Ndugu waungwana wana chit chat salaam..
Naleta hoja hii mbele yenu ili tujadili na kufikia hitimisho la hiki kinachoendelea kwani ni dhahiri kuwa kuna kila dalili za mchezo mchafu unaofanywa aidha kwa dhahiri ama kificho ili kumfanya
Lady doctor achukue taji hili kiupendeleo.
Awali ya yote ningependa kuwakumbusha japo kwa kifupi tu historia ya shindano hili hasa kwa wale wageni nalo.
Shindano hili lilikuwa likiendeshwa na ndugu Lundenga
Ruhazwe JR ambapo katika kipindi chote alikuwa
smart kwa kutojitanabaisha na mgombea yeyote.. Hii ilikuwa inajenga taswira ya kidemokrasia kwa wagombea na wapambe wake hivyo hata mgombea yeyote alipita kidemokrasia bila kuibua malalamiko...
TOFAUTI ILIYOPO SASA.
Katika shindano hili
muandaaji na mratibu mkuu wa shindano hili ndugu
Arushaone kwa uwazi kabisa pasi na kificho amejinatanabisha na mgombea mmoja ambae ni
Lady doctor hadi kufikia hatua ya kumpigia kampeni za waziwazi kuwa ndiye anayetaka atwae taji hilo.. Katika mazingira haya unajengeka wasiwasi mkubwa endapo wagombea wengine watatendewa haki hasa
shansarie ambaye ameonekana kuwa mwiba mkali kwa
Lady doctor tangu hatua za awali za fainali hizi. Ni dhahiri kuwa
Arushaone akiwa kama
mratibu mkuu na muandaaji wa shindano yuko radhi kuhujumu shindano hili ili ashinde
Lady doctor ambae ana maslahi nae binafsi kitu ambacho hakikubaliki KATIKA JAMII YETU YA KIDEMOKRASIA NA INAYOPENDA MABADILIKO YA KWELI.
WITO
Tulikatae jambo hili kwa kupinga kile anachofanya
Arushaone dhidi ya wagombea wengine. TUCHAGUE KUWA UPANDE WA DEMOKRASIA NA USHINDANI HURU NA WA HAKI.
NAWASILISHA.
Baba V
Mwenyekiti wa mahusiano na ndoa Chit chat ©2012.