HOJA NDANI YA HOJA: Rais Magufuli na bahati nasibu ya korona - ITALIPA?

Alisikika kiongozi wa chama fulani na hivi punde anataka kugombea nyadhifa fulani ndani ya nchi iliyojaa asali na maziwa.Mkuu vifo vyetu havishabihiani na corona tutasubiri malaria, njaa na kipindu pindu.Tupige kazi dr.john Pombe Magufuli.
 
waki tulockdown na sisi tutawafungia wasije huku halafu tuone nani atapata hasara
 
Mwache rais wetu musimchanganye akili mzigo alionao unamtosha sana. Hiyo lockdown mnayoisema yaweza kuwa muhimu lakini wenzetu wamefanya hivyo na wana uwezo wa kugawa chakula nyumba kwa nyumba. Naendelea kusisitiza kwamba maisha yetu in korona tosha mh. Rais aliposema tumwombe Mungu namuunga mkono. Sisi njaa itatuua kuliko korona.
 
I firmly believe, the worse part is over. Kama kuambukiza kungefanana na Europe au Marekani, sijui ingekuwaje.
 
Takwimu za DRC umepotosha maksudi au vipi? maana mpaka sasa wana wagonjwa 51 na vifo 3.
Pia sijajua kwa nini hujazigusia Burkina Faso yenye maambukizi 152 na vifo saba, Ghana maambikizi 136 na vifo 4, Senegal yenye maambukii 105, Ivory Coast 96, Cameroon 88 na vifo 2, Tuombe tu kwamba base ya virusi isitanuke maana ikitanuka maambukizi yanaana kuongeeka exponentially.
 
Kikubwa ni kufuata maelekezo ya wataalamu wa afya na kumuomba mungu!

Sent using Jamii Forums mobile app
Wataalamu waliobobea wanasema, pima, pima, pima, pima - anayegundulika atapelekwa kwenye isolation - sisi tunafanyaje? Watu wanajipeleka Muhimbili kupimwa waziri anasema walirudishwa hadi wawe na hali mbaya - hawakupimwa. Wataalamu wanasema punguza misongamano - sisi tunafanya nini! Wataalamu wanasema watu wapungue mitaani ili kudhibiti maabukizo - sisi tunafanya nini! kazi tu!. Kwani huko kwingine Mungu hayupo au hawamuombi?
Nashindwa pia kujua mwongo nani - Makonda alituambia mtoto wa Mbowe ana Corona, Mbowe akathibitisha kuwa ni kweli na akasema mwanae hajasafiri kwenda nje ya nchi, lakini waziri anasema kesi zote ni za kutoka nje, hakuna maabukizi ya ndani! Hakika mficha ficha maradhi kilio humfichua. Tuseme kweli, tukizidiwa wenye uwezo watusaidie
Tutakapoanza kupukutika kama majani sijui tutaficha wapi nyuso zetu. China walipuuza hadi yule daktari aliyewaambia wakataka kumuweka ndani - walipokuja kukubaliana nae it was late. Italia watu waliendelea kuwa kwenye vilabu, ulipokuja kulipuka - niliona kiongozi wao akilia kabisa akisema tumefanya kila tunaloweza lakini tatizo halipungui - tunasubiri msaada kutoka juu! Marekani Trump alichukulia poa hadi kusema ni chinese virus, akasema gharama ya kufunga uchumu ni kubwa kuliko corona, leo hii Marekani ina wagonjwa wengi kuliko hata ilivyotokea China Na Trump - soon atatokwa machozi ya Mamba!
Sisi tunafanyaje - chapa kazi tu mambo ya corona ni poa tu! POA TU!!!

Tumuombe Mungu lakini tusimdhihaki maana hata Malaria tunawasikiliza wataalamu, tunaenda hospitali!
 
Kwa nature ya maambukizi yalivyo ni mwendawazimu pekee anayeamini data za serikali.

1.Kwanza, wanaripoti wale waliowapima, hawaripoti wasio wapima

2. Pili hata hao waliowapima mostly likely wanaundereport hii ni kutokana na ego ya bwana mkubwa kumess up kutochukua hatua mapema. Na kwa jinsi inavyoonekana hii kitu iko underreported 10 times
Mimi wakiniambia kuna cases 12 wanazozijua mimi nazidisha na 10, maana yake ni cases 120 wanazozijua.

Kudanganya data kuna matatizo makubwa nako ni kuwafanya watu warelax

Huyu bwana mkubwa afunge mipaka, hana uwezo wa kuenforce karantini ya siku 14 huku akiwa na uhakika kuwa hakutakuwa na violation.

Just imagine kawaachia wachina kuingia nchini miezi yote ile ya mlipuko, leo Wachina wameamua kutufungia vioo kwa kufuta residence permit za wageni wote bila kujali taifa gani liliwapokea kipindi wanahaha.

Stubborness ya mtu mmoja itaangamiza Taifa, Baraza la Usalama la Taifa inabidi limkatalie huyo mzee kwa kumwambia bila woga kuwa measures zake zimekaa kihatari mno.

Kikubwa sasa ni Kufunga hiyo mipaka
Zuia mikusanyiko isiyo ya lazima na iincourage watu waliokatika vyombo vya usafiri kuvaa mask badala ya kuzipiga vita mask, kuvaa mask kwenye mikusanyiko ni muhimu maana hujui nani kaambukizwa
 
Mzee hapo kwenu mnabaraza la usalama la taifa?

Nilijua wapo hao jamaa tu lakini hawana mchango wa kisheria to define their roles the nation in a compatible way.

Sijui

Hoja ndani ya hoja?

Nchi yetu sijui km ni salama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nnachoona ni upuuzi wa kutojali afya za watu
Huyu mtu alisema ata wapige mbizi lazma ndege ya raisi inunuliwe
Kwani serikali ndo imeleta tetemeko,mchango akutia ndani

Kwa hii mifano michache uraisi wake ni wa kutukuka zaidi ya maisha ya yeyote
Haimwingii akilini kuona watu hawazalishi sababu ya Corona
Yawezekana kwa ugumu ama bahati ugonjwa huu usiwadhuru wengi wa jamii ya kiTz
Lkn huyu bwana anayejifanya kuwakandia kwetu mabeberu anatia haya sababu ya kuwagomea watabibu
Endapo hatutakua waangalifu kwa afya za wageni na kuhakikisha wako mazingira salama ni mwekezaji gani atabaki

Corona imekua zaidi ya ugaidi
Ana mawazo ya ubinafsi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anategemea sana wawekezaji na kwao hii hali si salama
Ana washauri wasio na njia mbadala
Kwa huu mwenendo wake atakosa mengi mno
Tanzania ni yetu ,kushindwa ikitokea ni kwa wote
Lkn lawama zitakua juu yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Italy, Spain, USA na na mataifa mengine makubwa kiuchumi yanakumbwa na upungufu wa vitu muhimu kama Ventilators sembuse sisi wa dunia ya tatu.

Mungu ni mwema siku zote na katika hili janga ameamua kulilinda bara letu la Afrika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…