Andikeni barua ya kugoma CAFPSG wanavaa jezi zilizoandikwa Visit Rwanda, je wanacheza mechi zao Rwanda? Hata akili kidogo tu ya kuchanganua mambo umekosa!?
Simba ni timu kubwa,CAF watawaogopa mkiwatishia kuwa hamchezi
Andikeni barua ya kugoma CAFPSG wanavaa jezi zilizoandikwa Visit Rwanda, je wanacheza mechi zao Rwanda? Hata akili kidogo tu ya kuchanganua mambo umekosa!?
Swali fikirishi je uwanja ukijaa maji tena mtafanyaje, pampu ya kuvuta maji uwanjani hakunaUONGOZI wa Simba baada ya kupata taarifa ya kubadilishwa ghafla kwa uwanja ambao utatumika kwa mechi yao ya nyumbani ya hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane, ulifanya kikao kizito Morocco kujadili jambo hilo.
.
Kikao hicho kilimalizika kwa azimio la kuandika barua nzito kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa lengo la kuona kama itaweza kulishawishi kurudisha mechi uwanja ambao ulipangwa ichezwe awali. Katika barua hiyo ambayo tayari imeshatua CAF, Simba imeandika ikihoji uamuzi wa shirikisho hilo kuhamisha mechi ya marudiano ya fainali kutoka Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam hadi New Amaan Complex, Zanzibar. Simba imetoa hoja tatu nzito za kuionyesha CAF kuwa uamuzi wa kubadili uwanja haukuwa sahihi.
.
Hoja ya kwanza ambayo Simba imeitumia katika barua yake ya kuonyesha mashaka kwa uamuzi wa CAF ni kukiukwa kwa kanuni ya 9(3) ya mashindano hayo juu ya utaratibu wa kufuatwa katika kufanya mabadiliko ya uwanja. Kanuni hiyo inafafanua hivi: “Eneo, tarehe na muda wa kuanza mchezo wa mechi za makundi, robo fainali, nusu fainali na fainali unapangwa na kamati ya mashindano ya klabu ya CAF baada ya kushauriana na shirikisho mwenyeji.
.
Simba imejiridhisha kuwa hakukuwa na mashauriano yoyote ambayo yalifanyika kabla ya uamuzi huo na badala yake kamati ya mashindano ya klabu ya CAF iliamua yenyewe kuipeleka mechi hiyo Zanzibar kwenye Uwanja wa New Amaan Complex bila kufanya mashauriano na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
.
“Tumejiridhisha kuwa uamuzi ulifanyika bila kufanyika mashauriano. Kwa vile kabla ya hapo hakukuwa na angalizo lolote kutoka CAF kuhusu uwanja na hata TFF yenyewe haikufanya mawasiliano na CAF juu ya suala la uwanja maana ni lazima pia yahusishe klabu mwenyeji na serikali,” amefichua mmoja wa vigogo wa Simba.
.
Hoja ya pili ambayo Simba imeiweka kwenye barua yake kwa CAF ni kwamba tayari ilishaanza mchakato wa kuuza tiketi za mchezo huo ambapo hadi sasa imeuza zaidi ya 20,000, namba ambayo ni kubwa zaidi ya idadi rasmi ya mashabiki wanaopaswa kuingia katika Uwanja wa New Amaan ambao unaingiza mashabiki 15,000 tu hivyo Simba inahoji ipi itakuwa hatima ya zaidi ya mashabiki 5,000 ambao tayari wameshakata tiketi zao na watashindwa kuwepo uwanjani kwa vile New Amaan Complex haitoshi kuingiza idadi hiyo ya mashabiki.
.
Hoja ya tatu ambayo Simba imeiweka mezani wasiwasi wa mazingira ya uamuzi huo kufanyika kwa upendeleo na mgongano wa kimaslahi, kinyume na ibara ya 2(3) ya katiba ya CAF inayolazimisha uadilifu na maadili kwa wanachama wa CAF na wanafamilia wa mpira wa miguu Afrika.
.
Simba imeambatanisha ushahidi wa taarifa ya RS Berkane kuwataarifu mashabiki wao kuwa mechi hiyo itachezwa Zanzibar kabla hata mabadiliko hayo ya uwanja hayajatangazwa jambo ambalo kiutaratibu halikuwa sahihi na ikiamini tayari timu hiyo ya Morocco ilishafahamu hilo mapema kutokana na kuwa na kigogo mmoja mzito ndani ya CAF.
.
Pamoja na hilo, Simba imeambatanisha ushahidi wa RS Berkane kuweka oda ya hoteli ambayo itafikia Zanzibar kabla hata barua ya CAF ya mabadiliko ya uwanja haijatolewa.
View attachment 3337846
Wenye akili ni wawili tuu...... kwahiyo Simba hajawahi kushinda nje ya nchi??Psychologically Simba kuogopa kucheza Amani complex na kupambania kucheza kwa Mkapa ni ishara kwamba hawawezi kupata matokeo nje ya kwa Mkapa.
Yani wachezaji mpaka viongizi saikolojia yao wameshai tune kwamba sehemu pekee wanayoweza pata matokeo ni kwa mkapa.
Hii ni mbaya sana kwa timu inayojielewa na inayojua nini inafanya.
Kwenye mpira kinachokupa matokeo ni uwezo wa kocha na mbinu zake,team work na quality ya mchezaji mmoja mmoja.
