema Askofu Minde.
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Fredrick Shoo anaiambia Nipashe kuwa ukatili umekithiri nchini, akiwataka viongozi wote kusimama kutokomeza tatizo hilo.
"Wanadamu wote tuchukie ukatili, mwalimu ona uchungu kuharibu mtoto wa mwenzako, tuache kuiga mila za kigeni, vijana acheni kupenda fedha za haraka na kufanya matukio ya ushirikina, wazazi na walezi tuwatunze watoto," anahimiza Askofu Dk. Shoo.