Hoja: Kuwa makini na magari yenye cc 1800 kushuka chini

Hoja: Kuwa makini na magari yenye cc 1800 kushuka chini

falcon mombasa

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2015
Posts
9,189
Reaction score
9,299
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza uchunguzi huru nilioufanya barabarani haswa katika jiji la dar es salaam nimebaini yafuatayo

Ajali nyingi zinazotokea dar asilimia kubwa zinahusisha magari madogo madogo.

Lakini baada ya kufanya uchunguzi zaidi nimebaini chanzo kikubwa cha ajali hizi zinasababishwa na wanaoenendesha magari yenye cc chini ya 1800

kundi hili la magari ya kuanzia cc 650 hadi cc 1800 asilimia 85 linahusha madereva wasio na uzoefu (learners) na wengi wao ndio magari yao ya kwanza.

Hivyo basi wawapo barabarani husababisha ajali nyingi kutokana na wao kuwa waoga waoga hali inayosababisha wao kupoteza kujiamini na hivyo kufanya vitu vya ajabu ambavyo matokeo yake husababisha ajali ndogo na kubwa za kupigana pasi na kadhalika. mimi niwapo barabarani huwa sikaikaribu na magari yenye cc ndogo maana najua asilimia kubwa bado hawana uzoefu hivyo muda wowote anaweza kufanya maamuzi yasiyokuwa yakawaida na kusababisha ajali.

Nawasilisha
 
Asante mkuu.. Wahusika watachukua tahadhari
 
Hizo cc650 mpaka 1800 wao magari yao ya mkopo na hawana uzoefu na Barabara je wewe lile BMW la mama lina cc ngapi na halijawahi sababisha ajali?
 
Vigari vingine vidooogo(Ingawa mimi sina hata gari lenye tairi moja)..watu humo wanakosa hata hewa nzuri na safi ya kutosha,na kama tunavyojua mwili ukikosa hewa safi na ya kutosha kwa muda fulani basi akili inaweza isifanye kazi vizuri.

716d1235228152-big-guys-little-cars-jim-fits-2.jpg
Big-man-little-car.jpg
daily_picdump_727_640_01.jpg
 
Kwahiyo unasubiria uulize gari yako aina gani ili ukamilishe uzi wako???

Mkuu, gari yako aina gani? Bughati, Ashton Martin, Bentley, Lamborghini, au Special Edition????
 
Nilivyosoma heading nikahisi something wrong na magari ya 1800cc,kwenye details umeongelea mambo mengine yaani wanao miliki haya magari ya kuanzia1800cc na kushuka chini ni ma leaner,
Mbona kama hivi vitu havihusiani? mkuu under pressure?
 
Maroli mangap yanapata ajari? Au nayo ya cc 650?
Unajua takwimu za magari yaliyopo wewe? Unatambua kwamba magari mengi yaliyo barabarani ni madogo Kwa ajili ya watu kubana bajeti ya mafuta? Huwezi ringanisha wingi Wa ajari za tax na trekta!
TRENI IPO MOJA RELINI NA INAPATA AJALI sembuse huko barabarani?
Wewe ni mjinga sana na huna hata toroli!
 
Mkuu naona unayopoint apo ila umefny zaid generalization kana kwamba kila ajali ya gari ndogo husababishwa na lena ama kila mwenye gar ndogo ni gar yke ya kwanza kumbka weng wanatumia gar ndogo saiv kuliko kubwa coz ya kusave mafuta vyuma vishakaza na watu wanamake bajet kivyao
 
Mi hata funuo ya gari siijui, niambieni kwanza CC ni nini na naiangalia wapi? Kunajamaa kaacha gari lake hapa niamgalie
 
Utafiti/uchunguzi wako unakosa details muhimu sana ili uwe valid kwa wasomaji.

1. Unajua idadi ya magari madogo (650cc -1800cc) kulingabiaha na magari makubwa barabarani?

2. Umetafuta ratio ya hayo magari makubwa vs madogo ili kujua kwa ulinganifu huo nani anatengeneza ajali nyingi?

3. Umeangalia hali ya uchumi, hujabaini kuwa magari madogo yanapendelewa zaidi yamakubwa kwa ajili ya kusave budget za familia?

Hence, hoja ya kuwa na gari dogo vs experience(learners) haipo valid.
 
Mkuu naona unayopoint apo ila umefny zaid generalization kana kwamba kila ajali ya gari ndogo husababishwa na lena ama kila mwenye gar ndogo ni gar yke ya kwanza kumbka weng wanatumia gar ndogo saiv kuliko kubwa coz ya kusave mafuta vyuma vishakaza na watu wanamake bajet kivyao
naam mkuu
 
Acha kutibua watu, wana frustrations zao bhana. Wengi wanaendesha vibaby walker afu wewe useme ni learners? Angalia comments zao ndiyo utajua jinsi ulivyowakorofisha...
 
Back
Top Bottom