Hoja Mbadala: Katiba Ya Muungano Kuja Kabla ya Katiba ya Tanganyika (Tanzania Bara) ni Makosa!

Hoja Mbadala: Katiba Ya Muungano Kuja Kabla ya Katiba ya Tanganyika (Tanzania Bara) ni Makosa!

Mchambuzi; Hoja yako ni maridhawa.

Hata hivyo, binafsi naamini kuwa bila kuzungumzia uwepo wa Muungano yote yanayofanyika bado yataleta matatizo mbeleni. Kitu cha kwanza kabla hatujaamua kuandika Katiba ya Muungano au ya Tanganyika for that matter wananchi wa Zanzibar walitakiwa wapige kura ya maoni kama wanataka kutoka kwenye Muungano au la. Uamuzi wa Wazanzibari ungeamua kama tunakuwa na serikali ya Tanganyika au vipi na kama tunaendelea na Muungano unakuwa vipi. Sasa hivi, Wazanzibari hata tukirudisha Tanganyika bado wataona wanaonewa.

Kabla ya kuamua kuhusu Katiba ya Muungano au ya Tanganyika ni lazima wananchi wa Zanzibar wangeamua kwanza kama wanataka Muungano. Kama wakitaka kutoka kwenye Muungano basi la kwanza ambalo linafanyika ni wao wanaweka tarehe ya siku ya kufungasha virago vyao halafu huku Tanganyika tunaamua tunataka kufanya nini. Kwa sababu hapo hakutakuwa na masuala ya Katiba ya Muungano.

Kitu gani kinachokufanya uwatwishe wazanzibari mzigo mzima wa kuuvunja Muungano?
 
Tafsiri ya nyuma ya pazia tume ya jaji Warioba imetoa fursa ya (Referendum) badala ya kupiga kura wananchi watoe maaoni kukubaliana na rasimu ya katiba ambyo imetoa mchanganyua wa mambo kwenye mfumo wa serikali taut na mambo yahusuyo muungano.baada ya maoni wakikubali serikali tatu hapo ndipo [rasimu hii itagawanywa kubaki na mambo ya muungano tu na yale yaliyobaki kuundiwa katiba ya Tanganyika kabla hazijapitishwa kuwa katiba
 
Mkuu Mchambuzi

Kwangu mimi naona title yako inatakiwa kusomeka kinyume na ulivyoiweka.

Kumbuka katiba ya sasa ya JMT haitambui uwepo wa Tanganyika, inatambua serikali mbili tu ile ya Zanzibar na ile ya JMT. Kuanzisha serikali nyingine nje ya hizo mbili ni swala la kikatiba si nje ya hapo. Kwa ufupi haiwezekani kabisa kuanzisha mchakato wa kufufua serikali ya Tanganyika bila mabadiliko ya katiba ya JMT, kinyume cha hapo the whole process would be unconstitutional/illegal.

Nadhani proposal ya tume ya Warioba ndiyo sahihi kisheria maana kwa sasa ni lazima kwanza Serikali ya Tanganyika itambuliwe kikatiba ndiyo mchakato wa kuunda institutions zake ufuate. Hili ni la muhimu zaidi leo maana hata ukitaka kuzungumzia kuuvunja muungano through legal process unafanyaje kwa katiba ya sasa? Hizo negotiations serikali ya znz itaketi na nani maana hakuna serikali ya Tanganyika kwa sasa? Swali hili pia unaweza kujiuliza ikiwa kutahitajika majadiliano ya kuunda serikali moja, what would be the parties?
 
Last edited by a moderator:
Mara kwa mara anapokuwa anaongea Warioba anapata kigugumizi kutamka Tanganyika ilhali akitamka Zanzibar bila shida. Utamsikia akisema Zanzibar na kisha Tanzania Bara? Kwa nini hasemi Tanzania Visiwani anapokuwa anazungumzia Zanzibar? There is a really problem kwenye huu muungano. Ni nchi zipi ziliungana? Pasipo kuzifahamu itakuwa vigumu kujadili muungano. Warioba wewe ni mwanasheria. Please tell us! Mchanganyiko huu umesababisha watu na akili zao kusherehekea uhuru wa Tanzania Bara 9/12 nchi ambayo haipo. Hiyo ni tarehe ambayo Tanganyika ilipata uhuru. Anything Tanzania ni kuanzia 26/4//64. Tusidanganyane na kupotosha historia kwa vizazi vijavyo.


Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums

Miaka ya mwanzo ya 1980s, mwanazuoni mmoja aitwaye Profesa Srivastava alijadili mapungufu ya katiba ya JMT (1977) hasa akilenga kuonyesha kwamba mfumo wa awali uliokusudiwa chini ya makubaliano ya muungano 1964 ulikuwa ni wa serikali tatu, sio mbili as stipulated kwenye katiba ya 1977; Mwanasheria Mkuu wakati huo alikuwa ni mwenyekiti wa sasa wa tume ya mabadiliko ya katiba - Jaji Warioba, na alinukuliwa na gazeti la serikali la daily news la tarehe 16 Machi 1982 akisema yafuatayo:

"Nina wasiwasi kuwa Profesa alikuwa akiitizama Katiba ya 177 katika mtizamo wa ki-shirikiano ambapo tungeweza kuwa na serikali tatu tofauti. Nina uhakika waliotunga Katiba ya 1977 hawakuwa na mawazo hayo vichwani mwao."


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Tafsiri ya nyuma ya pazia tume ya jaji Warioba imetoa fursa ya (Referendum) badala ya kupiga kura wananchi watoe maaoni kukubaliana na rasimu ya katiba ambyo imetoa mchanganyua wa mambo kwenye mfumo wa serikali taut na mambo yahusuyo muungano.baada ya maoni wakikubali serikali tatu hapo ndipo [rasimu hii itagawanywa kubaki na mambo ya muungano tu na yale yaliyobaki kuundiwa katiba ya Tanganyika kabla hazijapitishwa kuwa katiba
Wananchi wakatae, wasikatae, serikali ya tatu imekuwepo tangia muungano uzaliwe lakini haionekani kwa wazi kutokana na kiini macho kilichopo ambapo rais wa muungano ni huyo huyo anayesimamia masuala ya Tanganyika ambayo hayapo kwenye muungano;Ni yeye anayeunda baraza la mawaziri lenye kusimamia masuala yasiyokuwa ya muungano (kwa mfano Afya, Maji) yani ya Tanganyika, lakini pia ni yeye anayeteua mawaziri wa kusimamia masuala ya muungano (kama vile mambo ya nje, ndani n.k), huku rais wa zanzibar yeye akiteua mawaziri wa kusimamia masuala ya zanzibar yasiyokuwa ya muungano (uvuvi, uchukuzi, n.k); kama unanifuatilia vizuri, ina maana kuna three heads of goverments, moja chini ya rais wa zanzibar, na nyingine rais wa muungano huyo huyo pia akiwa ndiye rais wa tanganyika (masuala yasiyokuwa ya muungano).

Ni kwa mantiki hii, wale wasiokuwa na uelewa wa kiini macho hiki wanakuwa wepesi kushawishika eti serikali tatu itakuwa ni mzigo wakati wizara zilizo nyingi kwa miaka karibia 40 ni zile zinazohusika na masuala ya bara tu (tanganyika), huku chache zikiwa zile zinazoshughulika na masuala ya zanzibar tu, na chache zaidi masuala ya muungano; nadhani hadi hapa unaelewa kiini macho kilichopo, unaelewa kwamba tuna serikali tatu in practice tangia 1964(ingawa in theory hatuoni) na pia kwamba hoja juu ya gharama za kuendesha serikali tatu ni kubwa ni hoja mufilisi.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mkuu Mchambuzi

Kwangu mimi naona title yako inatakiwa kusomeka kinyume na ulivyoiweka.

Kumbuka katiba ya sasa ya JMT haitambui uwepo wa Tanganyika, inatambua serikali mbili tu ile ya Zanzibar na ile ya JMT. Kuanzisha serikali nyingine nje ya hizo mbili ni swala la kikatiba si nje ya hapo. Kwa ufupi haiwezekani kabisa kuanzisha mchakato wa kufufua serikali ya Tanganyika bila mabadiliko ya katiba ya JMT, kinyume cha hapo the whole process would be unconstitutional/illegal.

