HOJA NDANI YA HOJA: Rais Magufuli na bahati nasibu ya korona - ITALIPA?

Umedadavua vr sana mkuu nimekuelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu huo ndio ukweli, ila hawataki kuukubali, jamaa kaangalia Hali ya kipato Cha mtanzania na halingumu ya maisha akaona nibora ajifunge bomu shingoni likilipuka kilamtu atajuwa Ni jinsigani ya kujiokoa
 
Siku hizi umepatwa na nini???
Maana unajikopa. Mpaka aibu jiwe ana bahati ipi sasa hapa???


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisi ligi yetu ni Burundi na Sudan Kusini kwa kila hali.

Tumekwishatoka kwenye kundi la nchi nyingi kama hizo ulizoorodhesha hapo.

Hii ndio Tanzania yetu ya leo.

Sasa, niseme tu, siku hizi napata shida sana kusoma makala hizi ndefu ndefu zenye mizunguko.

Hapo nilipoishia, "Bahati Nasibu" ilikuwa bado kabisa..., sasa sijui bahati nasibu gani inayomsubiri!

Nitasoma michango ya wengine huko chini, labda kuna jibu la swali langu!
 
Mweeh.. hivi kusoma nako ni kugumu; mbona sijasema wameamua? Mjadala upo ndiyo upo na usishangae ukapamba moto ndani ya wiki mbili zijazo.
 

Kuna factors mbalimbali kwenye kila nchi na kundi la watu; objectivity haina maana kila kitu kiko sawa. Dishonest ni kujikuta "crying wolf" ili kuwatisha watu wapanic kila linapotokea jambo dogo au ambalo si kubwa kivile.. mwisho wa siku tutajikuta tunalia "wolf" na watu wasisikillize tena.
 
Mmk tatizo kubwa ni uwaxi

Mmk tatizo letu accurate information. Je data tunazopewa ni sahihi?
Mbeya, dom tayar kuna wagonjwa na hawajaripotiwa bado
Jamani, mbona taarifa za ugonjwa ndiyo ziko hivi? wagonjwa wanapimwa, vipimo vinapelekwa kupata matokeo.. matokeo yakija ndio namba zinakuwa adjusted. Hili ni kweli hata hapa na mara nyingi matokeo yanakuwa nyuma ya siku kulinganisha na muda waliopimwa. Ndio maana unaona leo Marekani ina wagonjwa wengi kweli kweli. Kubwa ni vipimo. Sasa inawezekana kabisa wagonjwa wameongezeka lakini matokeo ya vipimo bado hayajatoka.. nchi nyingi bado hazijaweza kupima hapo hapo na kutoa matokeo hapo hapo. Huko si kuficha ndio hali halisi.
 
Asante, kumbe nimeeleweka... nilidhani labda niliandika kwa Kigagagigikoko...
 
Bado sidhani kama umenipata; bado ugonjwa haujalipuka Afrika kama watu walivyokuwa wanahofia ukiondoa Afrika ya Kusini...
 
Kwa nature ya maambukizi yalivyo ni mwendawazimu pekee anayeamini data za serikali.

1.Kwanza, wanaripoti wale waliowapima, hawaripoti wasio wapima

Sasa unaweza vipi kuripoti usiowapima?

Hizi ni hisia tu...
 
Hili huwa linanishtuaga; na wasipokufa 'sana'?
Mkuu tunaviongozi wengi ambao huamini kwamba wakisema kitu hakuna challenges kutoka Kwa wanao waongoza, wanajiona wako juu kuliko wengine wote

Kumbe sifa ambayo wengi wameikosa ni Ile Hekima ya kutamka nini na Kwa Wakati gani na mahali gani

Huwezi mtu ukawa ni wa kujitamkia tu bila kupima Kwanza unachokitamka,

Viongozi wa Aina hii ni hataree na hawafai, huwezi kuwatakia kifo Watanzania, ni kukosa hekima
 
Mweeh.. hivi kusoma nako ni kugumu; mbona sijasema wameamua? Mjadala upo ndiyo upo na usishangae ukapamba moto ndani ya wiki mbili zijazo.

..Bahati nasibu siyo neno sahihi.

..Neno ulilopaswa kutumia ni KAMARI / GAMBLE.

.. sidhani kama Tanzania ina CAPACITY [ vifaa, wataalamu, fedha, miundombinu] ya kupima, kuhifadhi, na kuwatibu waathirika.

..pia MFUMO wa maisha ya waTz hauruhusu kuchukua hatua ngumu za kujikinga [ isolation, social distancing, lockdown] na hatari ya mlipuko wa Corona.

..Kwa hiyo Raisi kusisitiza kwamba tumuombe MUNGU atuepushe na janga la Corona amekuwa mkweli. Serikali haina uwezo wa ku-deal na tatizo hili. Na hata wajomba / mabeberu ambao wangeweza kutusaidia na wenyewe wameelemewa.
 
Namuomba Mungu atuepushe na lolote kati ya hizo bashiri zako zote mbili Mkuu Mwanakijiji kwa sababu mbili muhimu.

BAHATI NASIBU IKIFANIKIWA
Haina haja ya kuwa na furaha ndani ya nyumba yako ilihali jirani zako wote wameshika tama.

BAHATI NASIBU IKIBUMA
Askari akifia vitani hahesabiwi kama msaliti bali mzalendo, Dr. Magufuli akishindwa vita hivi atakua ni Askari aliyefia vitani hivyo kiungwana heshima yake itabaki pale pale.

MY TAKE
Swali ni je! Nchi kama Uganda walifunga mipaka kabla hata ya ugonjwa kuingia mhona sasa nao wanazo kesi za COVID - 19?

Italia pamoja na kuwa miongoni mwa nchi za ulimwengu huo wa kwanza mbona imefikia wakati Waziri Mkuu kanyosha Mikono kusalimu amri?

USA, UK, IRAN na kwengimeko pamoja na kuchukua kwao extremely measure kujikinga na ugonjwa huu mbona wana maambukizi mengi zaidi?

KWA UJUMLA WATU TUPIGE GOTI TUMWOMBE KARIMA ATUEPUSHE NA GONJWA HILI KWAKUA JITIHADA ZA MWANADAMU HAZIZIDI KUDRA.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bado sidhani kama umenipata; bado ugonjwa haujalipuka Afrika kama watu walivyokuwa wanahofia ukiondoa Afrika ya Kusini...
ni kweli haujalipuka ila tahadhari za kiafya zilitakiwa zichukuliwe mapema kuliko kucheza na bahati nasibu. Kwa tabia ya ugonjwa huu ongezeko huanza taratibu sana na ghafla hupanda pale ambapo hamtegemei. DRC walikaa na case zao 3 kwa zaidi ya wiki tatu, ilipoanza kupanda ndo hiyo imekwenda kwenye 51 na vifo. USA the same hivi sasa wanazungumia maambukizi zaidi ya 17000 kwa siku. Hivyo tusione kama tuko unique sana kuliko wazungu na kuendeleza ukawaida wetu
 
ASILIMIA KUBWA YA WATANZANIA NI MASKINI WA KUTUPWA, AKITOKA NJE ANAENDA KUTAFUTA CHAKULA CHA KULA SIKU HIYO PAMOJA NA ASUBUHI IFUATAYO IKIWEZEKANA, SASA ASIPOTOKA NJE KWENDA KUTAFUTA UJUE ATASHINDA NJAA SIKU HIYO.
UNATAKA RAIS AZUIE WANANCHI WAKE WASITOKE NJE KUTAFUTA CHAKULA ILI WAISHI WEWE UTAKUWA NI MCHAWI, UNA UBINAFSI WA MOYO WAKO. RAIS ATAANGALIA NAMNA NYINGINE AMBAYO ANAONA ITAFAA ZAIDI KWA WATU WAKE, NA ATAWASIHII WATU WAKE WAMTEGEMEE MUNGU KWA IMANI ZAO HUKU NAYE AKIJITAHIDI KUTAFUTA JIBU LA UHAKIKA LA KUDHIBITI GONJWA HILO.

NAMPONGEZA RAIS WANGU, MUNGU AMLINDE NA AMBARIKI. MUNGU AKIMLINDA RAIS NA AKAMBARIKI ITAKUWA NI NEEMA KWA WANANCHI AWAONGOZAYE AMEEN!!
 
Tusaidie mkuu, Je, kwenye ukoo wenu kunaaliye na maambukizi?

Na ole useme hakuna, maana yake ungependa uone maambukizi yakizidi kuenea Kwa wengine tu Ila sio kwenu??
Unataka kuona Serikali ikiendelea kuripot ongezeko la wagonjwa ambalo miongoni mwao ukoo wenu hakuna?

Ukiwa mpinzani kwani ni lazima ujivike ushetwani?

Kama kwenye ukoo wenu hakuna hata mmoja aliyeathirika,unataka waongezeke kutoka wapi sasa?😉
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…