Hoja: Kuwa makini na magari yenye cc 1800 kushuka chini

Nilivyosoma heading nikahisi something wrong na magari ya 1800cc,kwenye details umeongelea mambo mengine yaani wanao miliki haya magari ya kuanzia1800cc na kushuka chini ni ma leaner,
Mbona kama hivi vitu havihusiani? mkuu under pressure?
Uandishi kama wa magazeti ya Ijumaa na uwazi vile?? heading na content havifanani kabisa
 
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza uchunguzi huru nilioufanya barabarani haswa katika jiji la dar es salaam nimebaini yafuatayo

Ajali nyingi zinazotokea dar asilimia kubwa zinahusisha magari madogo madogo.

Lakini baada ya kufanya uchunguzi zaidi nimebaini chanzo kikubwa cha ajali hizi zinasababishwa na wanaoenendesha magari yenye cc chini ya 1800

kundi hili la magari ya kuanzia cc 650 hadi cc 1800 asilimia 85 linahusha madereva wasio na uzoefu (learners) na wengi wao ndio magari yao ya kwanza.

Hivyo basi wawapo barabarani husababisha ajali nyingi kutokana na wao kuwa waoga waoga hali inayosababisha wao kupoteza kujiamini na hivyo kufanya vitu vya ajabu ambavyo matokeo yake husababisha ajali ndogo na kubwa za kupigana pasi na kadhalika. mimi niwapo barabarani huwa sikaikaribu na magari yenye cc ndogo maana najua asilimia kubwa bado hawana uzoefu hivyo muda wowote anaweza kufanya maamuzi yasiyokuwa yakawaida na kusababisha ajali.

Nawasilisha
Sometimes naikubali JF hata bila kupenda.
Nimekusoma ingawa sijakuelewa kabisa mkuu
 
Mmmmh
Ili uwe na gari ya cc kubwa maana yake usiwe na hela za mawazo
 
Siyo kweli, your theory is as pure as a fallacy to be ignored!
 
Acha kutibua watu, wana frustrations zao bhana. Wengi wanaendesha vibaby walker afu wewe useme ni learners? Angalia comments zao ndiyo utajua jinsi ulivyowakorofisha...
hahahahaha mkuu hii koment ya kufunga mwaka
 
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza uchunguzi huru nilioufanya barabarani haswa katika jiji la dar es salaam nimebaini yafuatayo

Ajali nyingi zinazotokea dar asilimia kubwa zinahusisha magari madogo madogo.

Lakini baada ya kufanya uchunguzi zaidi nimebaini chanzo kikubwa cha ajali hizi zinasababishwa na wanaoenendesha magari yenye cc chini ya 1800

kundi hili la magari ya kuanzia cc 650 hadi cc 1800 asilimia 85 linahusha madereva wasio na uzoefu (learners) na wengi wao ndio magari yao ya kwanza.

Hivyo basi wawapo barabarani husababisha ajali nyingi kutokana na wao kuwa waoga waoga hali inayosababisha wao kupoteza kujiamini na hivyo kufanya vitu vya ajabu ambavyo matokeo yake husababisha ajali ndogo na kubwa za kupigana pasi na kadhalika. mimi niwapo barabarani huwa sikaikaribu na magari yenye cc ndogo maana najua asilimia kubwa bado hawana uzoefu hivyo muda wowote anaweza kufanya maamuzi yasiyokuwa yakawaida na kusababisha ajali.

Nawasilisha
MKUU AMA UNABARABARA ZAKO MAANA ALMOST 90% NI HAYO YA CC NDOGO DSM.. sasa sijui huwa unazikwepa vipi
 
Kwa hiyo tatizo ni magari au mafereva,?
Basi Kama no kweli upeleke utafiti wako kwa makampuni ya kutengrneza magari Kama ni wa uhakika watajua Cha kufanya
 
Back
Top Bottom