Nadhani proposal ya tume ya Warioba ndiyo sahihi kisheria maana kwa sasa ni lazima kwanza Serikali ya Tanganyika itambuliwe kikatiba ndiyo mchakato wa kuunda institutions zake ufuate. Hili ni la muhimu zaidi leo maana hata ukitaka kuzungumzia kuuvunja muungano through legal process unafanyaje kwa katiba ya sasa? Hizo negotiations serikali ya znz itaketi na nani maana hakuna serikali ya Tanganyika kwa sasa? Swali hili pia unaweza kujiuliza ikiwa kutahitajika majadiliano ya kuunda serikali moja, what would be the parties?


Mkuu, karibu katika mjadala; I come from a background kwamba katiba ya 1977 haikuwa katiba halali kwa maana ya kwamba ilitakiwa iendane na yaliyokuweoo kwenye mkataba wa muungano, 1964 ambapo among other things, lengo lilikuwa ni serikali tatu, sio mbili wala moja; ni kutokana na mgogoro huu ndio maana tumekuwa na mvutano mkubwa juu ya autonomy ya zanzibar kutokana na ubovu wa katiba ya 1977 lakini pia kwa sisi wachache, tumekuwa tunaungana na wanaharakati kama mtikila kudai tanganyika yetu;

Hoja yako inajadili kama vile katiba ya 1977 is divine wakati hiyo ndio kiini cha mgogoro wa muungano wetu, na tume ya warioba ilikuwa na nafasi ya kurekebisha napungufu yaliyopo kwa kurudi nyuma zaidi na kuangalia wapi tulikosea kisha kutengeneza terms of reference za ku engage na wananchi, sio kufukia mapungufu ya awali kama vile they don't matter any more;

A constitutional government haina maana kwamba the government follows the letter of the constitution and the law; pre requisite ya constitutional government ni kwamba the laws themselves lazima ziwe just, fair, equitable, hivyo ndivyo katiba inapata uhalali;kutokana na ukosefu wa uhalali huu, haikuchukua muda mrefu kwa zanzibar kuja na katiba yake (1979), ambayo ikaboreshwa zaidi 1984 kwani katiba ya 1977 among other things ilitamka kwamba muungano ni baina ya Tanzania bara na Tanzania Zanzibar (sio Tanganyika na Zanzibar!!!); 2010 walifanya mabadiliko zaidi kwa nia ya kujenga zaidi her autonomy, sovereignty and identity lakini kwa bahati mbaya wasio waelewa juu ya sheria ya mkataba wa kimataifa, madai ya wazanzibari wanayaona kama hayana mantiki na ni wakorofi; Je, kwa Tanganyika (ukipenda Tanzania bara), haya yapo wapi i.e autonomy, identity, sovereignty?kumbuka, ni ukorofi wa mandela, ghandi ndio ulioleta uhuru wa kweli na pia ni wakorofi kama lissu, mtikila na wengine ndio watawaletea watanzania uhuru wa kweli;

Kumbuka, katiba ya muda ya muungano (1965)ilikuwa ni katiba ya Tanganyika iliyofanyiwa marekebisho kidogo kwa ahadi kwamba mchakato wa sasa chini ya warioba ungefuata ndani ya mwaka mmoja; badala yake, tukaingia katika kiza cha katiba ya muda kwa miaka 12 (1965 to 1977), na baada ya kiza hiki, katiba mpya ikavuruga kabisa malengo yote ya muungano; ilitarajiwa kwamba baada ya miaka 50 ya kutotimiza ahadi ya uteuzi wa tume ya katiba itakayosimamia mchakato wa katiba ya znz, na muungano huku tanganyika ikiendelea na katiba yake, tume ya warioba leo pamoja umuhimu wake bila ya uangalifu itaturudisha nyuma badala ya kusonga mbele; kwanini tusubiri maoni ya wananchi juu ya mfumo wa muungano kisha tutunge katiba mpya ya tanganyika? Ina maana tanganyika inahitaji katiba yake only on certain conditions? Kwanini mshirika mwingine wa muungano (zanzibar) yeye hakusubiri maamuzi juu ya mfumo wa muungano kujipatia katiba yake? Ni katika muktadha huu nimemuuliza mzee mwanakijiji swali kwamba je - in the context of the union btn TG na ZNZ, suala la autonomy ni relative or absolute? Ningependa kusikia maoni yako katika hili;


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
M nahisi kati ya kuta za nje na ndan unapojenga nyumba huwa ni muhimu kwanza kuta za nje ili ziweze kubeba paa la nyumba. katiba ya Muungano then Nchi washirika.
 