Ukiwaangalia Berkane unaona wamewaacha mbali sana Simba in all three aspects.
Hii kujifanya wanataka sana mechi ichezewe kwa Mkapa ni kujidanganya tu lakini uwezo wa Simba kwa Berkane ni duni sana.
Muhimu jengeni na ziwekeni sawa mentality za wachezaji wenu wawe wapambanaji kokote pale watakapocheza sio kutegemea home tu.
Nashauri Simba tsipeleke timu uwanjani iwapo huja zetu hazitajibiwa ipasavyo.UONGOZI wa Simba baada ya kupata taarifa ya kubadilishwa ghafla kwa uwanja ambao utatumika kwa mechi yao ya nyumbani ya hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane, ulifanya kikao kizito Morocco kujadili jambo hilo.
.
Kikao hicho kilimalizika kwa azimio la kuandika barua nzito kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa lengo la kuona kama itaweza kulishawishi kurudisha mechi uwanja ambao ulipangwa ichezwe awali. Katika barua hiyo ambayo tayari imeshatua CAF, Simba imeandika ikihoji uamuzi wa shirikisho hilo kuhamisha mechi ya marudiano ya fainali kutoka Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam hadi New Amaan Complex, Zanzibar. Simba imetoa hoja tatu nzito za kuionyesha CAF kuwa uamuzi wa kubadili uwanja haukuwa sahihi.
.
Hoja ya kwanza ambayo Simba imeitumia katika barua yake ya kuonyesha mashaka kwa uamuzi wa CAF ni kukiukwa kwa kanuni ya 9(3) ya mashindano hayo juu ya utaratibu wa kufuatwa katika kufanya mabadiliko ya uwanja. Kanuni hiyo inafafanua hivi: “Eneo, tarehe na muda wa kuanza mchezo wa mechi za makundi, robo fainali, nusu fainali na fainali unapangwa na kamati ya mashindano ya klabu ya CAF baada ya kushauriana na shirikisho mwenyeji.
.
Simba imejiridhisha kuwa hakukuwa na mashauriano yoyote ambayo yalifanyika kabla ya uamuzi huo na badala yake kamati ya mashindano ya klabu ya CAF iliamua yenyewe kuipeleka mechi hiyo Zanzibar kwenye Uwanja wa New Amaan Complex bila kufanya mashauriano na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
.
“Tumejiridhisha kuwa uamuzi ulifanyika bila kufanyika mashauriano. Kwa vile kabla ya hapo hakukuwa na angalizo lolote kutoka CAF kuhusu uwanja na hata TFF yenyewe haikufanya mawasiliano na CAF juu ya suala la uwanja maana ni lazima pia yahusishe klabu mwenyeji na serikali,” amefichua mmoja wa vigogo wa Simba.
.
Hoja ya pili ambayo Simba imeiweka kwenye barua yake kwa CAF ni kwamba tayari ilishaanza mchakato wa kuuza tiketi za mchezo huo ambapo hadi sasa imeuza zaidi ya 20,000, namba ambayo ni kubwa zaidi ya idadi rasmi ya mashabiki wanaopaswa kuingia katika Uwanja wa New Amaan ambao unaingiza mashabiki 15,000 tu hivyo Simba inahoji ipi itakuwa hatima ya zaidi ya mashabiki 5,000 ambao tayari wameshakata tiketi zao na watashindwa kuwepo uwanjani kwa vile New Amaan Complex haitoshi kuingiza idadi hiyo ya mashabiki.
.
Hoja ya tatu ambayo Simba imeiweka mezani wasiwasi wa mazingira ya uamuzi huo kufanyika kwa upendeleo na mgongano wa kimaslahi, kinyume na ibara ya 2(3) ya katiba ya CAF inayolazimisha uadilifu na maadili kwa wanachama wa CAF na wanafamilia wa mpira wa miguu Afrika.
.
Simba imeambatanisha ushahidi wa taarifa ya RS Berkane kuwataarifu mashabiki wao kuwa mechi hiyo itachezwa Zanzibar kabla hata mabadiliko hayo ya uwanja hayajatangazwa jambo ambalo kiutaratibu halikuwa sahihi na ikiamini tayari timu hiyo ya Morocco ilishafahamu hilo mapema kutokana na kuwa na kigogo mmoja mzito ndani ya CAF.
.
Pamoja na hilo, Simba imeambatanisha ushahidi wa RS Berkane kuweka oda ya hoteli ambayo itafikia Zanzibar kabla hata barua ya CAF ya mabadiliko ya uwanja haijatolewa.
View attachment 3337846
Lini uliona vist zanzibar kunako jezi ya mnyama?Kuna shida gani mechi ikichezwa Zanzibar? Simba wenyewe wameitangaza sana Zanzibar kwa zile jezi zao za 'Visit Zanzibar', ina maana walikuwa wanazivaa na kuitangaza kinafiki?
Mbona sasa hivi tumeshuhudia mambo mengi yakifanyika huko Kizimkazi, je hii ina maana kwamba Simba hawapo tayari kuiheshimisha KiziMkazi?
CAF wameamua kufanya hivyo ili kumheshimisha rais, Dr, mama Samia Suluhu Hassan na Watanzania, kwanini Simba wapinge, je wao si sehemu ya Watanzania?