Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 2,818
- 7,940
Wakuu,
Leo nimekuwa nikitafakari jambo moja ambalo limekuwa sehemu ya maisha yetu kila siku – simu za mkononi.
Ni ukweli kwamba simu imerahisisha mawasiliano, biashara, elimu na hata huduma za kijamii. Lakini kwa upande mwingine, kuna maswali makubwa:
Vijana wengi sasa wamelala na simu, kuamka ni simu, kula ni simu, hata kusoma ni simu.
Mitandao ya kijamii imewafanya vijana wengi kuwa “addicted”, yani uraibu wa – likes, comments na views zimekuwa kipimo cha furaha.
Kuna ongezeko la uzembe darasani, kupungua kwa muda wa kusoma vitabu na kufanya tafakari ya kweli.
Afya pia imeanza kuathirika: usingizi usio na mpangilio, matatizo ya macho, hata msongo wa mawazo (anxiety & depression) kutokana na comparison online.
Na tusisahau, simu pia zimekuwa chombo cha kupoteza maadili – ponografia (pilau), utapeli mitandaoni, ulevi wa betting.
Swali linabaki: Je, simu za mkononi ni chombo cha maendeleo au ndio “silaha tulizopewa bure” zinazomaliza kizazi kijacho kimya kimya?
👉 Wana Jamii, mnaonaje hili? Ni kweli simu zinaangamiza kizazi cha vijana au tatizo ni jinsi tunavyotumia teknolojia hii?
Nataka usikie maoni tofauti: wazazi, vijana, walimu, na hata wadau wa teknolojia.
🗣️ Hebu tujadiliane!