M nahisi kati ya kuta za nje na ndan unapojenga nyumba huwa ni muhimu kwanza kuta za nje ili ziweze kubeba paa la nyumba. katiba ya Muungano then Nchi washirika.

kwanini haujazungumzia msingi wa hiyo nyumba?si ajabu nyumba ikaporomoka;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Suala la serikali tatu, yaani ya Zanzibar, Tanganyika na Tanzania haliwezekani. Nafikiri hata Warioba ameanza kutetereka baada ya kupitiwa na kimbunga kikali kutoka upande wa CCM. Kwa kuwa sera ya CCM ni serikali mbili, nyinyi hata mngefanyaje lazima mkubaliane na sera za chama tawala ya kubaki na serikali mbili tu.!
 
Kitu cha kwanza kabla hatujaamua kuandika Katiba ya Muungano au ya Tanganyika for that matter wananchi wa Zanzibar walitakiwa wapige kura ya maoni kama wanataka kutoka kwenye Muungano au la.
Kwanini hiyo Kura ya maoni iwe kwa Wazanzibari peke yao? Jambo la kura ya maoni linatakiwa liwe bilateral and neutral to all segments ili kuwa decent
 
Mchambuzi; hoja yako ni maridhawa. Hata hivyo, binafsi naamini kuwa bila kuzungumzia uwepo wa Muungano yote yanayofanyika bado yataleta matatizo mbeleni. Kitu cha kwanza kabla hatujaamua kuandika Katiba ya Muungano au ya Tanganyika for that matter wananchi wa Zanzibar walitakiwa wapige kura ya maoni kama wanataka kutoka kwenye Muungano au la. Uamuzi wa Wazanzibari ungeamua kama tunakuwa na serikali ya Tanganyika au vipi na kama tunaendelea na Muungano unakuwa vipi. Sasa hivi, Wazanzibari hata tukirudisha Tanganyika bado wataona wanaonewa. Kabla ya kuamua kuhusu Katiba ya Muungano au ya Tanganyika ni lazima wananchi wa Zanzibar wangeamua kwanza kama wanataka Muungano. Kama wakitaka kutoka kwenye Muungano basi la kwanza ambalo linafanyika ni wao wanaweka tarehe ya siku ya kufungasha virago vyao halafu huku Tanganyika tunaamua tunataka kufanya nini. Kwa sababu hapo hakutakuwa na masuala ya Katiba ya Muungano.
Mimi huwa ninapata mashaka kwenye kauli hii ambayo nimeshaisikia sana, zaidi ikitoka kwetu Watanganyika. [Kwa makusudi najizuwia kutumia jina la Watanzania Bara ambalo tumepachikwa na tunakwenda nalo bila ya kujua kama tunalikubali au la].

Kwa nini tuwaulize Wazanzibari tu kama wanataka au hawataki Muungano? Watanganyika je, na wao hawakupaswa kuulizwa kama wanautaka Muungano au hawautaki?

Nikirudi kwa mada ya Mchambuzi, ninakubaliana naye sana tu kuwa ili kuepuka migogoro ya kisheria huko tuendako, iko haja ya kwanza kufanya hilo ulilopendekeza Mh. MWANAKIjiji la kuwauliza Wazanzibari na Watanganyika, kama wanataka Muungano uwepo na wa aina gani. Ikiwa mmoja atakataa, hakutakuwa na haja ya kuendelea na haya yananayofanyika sasa. Kama wakikubali wote, kwanza kila "mshirika" mmoja atunge katiba yake, baadaye waziwasilishe mezani kuunda katiba ya Muungano, tena kwa mambo ya Muungano tu.
 
