Sir John Roberts
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 12,835
- 23,584
Kwanza niseme nakubali kabisa Rais anafanya kazi kwa ratiba alizopangiwa na wasaidizi wake. Siku 4 zilizopita Mh. Samia Suluhu Hassan katika ziara yake mkoani Katavi ameonekana katika msafara wake wa magari zaidi ya 100 akipita kwa kasi sana huku wananchi wakiwa wamejipanga barabarani kushangaa msafara wa Kiongozi wao.
Nimejiuliza maswali kadhaa kichwani kwangu huyu Rais tumemchagua sisi wananchi tuliosimama barabarani (ndio tumemchagua kwasababu wakati wa kupiga kura tulipiga kwa Marehemu magufuli na mgombea mwenza wake ambae ni huyu bibi samia).
Nimejiuliza anajisikiaje anapoona wananchi waliomchagua wapo barabarani yeye akipita kwa kasi bila kuwapa hata salamu huku akiwa na ulinzi wa kutisha kiasi cha kusema labda wananchi waliomchagua ndio tishio?
Jamani ieleweke sipingi ulinzi kwa Kiongozi wa nchi lakini nimeona tu kuwa waliomchagua wangepata faraja hata kupungiwa mkono tu na Kiongozi wao.
Kila la heri Rais samia Mungu akulinde afya njema na Hekma katika kuliongoza taifa letu.