Mchambuzi
JF-Expert Member
- Aug 24, 2007
- 4,850
- 9,434
Sio sahihi kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuja kabla ya uwepo kwa ukamilifu – kwa Katiba za mataifa mawili yanayounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – yani Jamhuri ya Watu Wa Zanzibar na Jamhuri ya Watu Wa Tanganyika (Tanzania Bara).
Kwa vile ndugu zetu wazanzibari ni waelewa zaidi juu ya unuhimu wa national identity and national sovereignity katika masuala ya mahusiano na pia mashirikiano ya kimataifa, miaka karibia 30 iliyopita (1984), ikiwa ni miaka saba tu baada ya katiba ya JMT (1977) kuzaliwa, walifanya juu chini na kushinikiza kuzaliwa kwa Katiba yao kamili bila ya kujalisha uwepo wa katiba ya JMT(1977), ambayo miongoni mwa mengineyo, walifutilia mbali jina batili walilopewa chini Katiba ya 1977 kwani katiba hii ilifuta jina halisi la "Zanzibar" na kuweka jina batili la "Tanzania Visiwani", huku Tanganyika ikibadilika na kuwa Tanzania Bara, jina ambalo kutokana na ukosefu wa umakini kwa upande wa watanganyika, wamebakia kutambulika kwa utambulisho batili wa "Watanzania Bara"; Wazanzibari walienda mbali na werevu wao ambapo mwaka 2010 na waliamua kuboresha katiba ya zanzibar (1984) ili kuweka bayana nia ya taifa la Zanzibar, kwanza ‘to maintain her sovereignty and national identity' kabla ya masuala mengine yoyote, likiwepo suala juu ya Muungano wake na Tanganyika (Tanzania Bara);
Kwa upande mwingine, Katiba ya sasa ya Tanzania (1977) imeendelea kuwa ndio Katiba kwa masuala ya Tanganyika huku pia ikiwa ni Katiba kwa masuala ya Muungano, suala ambalo linazidi kuleta utata juu ya muungano uliopo; Kuendelea kukosekana kwa ‘decleration of national sovereignty and national identity' kwa Tanganyika kwa mujibu wa Katiba ya Tanganyika (Tanzania Bara), huku upande mwingine wa muungano (Zanzibar) ukiwa tayari umefanya hivyo, ni utata unaohitaji ufumbuzi wa haraka;
Bila ya kujalisha iwapo muungano baina ya Zanzibar na Tanganyika (Tanzania Bara) utakuwa ni muungano wa mkataba au wa aina yoyote ile, kuna umuhimu kwa upande wa Tanganyika (Tanzania bara) kwanza kuja na Katiba yake iliyokamilika na inayoelezea bayana masuala ya national sovereignty na national identity kama ilivyofanya Zanzibar; Ndani ya katiba hizi ndio lizungumzwe suala juu ya jinsi gani pande zote mbili zinataka kushirikiana na mataifa mengine, ikiwa ni pamoja na nchi shirikishi za muungano – yani Tanganyika (Tanzania Bara) na Zanzibar, kama mataifa huru.
Kwa maana nyingine, Muungano wa Tanganyika (Tanzania bara) na Zanzibar) utokane na matakwa ya wananchi wa pande zote mbili, kwa mujibu ya yaliyomo ndani ya Katiba za pande hizi mbili – yani Katiba ya Tanganyika (Tanzania Bara) na Katiba ya Zanzibar; Nje ya hapo, kitendo cha tume ya Jaji Warioba kuja na Katiba ya Muungano bila ya uwepo wa Katiba za pande zote mbili yani – Katiba ya Tanganyika (Tanzania bara) na Katiba ya Zanzibar itakuwa ni kupoteza muda na fedha za walipa kodi, lakini mbaya zaidi, itaimarisha tatizo lililopo badala ya kulitafutia ufumbuzi wenye manufaa kwa nchi shirikishi za muungano;