Last edited by a moderator:
Mchambuzi,

Nakubaliana na hoja yako ya kupatikana kwanza kwa katiba ya Tanganyika ndio tukajuwa namna gani katiba ya muungano ije. kwa watawala hilo sifikirii kama watalikubali kama ilivyo kawaida ya nchi hii kuendeshwa kwa kuhakikisha wananchi wanapewa cosmetic platform ya kutoa maoni kwa sababu maoni halisi ya wananchi huenda kinyume na watawala na azma zao.

Ndio sababu wanazungumzia katiba kuu wakati ya Tanganyika haijaundwa. Idealy referendum ingeliweka wazi legitimacy ya mfumo ujao na kama kuna endorsement ya wananchi isio na shaka juu kuwepo kwa muungano, namna ya mfumo na mengi ya msingi.
 
Mchambuzi; Hoja yako ni maridhawa.

Hata hivyo, binafsi naamini kuwa bila kuzungumzia uwepo wa Muungano yote yanayofanyika bado yataleta matatizo mbeleni. Kitu cha kwanza kabla hatujaamua kuandika Katiba ya Muungano au ya Tanganyika for that matter wananchi wa Zanzibar walitakiwa wapige kura ya maoni kama wanataka kutoka kwenye Muungano au la. Uamuzi wa Wazanzibari ungeamua kama tunakuwa na serikali ya Tanganyika au vipi na kama tunaendelea na Muungano unakuwa vipi. Sasa hivi, Wazanzibari hata tukirudisha Tanganyika bado wataona wanaonewa.

Kabla ya kuamua kuhusu Katiba ya Muungano au ya Tanganyika ni lazima wananchi wa Zanzibar wangeamua kwanza kama wanataka Muungano. Kama wakitaka kutoka kwenye Muungano basi la kwanza ambalo linafanyika ni wao wanaweka tarehe ya siku ya kufungasha virago vyao halafu huku Tanganyika tunaamua tunataka kufanya nini. Kwa sababu hapo hakutakuwa na masuala ya Katiba ya Muungano.
Kama wangekuwa serious kabisa katika kuondoa mikanganyiko ya muungano, hatua hizi unazozipendekeza mzee wangu M. M ni dhahiri kuwa ilikuwa ni vyema zikafuatwa, lakini- kwa makusudi kabisa- hawataki kufanya hili: watu wazima na heshima zao wanaanzisha mchakato wa katiba ya muungano ambao kukubalika kwa muundo wake bado ku mashakani.

Imani kuwa muundo huo wa muungano wananchi wanautaka sijui wanaipata wapi hata waamue kuandaa katiba yake!
 
kweli umenena mwana kwanini Mhe Warioba hapendi kusema kuwa tanzania bara ni watanganyika alikuwa na kigugumizi sana wakati anatoa ripoti yake ya rasimu sijui kwanini jamani ? hapa nimepapenda ndio maana nipaste hivi:

Bila ya kujalisha iwapo muungano baina ya Zanzibar na Tanganyika (Tanzania Bara) utakuwa ni muungano wa mkataba au wa aina yoyote ile, kuna umuhimu kwa upande wa Tanganyika (Tanzania bara) kwanza kuja na Katiba yake iliyokamilika na inayoelezea bayana masuala ya national sovereignty na national identity kama ilivyofanya Zanzibar; Ndani ya katiba hizi ndio lizungumzwe suala juu ya jinsi gani pande zote mbili zinataka kushirikiana na mataifa mengine, ikiwa ni pamoja na nchi shirikishi za muungano – yani Tanganyika (Tanzania Bara) na Zanzibar, kama mataifa huru; Kwa maana nyingine, Muungano wa Tanganyika (Tanzania bara) na Zanzibar) utokane na matakwa ya wananchi wa pande zote mbili, kwa mujibu ya yaliyomo ndani ya Katiba za pande hizi mbili – yani Katiba ya Tanganyika (Tanzania Bara) na Katiba ya Zanzibar; Nje ya hapo, kitendo cha tume ya Jaji Warioba kuja na Katiba ya Muungano bila ya uwepo wa Katiba za pande zote mbili yani – Katiba ya Tanganyika (Tanzania bara) na Katiba ya Zanzibar itakuwa ni kupoteza muda na fedha za walipa kodi, lakini mbaya zaidi, itaimarisha tatizo lililopo badala ya kulitafutia ufumbuzi wenye manufaa kwa nchi shirikishi za muungano;
 
Mkuu ivonya-ngia,

Kwa mujibu wa bandiko lako namba 37 hapo juu, inaelekea kwamba kwa mtazamo wako, Katiba ya JMT (1977) is divine na kwamba ili muungano wetu uendelee lakini pia uimarike, hatuna budi kuheshimu yaliyomo kwenye Katiba ya 1977; Kama nipo sahihi juu ya mtazamo wako, I don't subscribe to that school of thought na badala yake naamini kwamba chanzo cha mgogoro wa muungano wetu ni katiba ya 1977 ambayo bila ya aibu wala kificho ilichakachua makubaliano ya muungano per articles of the union, 1964;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
I come from a background kwamba katiba ya 1977 haikuwa katiba halali kwa maana ya kwamba ilitakiwa iendane na yaliyokuweoo kwenye mkataba wa muungano, 1964 ambapo among other things, lengo lilikuwa ni serikali tatu, sio mbili wala moja; ni kutokana na mgogoro huu ndio maana tumekuwa na mvutano mkubwa juu ya autonomy ya zanzibar kutokana na ubovu wa katiba ya 1977 lakini pia kwa sisi wachache, tumekuwa tunaungana na wanaharakati kama mtikila kudai tanganyika yetu;

Mkuu Mchambuzi

Sawa ni maoni yako na mtazamo wa baadhi ya wananchi kuwa katiba ya mwaka 1977 haikuwa halali on bases ulizozielezea. Lakini tume ingewezaje kuegemea mtazamo huo? Kumbuka tume yenyewe iliyoteuliwa na Rais ni zao la katiba hiyo hiyo, mtoto amkane mzazi wake inabatilisha nini? Kumbuka pia haijapata kutokea in a formal process kwa katiba hiyo ya 1977 kuwa denounced.

A constitutional government haina maana kwamba the government follows the letter of the constitution and the law; pre requisite ya constitutional government ni kwamba the laws themselves lazima ziwe just, fair, equitable, hivyo ndivyo katiba inapata uhalali;

Mkuu unadhani hii inaweza kuipa upenyo Tanganyika kujiunda pasipo kutambuliwa kwanza? Kuanzisha serikali ni jambo zito mno kuifanya hiyo pre requisite to prevail. Kumbuka hii ni restructuring ya mfumo mzima wa nchi. Bado uhalali wake unahitaji kutambuliwa kwanza na katiba. Ningekubaliana na wewe kwamba mpira wa constitution amendment kwa provision husika ya muungano ungetupwa kwanza kwa parliament then tume ya kina Warioba ingeendelea pale parliament ilipoamua. Hakuna namna nyingine ya kubadili uhalali wa hiyo katiba.

kwanini tusubiri maoni ya wananchi juu ya mfumo wa muungano kisha tutunge katiba mpya ya tanganyika?;

Hapa nakubaliana nawe. Ni kweli safari ya mchakato wa katiba mpya ilitakiwa ianze na hili juu ya muundo mzima wa muungano. Raia wa Tanzania kamwe hawajawahi kupewa nafasi ya kuamua si tu hitaji la muungano bali pia mfumo wake. Muungano ndio axis ya katiba ya JMT, pasipo maridhiano katika hili mambo yote yanayozaliwa ni migogoro.

Kwanini mshirika mwingine wa muungano (zanzibar) yeye hakusubiri maamuzi juu ya mfumo wa muungano kujipatia katiba yake? ;

Mkuu, hili ni rahisi kulitambua maana katiba ya JMT iliyopo tayari inazitambua serikali mbili. Ile ya Zanzibar na ile ya JMT. Kwa kuwa tayari Zanzibar inatambuliwa ilikuwa rahisi kwao kuwa na katiba.

Ni katika muktadha huu nimemuuliza mzee mwanakijiji swali kwamba je - in the context of the union btn TG na ZNZ, suala la autonomy ni relative or absolute? Ningependa kusikia maoni yako katika hili;

Nachelea kuwa na jibu la moja kwa moja katika hili Mkuu maana kwangu issue kama ya muungano wa nchi zilizowahi kuonja self sovereignity haiwezi kuwa absolute. Always there will be stages involving discussions kwenda kwenye set vision ambayo pia inaweza kubadilika.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu ivonya-ngia

Kuna baadhi ya hoja zako nakubaliana nawe, lakini kwa sasa naomba nijikite zaidi katika maeneo ambayo naona yana utata zaidi; Je nikitamka yafuatayo, iwapo utapinga, utapinga kwa hoja gani?

Kwanza kwamba kwa miaka karibia 40 sasa, in practice, serikali ya Tanganyika imekuwepo ingawa in theory walio wengi wamepumbazwa haipo - Je unakubali au unakataa kwamba serikali ya Tanganyika kwa ustadi mkubwa inafunikwa na kiini macho cha katiba ya 1977 ambayo imempa rais wa JMT kimazingaombwe kuwa head of states of Tanzania, Tanganyika na Zanzibar? Kwa maana nyingine, je wafahamu kwamba kutokana na kiini macho cha muungano, by default, rais wa JMT pia ni Rais wa Tanganyika in Practice, huku pia akiwa ni Rais wa serikali ya muungano na hali hii ipo tangia mwaka 1964?

Pili, je wafahamu kwamba katiba ya muda ya muungano ilikuwa ni katiba ya Tanganyika ambayo ilifanyiwa maekebisho kidogo kukidhi matumizi hayo kwa muda huku ikiwekwa bayana kwamba tume ya katiba itateuliwa ndani ya mwaka mmoja kushughulikia katiba za zanzibar na ya JMT huku katiba ya Tanganyika ikiendelea kuwepo, na badala yake uchakachuajia wa mkataba wa muungano ukaanza na kupelekea nchi kutawaliwa na katiba ya muda kwa miaka 12 (1965 to 1977) na hatimaye Katiba mpya (1977) ambayo haikuwa na nia njema ya muungano per articles 1964, ikazaliwa (mfano wa uchakachuaji ni kubadilishwa kwa majina ya wazazi wa muungano kutokea tanganyika na zanzibar na kuwa tanzania bara na tanzania zanzibar, vyama vya siasa kuingizwa kwenye katiba kinyume na content ya articles of the union n.k), Unateteaje ubovu huu kwa hoja, hasa iwapo unalenga kujenga hoja kwamba katiba ya sasa (1977) ipo sahihi juu ya suala zima la muungano?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mkuu Mchambuzi

Hapana sikulenga kujenga hoja kuwa katiba ya sasa ipo sahihi juu ya muungano, hoja yangu ililenga kupingana nawe kuwa katiba ya 1977 si halali based on mere words na tume isimame by that view. Ilihitajika kwanza kuwepo institutional decision/declaration kama precedence.

Pia itakuwa ni unafiki mkubwa kusema kuwa muundo wa sasa wa muungano hauna matatizo. Ni kweli kuwa muungano huu umetimiza miaka takribani 49 sasa, lakini ni imara na unaridhisha pande zote? HAPANA. Mambo yanaenda kwa kudra za Mola tu. Kwa maneno mepesi ni kuwa pande mbili za muungano zinaishi kinafiki.

Ni kweli pia haikuwa haki kuiua Tanganyika na kuibakiza Zanzibar. Kama ilionekana ni haki kwa Zanzibar kubaki kwa nini haikuwa hivyo kwa Tanganyika? Kwa nini kuwe na marais wawili? Binafsi kwa muundo wa sasa ni bora twende kwenye serikali tatu ama tuwe na moja tu katu si hizi mbili.

Lakini kama mchangiaji mmoja alivyosema hapa kuwa maoni ya tume ni a form of referendum so ndo mambo uwanjani hivi na tumue sasa juu ya muungano tuutakao ama la tuikatae kabisa referendum hii tuombe kwanza kura ya ama Muungano-NO ama Muungano-YES.
 
Back
Top Bottom