Kwa taarifa zisizo rasmi, kamati kuu ya Chadema katika kikao chake imetoa msimamo kwamba kuna umuhimu kwa Katiba ya Tanganyika kuwepo katika mchakato wa sasa wa katiba mpya ingawa msimamo huo hauna formidable force (badala yake ni kama vile wahusika hawana uhakika kama wanachosema ni kitu sahihi), lakini muhimu zaidi, msimamo huo hauambatani na elimu kwa umma juu ya umuhimu wa katiba ya Tanganyika katika nyakati hizi; Pengine official statement ya chama italiweka suala hili wazi zaidi;vinginevyo niseme tu kwamba upatikanaji wa katiba ya Tanganyika is a political process, hivyo wananchi hawana option nyingine zaidi ya kutegemea chama cha siasa kufanikisha hili; sasa iwapo mwananchi ni mwana ccm au chama kingine chochote ambacho hakina msimamo wa serikali tatu, mwananchi huyo hana budi kuunga mkono msimamo wa chama kitakachojitokeza kupigania haki hii muhimu kwetu watanzania bara?!; na kwa sasa, chama chenye mwelekeo huo ni chadema, kinachohitajika ni a firm position na elimu kwa umma juu ya umuhimu wa suala hili ili harakati hizi ziungwe mkono kwa ufanisi zaidi;
Bila ya Tanganyika, Tanzania haikuwezekana na bado haiwezekani;
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums