Kwa maoni yangu,the best way ni kuwa na kura ya maoni kwa Zanzibar na Tanganyika separately. Hiyo inamaanisha utambuzi wa Tanganyika kwanza.
Halafu ndiyo tujue kama tutakuwa nchi moja (serikali moja au tatu), au nchi mbili tofauti..
Katiba ya baada ya uhuru inaweza kutumika kama katiba ya Tanganyika.
Muungano utakuwepo ikiwa pande zote mbili zitahusishwa na zitakubali.Mkuu Kobello,
Karibu katika mjadala; nakubaliana na wewe kwamba kila pande za muungano zifanye separate referendums;ningependa kujua mtazamo wako lakini katika hili kwamba je - iwapo matokeo ya pande zote mbili yatapishana, tunafanyaje hapo?
Vile vile naungana nawe katika hoja kwamba Katiba ya Tanganyika (1962) iendelee kuwa katiba ya Tanganyika pengine baada ya marekebisho ya hapa na pale kukidhi mahitaji ya nchi katika dunia ya leo; vinginevyo the fact kwamba katiba ya tanganyika (1962)ilifanywa kuwa katiba ya muda ya muungano baada ya a few amendments maana yake ni kwamba ilikuwa ni Katiba bora na sio bora katiba (kama ya 1977) kwani pande zote mbili ziliona inafaa for starters;
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Referendum ya pande mbili kwa kweli itakuwa ni kitu very challenging, ndio maana wengi wasiopenda kutumia muda mwingi kufikiri hadi jibu lipatikane wanaona ni bora referendum ya upande mmoja iwe ndio mwamuzi;Muungano utakuwepo ikiwa pande zote mbili zitahusishwa na zitakubali.
Siyo pande moja au pande sifuri.
Mkuu kobello, kwa hili la umuhimu wa katiba ya tanganyika to legalize our identity na sovereignty kwa ajili ya referendum ni hoja ya msingi sana ambayo nadhani hata tume ya warioba wakiisikia wataumia sana vichwa;Katiba ya '62 ni kianzio, ili kulegalize sovereignty yetu kwa ajili ya kura ya maoni.Mfumo wa Serikali ungeundwa baada ya kura ya maoni, ili kukidhi maslahi ya Tanganyika.
Mimi naona njia hii ndiyo sahihi.
Referrendum ya upande mmoja haiwezi kuwa mwamuzi. Tatizo ni kudharau maoni ya watanganyika, as if we are not as civilzed, to judge our own destiny bila kushurutishwa. Hili ni kosa kubwa wanalofanya wanasiasa.Referendum ya pande mbili kwa kweli itakuwa ni kitu very challenging, ndio maana wengi wasiopenda kutumia muda mwingi kufikiri hadi jibu lipatikane wanaona ni bora referendum ya upande mmoja iwe ndio mwamuzi;
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Hata viongozi au wawakilishi wetu wanaogopa ile kitu inaitwa "Central committee" ya vyama vya siasa. Hizi "Central committees" ndizo zinazoumiza kwa njia ya mbinyo demokrasia kwa watanzania. Na hazina nguvu yeyote kikatiba, ingawa wengi humu hufikiri tofauti (nina jina baya sana kwao).
Na kuna dalili kwamba matakwa ya walio wengi kuhusiana na muungano nayo yatadharauliwa the same way;Hatukutaka vyama vingi, tukadharauliwa na matokeo yake ndiyo tunayaona.