Hoja: Mapambano kati ya kizazi cha zamani cha wanasiasa na kizazi kipya

Hoja: Mapambano kati ya kizazi cha zamani cha wanasiasa na kizazi kipya

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,818
Reaction score
7,940
Wana JF,
Kuna jambo linanitesa kichwani siku hizi: mapambano yasiyo rasmi kati ya kizazi cha zamani cha wanasiasa na kizazi kipya.

Tukiri ukweli:

  • Kizazi cha zamani cha wanasiasa (waliobeba urithi wa siasa za chama kimoja, mapinduzi, na siasa za ujamaa) kimejikita kwenye mfumo wa heshima, nidhamu, "kusema ndiyo" na kushika mila za chama. Hawa wameishi kwenye siasa ambazo ni career ya maisha – mtu anaingia akiwa kijana, anatoka akiwa mzee.
  • Kizazi kipya kinaingia na kasi, kimekulia kwenye dunia ya “social media politics”, kina access ya taarifa kwa sekunde, na kinaamini katika uwazi, “speed” na accountability ya papo kwa papo. Hawa hawaoni tabu kum-challenge kiongozi hadharani bila woga.

Sasa vita iko hapa:

  • Wazee wanaona vijana ni wasio na adabu, hawana uvumilivu na hawajui historia.
  • Vijana wanawaona wazee ni “blocking stone”, hawataki kuachia madaraka na bado wanatumia mbinu za enzi za “Cold War politics”.

Tunaona wazi tafsiri ya haya mapambano kwenye:

  • Uchaguzi: vijana wanataka transparency na digital campaigns, wazee bado wanaamini nguvu ya misafara, ngoma na maneno ya jukwaani.
  • Bunge: vijana wachache wanaojaribu kuongea mambo ya “kisasa” mara nyingi wanakemewa na kuambiwa “wanakiherehere”.
  • Mitazamo ya maendeleo: wazee wanapenda miradi mikubwa ya hadhi, vijana wanataka miradi midogo-midogo yenye impact ya haraka kwa wananchi.
  • Teknolojia: vijana wanataka digital economy, wazee bado wanapambana na files na makabrasha.

Swali langu ni hili:
👉 Je, kizazi cha zamani kiko tayari kukabidhi kijiti kwa kizazi kipya, au kitapigana hadi tone la mwisho la damu cha kisiasa?
👉 Na je, vijana wa siasa wa sasa wako tayari kwa mzigo wa kuongoza, au bado wapo “online warriors (keyboard warriors)” zaidi kuliko “real leaders”?

Wakuu, hii vita ya vizazi inatupeleka wapi kisiasa kama Taifa?
 
Kihongosi ni kijana mwanasiasa wa juu wa chama kinachotawala tumuulize changamoto anazokutana nazo pale wanapopanga mambo ya chama chao na mzee mkongwe Wasira. Je wazee walioko chamani huwa wanakubali mawazo ya vijana wao chamani au wanaburuzana tu?
 
Sidhani kunatofauti ya aina yoyote, tofauti niliyoiona hapa siasa za zamani zilienda talatibu kama vile Nyerere alivyo hitaji, tofauti na sasa hayupo kila mwanasiansa ni baba wa Taifa.
 
Back
Top Bottom