Mkuu
Mchambuzi
Kwangu mimi naona title yako inatakiwa kusomeka kinyume na ulivyoiweka.
Kumbuka katiba ya sasa ya JMT haitambui uwepo wa Tanganyika, inatambua serikali mbili tu ile ya Zanzibar na ile ya JMT. Kuanzisha serikali nyingine nje ya hizo mbili ni swala la kikatiba si nje ya hapo. Kwa ufupi haiwezekani kabisa kuanzisha mchakato wa kufufua serikali ya Tanganyika bila mabadiliko ya katiba ya JMT, kinyume cha hapo the whole process would be unconstitutional/illegal.
Nadhani proposal ya tume ya Warioba ndiyo sahihi kisheria maana kwa sasa ni lazima kwanza Serikali ya Tanganyika itambuliwe kikatiba ndiyo mchakato wa kuunda institutions zake ufuate. Hili ni la muhimu zaidi leo maana hata ukitaka kuzungumzia kuuvunja muungano through legal process unafanyaje kwa katiba ya sasa? Hizo negotiations serikali ya znz itaketi na nani maana hakuna serikali ya Tanganyika kwa sasa? Swali hili pia unaweza kujiuliza ikiwa kutahitajika majadiliano ya kuunda serikali moja, what would be the parties?
Mkuu, karibu katika mjadala; I come from a background kwamba katiba ya 1977 haikuwa katiba halali kwa maana ya kwamba ilitakiwa iendane na yaliyokuweoo kwenye mkataba wa muungano, 1964 ambapo among other things, lengo lilikuwa ni serikali tatu, sio mbili wala moja; ni kutokana na mgogoro huu ndio maana tumekuwa na mvutano mkubwa juu ya autonomy ya zanzibar kutokana na ubovu wa katiba ya 1977 lakini pia kwa sisi wachache, tumekuwa tunaungana na wanaharakati kama mtikila kudai tanganyika yetu;
Hoja yako inajadili kama vile katiba ya 1977 is divine wakati hiyo ndio kiini cha mgogoro wa muungano wetu, na tume ya warioba ilikuwa na nafasi ya kurekebisha napungufu yaliyopo kwa kurudi nyuma zaidi na kuangalia wapi tulikosea kisha kutengeneza terms of reference za ku engage na wananchi, sio kufukia mapungufu ya awali kama vile they don't matter any more;
A constitutional government haina maana kwamba the government follows the letter of the constitution and the law; pre requisite ya constitutional government ni kwamba the laws themselves lazima ziwe just, fair, equitable, hivyo ndivyo katiba inapata uhalali;kutokana na ukosefu wa uhalali huu, haikuchukua muda mrefu kwa zanzibar kuja na katiba yake (1979), ambayo ikaboreshwa zaidi 1984 kwani katiba ya 1977 among other things ilitamka kwamba muungano ni baina ya Tanzania bara na Tanzania Zanzibar (sio Tanganyika na Zanzibar!!!); 2010 walifanya mabadiliko zaidi kwa nia ya kujenga zaidi her autonomy, sovereignty and identity lakini kwa bahati mbaya wasio waelewa juu ya sheria ya mkataba wa kimataifa, madai ya wazanzibari wanayaona kama hayana mantiki na ni wakorofi; Je, kwa Tanganyika (ukipenda Tanzania bara), haya yapo wapi i.e autonomy, identity, sovereignty?kumbuka, ni ukorofi wa mandela, ghandi ndio ulioleta uhuru wa kweli na pia ni wakorofi kama lissu, mtikila na wengine ndio watawaletea watanzania uhuru wa kweli;
Kumbuka, katiba ya muda ya muungano (1965)ilikuwa ni katiba ya Tanganyika iliyofanyiwa marekebisho kidogo kwa ahadi kwamba mchakato wa sasa chini ya warioba ungefuata ndani ya mwaka mmoja; badala yake, tukaingia katika kiza cha katiba ya muda kwa miaka 12 (1965 to 1977), na baada ya kiza hiki, katiba mpya ikavuruga kabisa malengo yote ya muungano; ilitarajiwa kwamba baada ya miaka 50 ya kutotimiza ahadi ya uteuzi wa tume ya katiba itakayosimamia mchakato wa katiba ya znz, na muungano huku tanganyika ikiendelea na katiba yake, tume ya warioba leo pamoja umuhimu wake bila ya uangalifu itaturudisha nyuma badala ya kusonga mbele; kwanini tusubiri maoni ya wananchi juu ya mfumo wa muungano kisha tutunge katiba mpya ya tanganyika? Ina maana tanganyika inahitaji katiba yake only on certain conditions? Kwanini mshirika mwingine wa muungano (zanzibar) yeye hakusubiri maamuzi juu ya mfumo wa muungano kujipatia katiba yake? Ni katika muktadha huu nimemuuliza mzee mwanakijiji swali kwamba je - in the context of the union btn TG na ZNZ, suala la autonomy ni relative or absolute? Ningependa kusikia maoni yako katika hili;
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums